Utafiti: Njia ambazo mwezi husababisha kubadilika kwa hali ya hewa duniani

Kwa miaka mingi watu wameutazama mwezi kwa dalili za mabadiliko ya hali ya hewa na kuamini kuwa mwezi wenye rangi unaashiria kuwa mvua itanyesha, mwezi mwekundu ukimaanisha mawimbi ya bahari na mwezi mweupe ukimaanisha kuwa hakutakuwa na mvua wala barafu.

Ni kweli mwezi umeonyesha uwezo wa kushawishi hali ya hewa ya dunia na mabadiliko ya hewa kwa njia kadhaa.

Kwa miaka bilioni nne unusu iliyopita, sayari mbili ziligongana zikachanganya kuwa sayari moja na ikawa dunia. Wakati wa mgongano huo wa sayari hizi mbili, dunia na sayari nyingine kwa jina Theia - jiwe dogo lililoibuka na kuwa mwezi tunaoujua sasa. Ndio maana tabia za mwezi zina uswawishi mkubwa kwa maisha hapa duniani.

Hata hivyo tabia za mwezi na athari zake kwa dunia hazieleweki ipasavyo. Changamoto sasa ni kutofautisha hadithi na ukweli kuhusu athari za mwezi kwa dunia.

Ushawishi mkubwa zaidi unaoonekana kutoka mwezini kuja hapa duniani ni mawimbi ya bahari. Dunia inapozunguka kila siku nguvu za mwezi huvuta maji hali ambayo husababisha maji hayo kupanda.

Sasa NASA wanasema kupanda kwa maji ya bahari kutoka na mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na nguvu za mwezi vitachangia kuongezeka kwa kiwango kikubwa cha mafuriko kutoka kwa mawimbi ya bahari miaka ya 2000.

Benjamin Hamlington, mwanasayansi mtafiti na mkuu wa kikosi cha wanasayansi wanaofuatilia mabadiliko ya bahari huko NASA anafuatilia jinsi maji ya bahari hubadilika kuambatana na sababu za asili na pia za kibinadamu na athari zake kwa miji iliyo pwani.

Hamlington anasema mafuriko maeneo ya pwani, yanayochangiwa na mwezi huenda yakasababisha uharibifu mbaya kwa miundo msingi na kubadilisha maeneo ya pwani.

"Tunaweza kuona mara nnne zaidi idadi ya mafuriko kutoka muongo mmoja hadi mwingine. Maji ya bahari yanapanda kila mahali kwa hivyo huenda tukaona mafuriko haya kote duniani.

"Mzunguko wa mwezi huenda ukawa na changamoto nyingi kwa wanadamu lakini kwa wanyamapori maeneo ya pwani huenda ikawa tisho kubwa kwao," Elia Rochlin professor katika chuo cha Rutgers anasema

"Wakati mzunguko wa mwezi ni mkubwa mawimbi makubwa hufurika makao ya mbu na kuwasomba kuja ardhini," anasema Rchlin.

Bila ya mawimbi hali ya hewa duniani zingekuwa tofauti kabisa. Mawimbi ndio huchangia kusonga kwa maji ambayo husababisha kuwepo maji yenye joto na baridi maeneo tofauti duniani.

Kuzunguka mwa mwezi kunatarajiwa kubadilika miongo kadhaa inayokuja lakini hata hivyo mwezi huathiri dunia kwa njia zingine nyingi.

Mwezi pia unakisiwa kuchangia viwango vya joto hasa maeneo ya Arctic.

Picha za Setilaiti zinaonyesha kuwa Arctic huwa na nyusi joto 0.55C zaidi wakati wa mwezi mzima.

Mwezi huchangia kuwepo mawimbi juu na chini ya bahari kulingana na Chris Wilson mtaalamu katika fisikia ya bahari.

Wakati maji na barafu baharini yakiwa sio tu maeneo ya dunia yanayokumbwa na mawimbi, mwezi pia una athari kwa dunia kavu na anga suala ambalo huathiri hali ya hewa.