Omicron: Tunafahamu yapi kuhusu aina hii mpya ya kirusi cha Corona?

Chanzo cha picha, Getty Images
Tumerudi eneo tunalolifahamu - wasi wasi unao ongezeka kufuatia kirusi kipya cha corona.
Kirudi cha hivi punde ndicho kimejifanyia mabadiliko makubwa kilichogundiliwa hadi sasa na kina mabadiliko ambayo yameelezwa na mwanasayansi mmoja kuwa yaliyo ya kutisha, huku mwingine akiniambia kuwa ndiyo aina mbaya zaidi ya kurusi walichowai kukiona.
Ni mapema na kesi nyingi zilizothibitishwa ziko jimbo moja nchini Afrika Kusini lakini kuna dalili huenda kimesambaa zaidi.
Wakati huo huo kuna maswali kuhusu kwa kasi gani kirusi hicho kinaweza kusambaa, uwezo wake wa kukwepa kinga iliyotokana na chanjo na kipi kitafanywa.
Kuna uvumi mkubwa lakini kuna majibu machache sana.
Kwa hivyo ni kipi tunachojua?
Kirusi hicho kimepewa jina Omicron na shirika la Afya Duniani kutokana na muundo wa majina ya msimbo ya kigiriki kama vile virusi vya Alpha na Delta.
Kinajifanyia mabadiko makubwa sana. Prof Tulio Oliveira kutola kituo cha kushughulikia ,ajanga nchini Afrika Kusin anasema kuna tofauti kubwa na virusi vingine ambavyo vimesambaa.
"Kirusi hicho kilitushangaza, kilipata mabadiliko makubwa na mengine mengi tulioyatarajia.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Prof de.Olberita alisemakulikuwa na mabadiliko 50 kwa jumla na zaidi ya 30 kweneye kiungo cha protini ambacho ndicho lengo la chanjo nyingi.
Kiwango hiki cha mabadiliko kimeonekana kwa mgonjwa mmoja ambaye hakuwa na uwezo kwa kukishinda kirusi hicho.
Mabadiliko mengine hayamaanishi ni mabaya, kilicho muhimu ni kuelewa ni kipi mabadiliko hayo yanafanya.
Wasi wasi ni kwamba kirusi hicho ni tofauti na kile cha kwanza kilichoibuka Wuhan China. Ikimaanisha chanjo zilizotengenezwa kukinga dhidi ya kirusi cha kwanza huenda zisiwe na ufanisi.
Baadhi ya mabadiliko yameonekana awali kwa virusi vingine, ambayo yanayotoa ishara ya kuhusika kwa kirusi hiki.
Kwa mfano N501Y kinaonekana kuharakisha kusambaa kwa kirusi cha corona. Kuna baadhi yao zinazofanya iwe vigumu kwa kinga ya mwili kutambua kirusi na inaweza kuchangia chanjo kutokuwa na ufanisi lakinia pia kuna vingine ambavyo ni mpya kabisa.
Prof Richard Lessells kutoka chuo cha KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini anasema kuna wasi wasi kuwa kirusi hiki kina maambukiazi makubwa, kuna uwezekano wa kusambaa kutoka kwa mtu kwenda kwa mwingine lakini kinaweza kukwepa kinga.
Kuna mifano mingi ya virusi ambavyo vinaonekana kuwa vinatisha kwa karatasi lakini hukuja kuwa bure. Kirusi cha Beta kilizua hofu miongoni mwa watu mwanzoni mwa mwaka kwa sababu kilikuwa kinakwepa mfumo wa kinga ya mwili. Lakini mwishowe ni kirusi kinachosambaa kwa kasi cha Delta kilichozua msukosuko duniani.
Utafiri wa kisayansi kwenye mahabara ndio utatoa picha safi, lakini majibu yatakuja kwa njia ya haraka kwa kukifuatilia kirusi kinaposambaa.
Bado ni mapema kufanya mamuzi lakini tayari kuna dalili zinazozua hofu.
Kuna visa Zaidi ya 100 ambavyo vimethibitishwa katika mkoa wa Gauteng nchini Afrika Kusini, visa vinne nchini Botswana na kimoja Hong Kong kinachohusishwa moja kwa moja na safari kwenda Afrika Afrika Kusini, Israeli na Ubelgiji nazo zimeripoti visa.
Lakini kuna dalili kuwa kirusi hicho kimesambaa hata zaidi,.
Aina hii ya kirusi kinaonekana kuwa na matokeo yanayoweza kutumiwa kukifuatilia bila ya utafiti wa kijenetiki.
Ikimaanisha kuwa asilimia 90 ya visa huko Gauteng huenda ni vya kirusi hiki na huenda tayari kipo katika mikoa mingi nchini Afrika Kusini.
Lakini hii haituonyeshi kuwa kinasambaa kwa haraka kuliko kile cha Delta, ni hatari zaidi au ni kwa kiwango gani kinaweza kukwepa kinga inokanayo na chanjo.
Haituonyeshi ni kwa njia gani kirusi hiki kitasambaa katika nchi ambapo asilimia kubwa ya watu wamechanjwa zaidi ya asilimia 24 ya watu nchini Afrika Kusini ambao sasa wamepata chanjo yote.
Kwa sasa tumebaki na kirusi kinachozua wasiwasi na kinachostahili kufuatiliwa kwa karibu na kinachozua maswali ya ni kipi kifenye na lini. Funzo kutoka janga hili ni kwamba huweza kusubiri kila wakati hadi pale utakapokuwa na majibu yote














