Kwanini umaarufu wa mfululizo wa filamu ya kikorea ya "The Squid Game" utakuwa wa kihistoria Netflix

Chanzo cha picha, Netflix
Hata kama hujaiona filamu hii kwenye televisheni, kuna uwezekano mkubwa kuwa uliona matangazo yake mtandaoni.
Maelfu ya watu duniani kote wanazungumzia kuhusu mfululizo wa filamu hii, ambayo imepata umaarufu mkubwa tangu ilipozinduliwa wiki mbili zilizopita kwenye Netflix.
Kiukweli uandaaji huu wa filamu wa Korea -ambao unazingatia mchezo wa kupambana ili uishi -unapata watazamaji wengi katika majukwaa mbalimbali na kuzidi hata takwimu ya watazamaji wa filamu za kimapenzi ya Bridgerton .
Ikiwa aina ya mfululizo wa filamu hiyo haujakaa kama simulizi , unahitaji kuangalia vitendo zaidi , wahusika wanaotambulika na muonekano wa mazingira ya binadamu yamewaunganishwa watazamaji wengi duniani.
Wauaji katika chumba cha mchezo
Katika kundi la watu 456, ambao wamekata tamaa na wameingia kwenye madeni, wanashawishiwa kushiriki mchezo hatari ambao watakaoshinda ndio wana nafasi ya kupata dola milioni 39 kama watafanikiwa kushinda kupita changamoto sita .
Kama ukishindwa , unakufa
Mchezo ulikuwa mrahisi. Wengi wao ndio walikuwa wakijiburudisha kama watoto.
Na kulikuwa na mchanganyiko wa michezo ya watoto na michezo hatari inayoweza kusababisha kifo ndio imevutia watazamaji wengi.
"Watu wanavutiwa na michezo ya watoto kuchezwa na watu wazima ambao wako tayari kuhatarisha maisha yao ili kushinda,muongozaji wa filamu ya Squid Game, Hwang Dong-hyuk ameeleza katika mahojiano.
"Michezo ilikuwa rahisi ,hivyo iliwawia watazamaji kuzingatia kuwaangalia kila mhusika badala ya masharti yaliyowekwa kwenye mashindano."

Chanzo cha picha, Netflix
Kuna pia kipengele cha nostalgia. Kwa mfano, shindano la pipi za Dalgona katika sehemu ya tatu ni moja ya michezo ambao Wakorea wanakumbuka zaidi utoto wao.
Katika shindano hilo, wachezaji wanapaswa kuwa makini kukata pipi kwa kutumia sindano.
Na kama pipi ikipata ufa na kuharibu muundo wake basi utakuwa umeshindwa.
Mtumiaji wa Tweeter wa Korea aliandika katika kurasa yake: "Squid Game inanifanya nitamani kula pipi za Dalgona tena. Ni zaidi ya miaka 20 imepita ... sidhani kama zipo bado? sidhani kama ninaweza kupata."
Wahusika wanaofanana na mimi na wewe

Chanzo cha picha, Netflix
Wataalamu wameainisha kuwa sifa moja katika filamu hii ni wahusika wake.
Wengi wao ni watu wa kawaida tu katika jamii.
Ingawa wote wana changamoto kubwa ya kifedha, wametoka katika sekta mbalimbali katika jamii.
Mfano wa mhusika mkuu , kwa mfano kuna mwanaume ambaye hana ajira na ana uraibu wa kucheza kamali na anahangaika kupata heshima katika familia yake.
Katika simulizi hii , utakutana na mtu ambaye alifanya jambo baya, kipindi cha nyuma na kuwa muhamiaji Pakistani ambako alikuwa akionewa na muajiri wake.
Kim Pyeong-gang, profesa wa maudhui ya utamaduni katika chuo kikuu cha Sangmyung , ameiambia BBC: "Watu wengi haswa vijana wa kizazi hiki wamekuwa wanaangaika mara nyingi kwasababu ya kutengwa na uwepo wa chuki katika uhalisia wa maisha, kuwasilishwa zaidi na wahusika hao."
Kama ilivyo kwa mataifa mengine ya jirani ya Asia, uhalisia wa mashindano ya hyper-katika jamii ya Korea Kusini imewakatisha tamaa wegi.

Chanzo cha picha, Netflix
Licha ya kufanya kazi sana , si rahisi kwa kila mtu kuweza kupata fursa ya kusoma chuo au kupata ajira nzuri.
Michezo katika riwaya hii, ingawa kwa upande mwingine ni hatari lakini inawakilisha jinsi dunia inavyoweza kuwa na usawa.
Kama jamii mmoja alivyosema katika mchezo huo : " Washiriki wote wako sawa, na tunawapa watu ambao walihangaika kutokana na uonevu na kutopata haki.

Chanzo cha picha, Netflix
Mchezo wa taa nyekundu na taa ya kijani
Vyombo vya habari vya nje vimeshindwa kuacha kutofautisha kati ya filamu ya The Squid Game na washindi wa Oscar wa mwaka 2019 wafilamu ya Parasites, ambao waliangalia suala la jamii kutokuwa na usawa .
Lakini Mashariki mwa Asia, watazamaji wanaonesha kuwa wameona filamu hiyo kufanana zaidi na filamu ya Japan ya mwaka 2014 "As The Gods Will."
Filamu ambayo iliangazia wanafunzi wa sekondari ambao walikuwa wametoka katika maisha yanayofanana , jambo ambalo limefanya wengine kudai kuwa The Squid Game walikuwa wameiga.
Kwa mfano filamu ya Japan ilikuwa na michezo ya watoto ikionesha "Taa nyekundu na kijani " .
Katika mchezo wa "Taa nyeundu , Taa ya kijani " mtu anamtaka mtu wa nyuma kukimbia wakati taa ya kijani ikiwaka na kusimama, taa nyekundu inapowaka.
Katika sehemu moja ya filamu ya The Squid Game, kuna roboti ambaye anawawekea alama washiriki ambao walishindwa mchezo ili waweze kuuliwa.
Hata hivyo, Hwang amekanusha madai hayo na kusema hakuna uhusiano kati ya filamu hizo .













