Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Meta: Kampuni ya facebook yabadilisha jina
Facebook imebadilisha jina lake la kampuni na kujiita Meta ikiwa ni mpango wake wa kujiimarisha sokoni.
Kampuni hiyo imesema ni heri kuweka huduma zake katika sehemu moja ili kuwavutia wateja zaidi katika mitandao ya kijamii katika vitengo vya uhalisia ulioigwa {Virtual Reality}.
Mabadiliko hayo hayatashirikisha mitandao ya watu binafsi kama vile facebook , Instagram na Whatsapp isipokuwa kampuni inayomiliki huduma hizo tatu..
Hatua hiyo inajiri kufuatia msururu wa habari zinazoipatia sifa mbaya Facebook , zinazotokana na nyaraka zilizovujishwa na wafanyakazi wake wa zamani.
France Haugen ameishutumu kampuni hiyo kwa kuzingatia sana kuhusu 'faida badala ya usalama wa wateja wake'.
Mwaka 2015, Google ilibadili jina la kampuni yake na kujiita Alphabet, hatahivyo jina hilo halijatambulika.
Mmimiliki wa Facebook Mark Zuckerberg alitangaza jina hilo jipya wakati alipokua akizindua mipango ya kujenga "metaverse" - ulimwengu wa mtandao ambapo watu wanaweza kushiriki katika michezo, kufanya kazi , kuwasiliana katika mazingira yalioigwa na yasio na uhalisi kwa kutumia vitoa sauti vinavyovaliwa katika kichwa.
Amesema kwamba chapa iliopo haiwezi kuwakilisha kila kitu tunachofanya hii leo, sio tu katika siku zijazo na hivyobasi kuhitajika mabadiliko.
'Kwa muda sasa, natumai kwamba tutaonekana kama kampuni ya Metaverse na nataka kuongoza kazi yetu na utambulisho wetu katika kile tunachojenga' , aliambia mkutano uliofanyika katika video.
'Hivi sasa tunatazama na kuripoti kuhusu biashara kama kampuni mbili tofauti , moja ikiwa familia yetu ya programu na nyengine kuhusu kazi yetu katika mitandao tofauti katika siku zijazo'.
'Katika hilo ni wakati kupata chapa mpya ya kampuni ili kujumuisha kila kitu tunachofanya , ili kuonesha sisi ni akina nani na kile tunachotumai kujenga'.
Kampuni hiyo pia ilizindua nembo mpya katika makao yake makuu katika eneo la Menlo Park , California siku ya Alhamisi, ikibadilisha nembo yake ya thumbs-up "Like" na umbo la rangi ya buluu.
Bwana Zuckerberg alisema kwamba jina hilo jipya litatafakari nembo hiyo wakati unapokwenda, na kwamba wateja hawatahitaji kutumia facebook kutumia huduma nyengine za kampuni hiyo.
Jina Meta linatoka kutoka katika neno la Kigiriki 'meta' ikimaanisha 'zaidi'.
Kwa mtu kutoka nje , metaverse inaweza kuonekana kama mtindo mwengine wa VR lakini wengine wanaamini huenda ikawa ndio mpango wa siku zijazo wa intaneti.
Badala ya kuwa katika Kompyuta , watu katika metaverse watatumia Headset kuingia ulimwengu usio halisi na kuunganishwa katika mazingira yote ya kidijitali.
Inatumainiwa kwamba ulimwengu usio halisi wa VR huenda ukatumika kwa chochote kuanzia kufanya kazi , kucheza michezo pamoja na kujiunga na matamasha hadi kuwasiliana na marafiki na familia. Facebook imesema kwamba inalenga kuanzisha kuuza hisa zake chini ya jina jipya la MVRS kuanzia tarehe mosi Disemba.
Nyaraka zilizovuja
Kampuni hiyo imeshambuliwa mara kadhaa na kuharibu sifa zake , huku gazeti la Washington post hii leo likiripoti kwamba facebook ilizuia habari muhimu kuhusu chanjo kutoka kwa waundaji wa sera zake wakati wa mlipuko wa virusi vya corona.
Ilikuwa habari mpya katika msururu wa nyaraka za siri zilizovujishwa na mfanyakazi wake wa zamani Bi Haugen kwa vyombo vya habari.
Miongoni mwa vitu vingine , ripoti hizo zimedai kwamba facebook ilishiriki katika utafiti ulioonesha kwamba Instagram ilikuwa ikidhuru afya ya akili ya vijana na ilishindwa kuondoa matamshi ya chuki katika mtandao wake nje ya Marekani.
Bwana Zuckerberg ametaja ripoti hizo kama juhudi za ushirikiano ili kutumia nyaraka zilizovuja ili kuchafua jina la kampuni hiyo ".
Uchambuzi wa James Clayton
Mwanahabari wa teknolojia Marekani ya kusini
Kujaribu kupatia jina kampuni ni hatua ngumu . Zuckerberg anasema kwamba alichagua jina Meta, kwasababu ya maana yake Kigiriki.
Lina maana ya Metaverse , mtandao usio halisia VR ambao anataka kuujenga.
Hizi hapa ndio sababu kwanini Facebook , huenda itapata taabu ya kila mtu kuwaita Meta.
Kwanza , hatua hiyo inaonekana kana kwamba facebook inataka kujiondoa katika vichwa vya habari ambavyo vimekuwa vikiiharibia jina.
Wakosoaji wanaamini Facebook imefanya hivyo kwasababu nembo yake imekuwa sumu. Tayari tumeona maseneta wakipuuza mabadiliko ya jina hilo huku mmoja wao akitaja hatua hiyo kama ya 'kujificha'.
Pili, Metaverse bado haipo. Zuckeberg alitaka kusisitiza kwamba ulikuwa mpango wa muda mrefu. Hivyobasi kuwa na jina ambalo halifanani na huduma zako ni kitu cha kushangaza . mapato yote ya Facebook yanatoka kutoka Facebook na Instagram.
Tatu, tunajua kwamba nembo nyengine kuu zimefeli. Kufikia sasa hakuna mtu anayeita Google ''Alphabet'',Jina ambalo ilijiita 2015.
Kile kilicho wazi ni kwamba kuendesha Instagram na Facebook sio kipenzi cha Mr Zuckerberg .
Yeye anataka kuanzisha ulimwengu wa Virtual , ambao anafikiri utabadilisha mazoea ya mwanadamu.
Ukosoaji wa kila mara wa jinsi anavyoendesha kampuni zake za mitandao unachosha.
Hivyobasi mpango huo mpya utampatia uwezo na muda wa kuangazia zaidi kitengo cha Virtual World ambacho kinamfurahisha.