Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Perseverance: Kwa nini wanasayansi tayari wanajua pakutafuta uhai kwenye sayari ya Mars
"Kwa hakika tuko katika mahali pazuri."Kuna unafuu miongoni mwa wanasayansi wanaokiongoza chombo cha Perseverance rover ambacho shirika la safari za anga za mbali la Marekani NASA limetuma kwenda sayari ya Mars.
Watafiti hao sasa wana uhakika kuwa wametuma chombo hicho kwenda eneo linalotoa fursa nzuri ya kugundua ikiwa kulikuwa na dalili ya maisha kwenye sayari hiyo nyekundu.
"Percy," jinsi inavyofahamika roboti hiyo, ilitua kwenye bonde Jazero mwezi Februari na tangu wakati huo imekuwa ikichukua maelfu ya picha za maeneo yaliya karibu.
Kutafsiriwa kwa picha hizo ndio msingi wa makala ya kisayansi kuhusu ugunduzi huo iliyochapiswa wiki hii kwenye nakala ya sayansi.
Utafiti umebainisha kuwa kwa sasa Perseverance ipo eneo la chini kabisa ambalo wakati mmoja lilikuwa ni ziwa kwenye ardhi ya sayari ya Mars. Tunazangumzia kuhusu kitu ambacho kilitokea zaidi ya miaka bilioni 3.5 iliyopita.
Kutoka kwa picha za Perseverence imetuwezesha kuamua kuwa mto ulikuwa umeungana na ziwa na kutiririka kwa mto huo kulipungua ghafla hivyo mchanga ukatengeneza muundo wa delta ambayo inaweza kuonekana katika sehemu nyingi kutoka duniani.
Professor Sanjeev Gupta kutoka Imperial College huko London ambaye ni mwandishi mwenzaa wa nakala hiyo ya sayansi anasema : "Baadhi ya watu wananiuliza: "Kipi kipya hapa? Kwani hatukuwa tunajua tayari kuwa kulikuwa na delta kwenye bonde la Jazero? 'Kwa kweli hatukujua,. Tulikuwa tunaona picha tu lakini hadi ufike huko hautakuwa na uhakika kamili.
Perseverance ilitua karibu kilomita mbili kutoka kwa mdomo wa mto lakini picha zilizonaswa na kamera yake zinaonekana bora zaidi wakati roboti iko eneo ambalo wanasayansi wanaliita the Kodiak.
Kando na Kodiak na mdomo mkuu wa mto Jazero pia ina mawe makubwa. Hii inaonyesha kuwepo kwa mafuriko baadaye katika historia ya bonde hilo.
"Kitu fulani kilibadlika. Hatujui iwapo ilikuwa mabadiliko ya hali ya hewa," anasema Prof Gupta. "Ili kuhamisha mawe makubwa kama hayo, unahitaji kitu kama mafuriko. Labda kulikuwa na maziwa ya theluji mahali fulani ambayo yalifanya maji kuelekea Jazero."
"Tunaona maziwa yakifurika duniani, sehemu kama Himalayas. Katika bonde la Ganges, kuna haya mawe makubwa yanayochanganya na mchanga wa mto na hapo ni wakati kuna mafuriko yanayotokea kwa ziwa la theluji," Gupa aliiambia BBC.
Kikundi cha wanasayansi wa Perseverance watachunguza mawe kando mwa Jazero ambayo yanaweza kuwa ishara za kingo ya bonde wakati ilikuwa na kina kirefu zaidi.
Roboti hiyo itakusanya na kuhifadhi sampuli kadhaa za mawe kutoka sehemu tofauti. Sampuni hizo zitaletwa duniani mapema miaka ya 2030 kufanyiwa utafiti kwenye mahabara kubaini iwapo kulikuwa na viumbe kwenye sayari ya Mars.
Mipango hii inaendelea na itahusu kutuma roboti nyingine kutoka NASA na washirika wake kutoka shirika la safari za anga za mbali la Ulaya kuleta sampuli hizo kutoka bonde ambapo Perseverance inazihifadhi.
Unaweza pia kusoma:
Ni chombo kitakachotengenezwa Uingereza. Kitakusanya mawe hayo na kuyasafirisha kwenda kwa roketi ambayo nayo itayasafirisha kwenda kwa mzingo wa sayari ya Mars ambapo setilaiti itakuwa inasubiri ili hatimaye iyasafirishe kuja duniani.
Tunakaribia sehemu muhimu sana ya kuchungua sayari ya Mars, Anasema Sue Horne, mkuu wa utafiti wa anga kwenye shirika la safari za anga za mbali la Uingereza.
"Wakati mitambo ya chombo hichoo ikifanyiwa majaribio mwezi ujao. Ndoto ya kuchunguza sampuli kutoka kwa sayari nyekundu karibuni itatimia."