Mexico yahalalisha utoaji mimba katika uamuzi wa kihistoria

Mahakama ya juu zaidi nchini Mexico imeamua kwamba adhabu za kosa la jinai la kutoa mimba ni kinyume cha katiba.

Uamuzi huo uliotolewa katika jimbo la kaskazini la Coahuila, unazuia wanawake kushtakiwa kwa kutoa mimba.

Utoaji mimba kwa sasa umepigwa marufuku katika majimbo yote isipokuwa manne ya nchi hiyo.

Jaji wa mahakama ya juu zaidi Luis Maria Aguilar alielezea hatua hiyo kama "hatua ya kihistoria kwa haki za wanawake".

Siku ya Jumanne, mahakama iliamuru jimbo la Coahuila kuondoa vikwazo vya kutoa mimba kutoka kwa kanuni yake ya jinai.

Uamuzi huo unaweza kufungua njia ya kuruhusu utoaji mimba katika nchi nzima.

Hivi sasa, utoaji mimba ni halali tu katika majimbo machache, isipokuwa kwa visa vya ubakaji au ambapo maisha ya mama yako hatarini.

Chanzo cha mahakama kimesema uamuzi huo utaathiri Mexico yote, ikiruhusu wanawake katika majimbo ambayo utoaji mimba ni uhalifu kufanya utaratibu huo kwa agizo la jaji.

Kundi la Habari juu ya Chaguo la Uzazi (GIRE), ambalo linafanya kampeni za haki za utoaji mimba, lilielezea uamuzi huo kama "wa kihistoria"

"Tunatumahi kuwa kote nchini wanawake na watu wenye uwezo wa kubeba ujauzito wana hali na uhuru wa kuamua hatima yao ya uzazi", lilisema.

Coahuila inapakana na jimbo la Marekani la Texas, ambapo mahakama ya juu zaidi iliruhusu sheria ya serikali kupiga marufuku utoaji mimba wowote baada ya wiki sita za ujauzito.

Uamuzi huo unaweza kufungua njia kwa watu kutoka Texas wanaotaka huduma ya utoaji mimba halali.

Uamuzi wa kuhalalisha utoaji mimba katika taifa ambalo ni la pili kwa ukubwa nchini kwa waumini wa Kikatoliki la Amerika Kusini unaweza kuonekana ya kushanga

Hata hivyo, mjadala huko Mexico umekuwa ukiendelea pole pole kuhusu kuondoa marufuku hiyo kwa muda.

Maandamano ya hali ya juu na wanaharakati wa haki za wanawake na wanawake yameelezea hitaji la haki kubwa za uzazi huko Mexico.

Hasa, mahakama ya juu zaidi iliulizwa kutoa uamuzi juu ya sheria katika jimbo la kaskazini la Coahuila inayowaadhibu wanawake wanaotoa mimba kinyume cha sheria na kuhukumiwa kwa kifungo cha hadi miaka mitatu.

Majaji 11 wa mahakama ya juu zaidi kwa pamoja walipiga kura kuhalalisha marufuku ya utoaji mimba katika jimbo hilo, na chini ya sheria ya Mexico, sasa itatumika kwa majimbo mengine yote nchini.

Inawezekana kuchukua muda kuanza kutekelezwa kote nchini, lakini kwa kweli uamuzi huo unapeana mwelekeo kwa kila jimbo kutokana na sheria hiyo mpya.

Kwa kuongezea, inapaswa kumaanisha kuwa wanawake waliofungwa kwa kutoa mimba wataachiwa huru mara moja.

Uamuzi huo unaweza kuwakasirisha wanasiasa wahafidhina zaidi huko Mexico na Kanisa Katoliki.

Hata hivyo, ushawishi wa kanisa umekuwa ukipungua katika miaka ya hivi karibuni na serikali inajichukuliwa kuwa ya kidunia.