Haki za wakimbizi zinalindwa na sheria za kimataifa, lakini nini kinatokea kiuhalisia?

Bahadin M Qadr alitoroka eneo la Kurdistan huko Iraq baada ya kuponea kifo katika jaribio la mauaji dhidi yake.

Huko Denmark, wazazi wakongwe wa Mahmoud Almohamad wameambiwa lazima warudi Syria,mikononi mwa utawala wa Assad.

Roseline - ambaye jinalake limebadilishwa - alinusurika katika safari ndefu kupitia Amerika Kusini, Amerika ya Kati na Mexico survived a month-long journey through South America, Central America and Mexico, lakini akaishia kurejea katika nchi aliyotoroka miaka kadhaa iliyopita.

Umoja wa Mataifa unasema watu milioni 26.6 duniani wanachukuliwa kuwa wakimbizi. Walilazimika kutafuta usalam mbali na nyumbani na haki hiyo ya kimsingi inatambuliwa - kuthibitishwa na Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.

Lakini wakimbizi wengi hawaoni haki zao kuheshimiwa. BBC ilizungumza na watu watatu wanaokimbia vita, mateso ya kisiasa na ufukara kuhusu utafutaji wao hatari wa usalama.

'Walinitoa nje na kujaribu kuniua'

"Nilitoka nje nikiwa nimevalia nguo za kulalia. Waliniburuza chini na kujaribu kuniua kwa kisu," anasema Bahadin, akizungumza na BBC kutoka kambi ya muda katika wilaya ya Grodno huko Belarus, ambako halijoto ya majira ya baridi ni chini ya baridi.

Yeye ni mmoja wa Wakurdi wengi wa Iraq wanaokabiliana na mazingira kwenye mpaka wa Belarus na Poland, akijaribu kutafuta hifadhi katika Umoja wa Ulaya au Uingereza.

Bahadin anasema jaribio la kumuangamiza lilifanyika Septemba 2020 mbele ya nyumba yake mjini Sulaymaniyah, kaskazini mwa Iraq.

Bahadin ambaye ni mkosoaji wa uongozi wa sasa wa Wakurdi, analaumu makundi yenye uhusiano na serikali kwa shambulio hilo.

Alipata jeraha kubwa karibu na moyo wake na alikuwa na bahati ya kuishi. Mkewe na watoto wake wanne bado wanaishi Sulaymaniyah.

"Wametuchosha [serikali]. Tunataka waondoke ili turejee Iraq. Hiyo ndio simulizi ya kusikitisha ya kwa nini tuliondoka nchini mwetu," anasema Bahadin.

Lakini muungano wa Ulaya (EU) imewazuia wahamiaji hawa kuingia eneo lao ikilaum Belarus kwa kiwaelekeza watu mpakani ili kuanzisha mzozo mpya wa wakimbizi.

Mvutano huo umemuacha Bahadin na wenzae wengi katika njia panda.

"Walilia na sikuweza kufanya chochote"

Familia ya Mahmoud Almohamad iliwasili Denmark mwaka 2015 baada ya kukimbia vita nchini Syria.

Alihitimu kutoka shule ya upili mapema mwaka huu akiwa na umri wa miaka 20, na kupewa nafasi ya kusomea udaktari katika chuo kikuu. Mambo yalikuwa mazuri.

Lakini serikali ya Denmark ikaamua kwamba ilikuwa salama kwa wakimbizi kurejea Syria. Tangu mwaka wa 2019, imebatilisha kibali cha makazi cha Wasyria 174 kati ya takriban 35,000 iliyowakaribisha

Wazazi wa Mahmoud, Suhil and Dalal, walikuwa miongoni mwa wale ambao wanatakiwa kurejea makwao ijapokuwa watoto na wajukuu wao wanaruhusiwa kuishi Denmark.

Mahmoud anasema uamuzi huo ulivunja moyo familia yake.

"Walisikitika [wazazi] sana," aliambia BBC. "Nilipowaacha Sjaelsmark [kituo cha kurudi] walilia na kulia, na sikuweza kufanya lolote."

"Natamani ningekuwa nao, lakini nina kazi, naenda kusomea udaktari, nina mambo mengi sana ya kufanya."

Msongo wa mawazo umekuwa mkubwa kiasi kwamba, siku ambayo wanatakiwa kufika kituo cha kurudi, mama yake na dada yake walizirai na kulazimika kupelekwa hospitali. Wahudumu wa afya walimfanyia binti yake CPR ya dharura.

Cha kushangaza ni kwamba, Denmark haiwezi kuwarudisha wakimbizi Syria kwa sababu haitambui utawala wa Assad na haina makubaliano nao.

Hiyo ina maana kwamba watu kama wazazi wa Mahmoud wanakabiliwa na kukwama kwa muda usiojulikana katika kituo cha kurudi hadi "wachague" kwa hiari yao kurejea Syria.

Mahmoud anasema wazazi wake wanahisi "kusalitiwa" na serikali ya Denmark.

"Walipokuja hapa na watoto wao, walihisi kuwa wamefika katika nchi inayoheshimu haki za binadamu. Lakini sasa wanahisi kama wametapeliwa na Denmark, kwa sababu Denmark iliwachukua watoto wao kutoka kwao," anasema.

"Watoto wanasoma na kufanya kazi kwa ajili ya [manufaa ya] Denmark, lakini sio wazazi wao. Wazee na ni wagonjwa na hivyo tunaweza kuwarudisha."

'Sio salama'

Mashirika kama Amnesty International na Human Rights Watch yanasema Syria "si mahali salama" pa kuwarejesha wakimbizi, kwani wapinzani wa kisiasa wa serikali ya Assad bado wanafungwa jela na kuteswa.

Watu waliokimbia nchi, kama babake Mahmoud, afisa wa zamani wa jeshi, wana uwezekano wa kuchukuliwa kama wasaliti ikiwa watarejea, kulingana na mashirika hayo.

"Utafiti wetu unaonyesha kuwa wakimbizi wote wa Syria wanaorejea wako hatarini kukumbwa na vifungo, kuteswa, kubakwa, kupotea na hata mauaji ambayo yanafanywa na vyombo vya usalama vya Syria na idara ya ujasusi," alisema Dan Hindsgaul, Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Amnesty International Denmark.

"Kutaka kurudisha watu kwenye hatari kama hiyo ni kinyume na wajibu wa haki za binadamu wa Denmark."

Serikali ya Denmark iliambia BBC kwamba tathmini ya hali ya usalama nchini Syria inafanywa na mamlaka huru kulingana na takriban ripoti 1,400, ambazo zinafanyiwa ukaguzi kila mara. Kila uamuzi unazingatiwa kikamilifu.

Inasema wale ambao wanatambuliwa kuwa hawako hatarini ikiwa watarudi nyuma wanahifadhiwa katika vituo vya kurudi kwa gharama ya Krone 300,000 za Denmark ($45,700) kwa mwaka, pesa ambazo zingeweza kutumika badala yake "kusaidia wakimbizi wanaohitaji msaada na ulinzi". Denmark ni mojawapo ya nchi chache zinazotoa msaada huo, inasema.