Rasi ya Korea: Vita vya nchi mbili zilizo vitani kwa zaidi ya miongo 7

Vikosi vya usalama vya Korea Kusini

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vikosi vya usalama vya Korea Kusini

Katika hotuba ya hivi karibuni aliyoitoa kwenye Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa , rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, alitoa wito wa Korea mbili na washirika wa nchi hizo mbili jirani ( Marekani ambayo inaunga mkono Korea Kusini, na China, ambayo ni mshirika mkubwa wa kiuchumi wa Korea Kaskazini) kutangaza mwisho rasmi wa mzozo na kuleta amani katika rasi ya Korea.

Waziri wa ngazi ya juu wa Kora Kaskazini awali alipuuzilia mbali wzo hilo kama " lililotolewa kabla ya muda".

Hatahivyo, dada menye ushawisi Kim Yo Jong, wa kiongozi wa Korea Kaskazini , Kim Jong Un, alisema kuwa nchi yake iko tayari kufufua mazungumzo na Karea Kusini iwapo itasitisha kile alichokiita "sera za uadui " kwa Pyongyang.

Moon Jae- in, Rais wa Korea Kusini

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Moon Jae- in, Rais wa Korea Kusini

Alielezea wazo hilo kama "la kufurahisha sana", lakini akaongea kuwa nchi yake haitataka mazunguzo juu ya pendekezo hilo hadi Korea Kusini itakapositisha kile alichokiita "sera zauadui " dhidi yao.

Kauli za dada yake kiongozi wa Korea Kaskazini zimetolewa kujibu wito mpya kutoka wa hasimu wake Korea Kusini kutangaza rasmi mwisho wa vita vya Korea.

Yo Jong ni dada mwenye ushawishi wa kiongozi wa Kora Kaskazini na mshauri maarufu wa kaka yake Kim Jong Un

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Yo Jong ni dada mwenye ushawishi wa kiongozi wa Kora Kaskazini na mshauri maarufu wa kaka yake Kim Jong Un

Mzozo ambao uliigawanya Peninsula katika nchi mbili, ulimalizika mwaka 1953 kwa silaha, sio kwa mkataba wa amani. Kiufundi nchi hizi mbili zimekuwa vitani, tangu wakati huo, na wakati mwingine kuwa na uhusiano mgumu. Je ni ipi hadithi ya vita baina ya Korea hizi mbili?

Mizizi ya tatizo

Encyclopedia Britannica inasema kuwa Vita vya Korea ni mzozo baina Jamuhuri ya Demokrasia ya Watu wa Korea (Korea Kakazini) Na Jamuhuri ya Korea (Korea Kusini ) ambapo mamilioni ya watu walipoteza maisha yao. Vita vilifikia kuwa vita vya kimataifa mwezi Juni 1950 wakati Korea Kaskazini ilipoivamia ngome ya kijeshi ya Korea Kusini kwa usaidizi na msaada wa kijeshi wa Muungano wa Usovieti.

Asili ya Vita vya Korea ilianza tangu kuanga kwa kwa Himaya ya Kijapan katika mwisho wa Vita ya II ya dunia, Septemba 1945.

Latitudo smbamba ya 38 iliyozitenganisha Korea mbili

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Latitudo smbamba ya 38 iliyozitenganisha Korea mbili

Tofauti na China, Manchuria, na makoloni ya zamani ya magharibi yaliyotwaliwa na Japan katika miaka ya 1941-1942, Tokyo iliichukua Korea kama sehemu ya Japan tangu 1910.

Hivyobasi, Korea haukuwa na serikali ambayo ilitarajiwa kurejeshwa baada ya vita kuisha.

Wengi waliodai kurejeshwa kwa mamalaka walikuwa wamekwenda uhamishoni nchini Uchina China, Manchuria, Japan, Muungano wa usovieti, na Marekani, na hivyo walikuwa katika vitengo viwili.

Kundi la kwanza lilikuwa limeundwa na wana mapinduzi waliojitolea waliokuwa na sera za Kimarxist ambao walipigana na Wajapan kama sehemu ya wanajeshi wa kikosi kilichotawaliwa na idadi kubwa ya Wachina kilichopigana vita vya msituni katika Manchuria na China.

Mmoja ya vikundi hivi kilikuwa ni kidogo lakini kilikuwa kilifanikiwa kikiwa na kiongozi wa vita vta msituni aliyeitwa Kim Il-sung, ambaye alipata mafunzi nchini Urusi na akawa afisa katika jeshi la Usovieti .

Kitengo cha pili, hakikuwa na malengo ya mageuzi…vuguvugu hili la kitaifa la Wakorea kilikuwa na maono ya Kisayansi, elimu na viwanda katika Ulaya, na Japan

Baada ya Vita kuu ya II ya dunia, na katika dhana ya kuharakisha juhudi za kuwapokonya silaha wanajeshi wa Kijapani na Kuwarejesha makwao walowezi waliokuwa Korea (waliokadiriwa kuwa karibu watu 700,000 ).

Marekani na Muungano wa Usovieti walikubali mwezi Agosti 1945 kuigawa nchi kwa minajili ya kiutawala kwa kutumia kile kilichoitwa latitudo 38 kaskazini.

Pande mbili hazikuweza kukubaliani juu ya muundo ambao ungewezesha kubuniwa kwa Korea moja iliyoungana, na katika mwaka 1947 aliyekuwa rais wa Marekani Harry Truman aliushawishi Umoja wa Mataifa kuchukua wajibu kwa ajili ya nchi, hatakama jeshi la Marekani lilibaki na udhibiti wa Kusini.

Idadi ya polisi wa Korea Kusini iliongezeka mara dufu , na hivyo kufanya idadi ya walinda usalama wa Kusini kufikia 80,000 ilipofika mwaka 1947

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Idadi ya polisi wa Korea Kusini iliongezeka mara dufu , na hivyo kufanya idadi ya walinda usalama wa Kusini kufikia 80,000 ilipofika mwaka 1947

Idadi ya polisi wa Korea Kusini iliongezeka mara dufu , na hivyo kufanya idadi ya walinda usalama wa Kusini kufikia 80,000 ilipofika mwaka 1947.

Wakati huo huo , Kim Il-sung alijumuisha udhibiti wake wa Chama cha kikomunisti pamoja na utawla wa kaskazini kama muundo wa utawala na vikosi vya kijeshi.

Mnamo mwaka 1948, jeshi la Korea Kaskazini na polisi kwa ujumla walikuwa takriban 100,000, wakijiimarisha kwa kikundi cha wapiganaji wa msituni wa Korea Kusini waliokuwa katika eneo la Haeju magharibi mwa Korea.

Vikosi vya usalama vya Korea Kusini

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vikosi vya usalama vya Korea Kusini

Tangu mwanzoni mwa mwaka 1948, Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya jitihada za kubuni Korea kusini huru, na wakomunist wa kusini wamekuwa wakipinga hili.

Jamuhuri ya Korea (Korea Kusini) aliundwa Agosti 1948 chini ya uenyekiti wa Syngman Rhee.

Hatahivyo, takriban wanajeshi 8,000 wa Korea Kusini na walau Wakorea 30,000 walipoteza Maisha yao.

Wengi wa waathiriwa walikuwa ni watu ambao wlionekana kama "watetezi wa haki " au "Wekundu". Utekelezaji wa wa maafa ukawa ndio hali ya maisha.

Vita vya Korea viliibuka Juni 25, 1950, wakati takriban wanajeshi 75,000 wa jeshi la Korea Kaskazini lilipovuka kwenye mpaka na kuingia Korea Kusini, ambao ulikuwa unajulikana kama 38th parallel , ambao ulikuwa ni mpaka baina yake na Jamuhuri ya watu wa Korea iliyokuwa ikiungwa mkono na Usovieti.