Russell's Viper: Jinsi nyoka huyu hatari anayekaribia kuangamia alivyorudi Bangladesh

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika baadhi ya maeneo ya kaskazini magharibi ya Bangladesh, hasusan wilaya inayokaribia bonde la Padma, watu kadhaa wamejeruhiwa katika siku za hivi karibuni kutokana na kuumwa na nyoka hatari anayejulikana kama Russell's viper, huku wawili kati yao wakiripotiwa kufariki.
Russell's Viper ni nyoka hatari zadi nchini Bangladesh.
Athari za kuumwa na nyoka huyu ni pamoja na kutokwa na damu mfululizo, damu kuganda mwilini, mfumo wa neva kuathirika macho kuwa mazito, kulemaa na figo kuacha kufanya kazi.
Cha kushangaza ni kwamba spishi ya nyoka huyu ilidhaniwa kuangamia Bangladesh miaka mingi iliyopita. Lakini katika kipindi cha miaka 10 hadi 12 iliyopita kuna ushahidi nyoka hao wameibuka tena.
Utafiti unaendelea Bangladesh kubaini jinsi spishi ya nyoka huyu ilivyorejea tena katika nchi hiyo.

Chanzo cha picha, Alamy
Ahsan Mansoor, Profesa, wa Kitengo cha Wanyama, katika Chuo Kikuu cha Chittagong, amefanya utafiti juu ya kuibuka tena kwa Russell's Viper nchini Bangladesh na hatari ya nyoka huyu kwa binadamu.
Utafiti huo ambao uliochunguza watu 20 walioumwa na Russell's viper katika maeneo tofauti ya Bangladesh kuanzia 2013 hadi 2016, ulichapishwa mwaka 2016 katika jarida la Asiatic Society, Bangladesh.
Wakati huo, ulibaini kwa nyoka hao wanapatikana katika wilaya 16 kati ya 64 za Bangladesh. Kulingana na utafiti, nyoka hao wanapatikana katika wilaya za kaskazini na kaskazini magharibi.
Utafiti huo pia ulifichua kuwa maeneo yaliyo na spishi nyingi ya nyoka hao ni wilaya za Rajshahi na Chapainawabganj.
Hata hivyo, wataalamu wanahofia kuwa spishi za nyoka huo zinaweza kuwa katika mengine ya nchi.
Bwana Ahsan aliafiki kumekuwa na idadi ndogo ya nyoka wa Russell katika sehemu tofauti za Bangladesh, lakini uwepo wa nyoka hawa haukueleweka vizuri kwa sababu ya ukosefu wa mazingira ya kuzaliana na chakula cha kutosha.

Chanzo cha picha, NurPhoto
Moja ya sababu kuu za kuongezeka kwa idadi ya nyoka nchini Bangladesh katika miaka ya hivi karibuni ni kupanda mazao mengi kwa mwaka katika ardhi hiyo hiyo - Farid Ahsan alisema wakati akizungumza na BBC Bangla.
"Zamani, mazao yalipandwa mara moja au mbili kwa mwaka na wakati uliobaki ardhi ilitelekezwa kwa sababu ya ukosefu wa maji. Pamoja na kuboreshwa kwa mfumo wa umwagiliaji katika miaka ya 90, wakulima walianza kulima mazao mara mbili hadi tatu kwa mwaka na ardhi ikaachwa kidogo. "
"Idadi ya panya katika ardhi huanza kuongezeka kwani kuna mazao shambani kwa mwaka mzima, ambayo ndiyo chakula kikuu cha nyoka hawa. Na panya wanapokua, nyoka huanza kupata chakula cha kutosha na kupata mazingira mazuri ya kuzaana. "Bwana Ahsan alisema.
Kwa sababu ya vichaka vyenye majani ardhi iliyoachwa chini, nyoka hawa wanaishi kwenye ardhi ya kilimo, na kuwafanya wale wanaolima mashambani kuwa katika hatari zaidi ya kuumwa na nyoka wa Russell.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kutokana na kuongezeka kwa maji ya mto wakati wa msimu wa masika, nyoka huyu anaweza kuingia Bangladesh hata kwa kuelea juu ya mito kutoka India, alisema Bwana Ahsan.
"Kufikia sasa, nyoka hawa zaidi wamepatikana katika Bonde la Padma. Tumeona kwamba sehemu nyingi ambazo nyoka hawa wamepatikana zina magugu ya maji."
Ingawa uwepo wa nyoka wa Russell ni dhahiri zaidi katika sehemu za kaskazini na kaskazini magharibi mwa Bangladesh, nyoka huyo amepatikana hivi karibuni katika wilaya ya kusini ya Patuakhali, alisema Profesa Farid Ahsan.
Kwa kuongezea, karibu nyoka watano wa nyoka wa Russell waliopatikana katika maeneo kadhaa ya kaskazini magharibi mwa 2014 na 2015 walitolewa.
Lakini, Profesa Ahsan anafikiria kwamba nyoka wachache waliotolewa hawajachangia pakubwa kuongeza idadi ya spishi hizi nchini Bangladesh.
Kuumwa na nyoka huyu ni hatari kiasi gani
Ijapokuwa kiwango cha kuumwa na nyoka wa Russell's hakiko juu sana Bangladesh, karibu 43% ya visa vya watu kuumwa na nyoka kila mwaka hushuhudiwa India na kati ya asilimia 30-40% ya visa vyote vya kuumwa na nyoka nchini Sri Lanka hutokana na nyoka hawa wa Russell's viper.
Kwa kuwa watu kawaida huishi kwenye ardhi ya kilimo, mara nyingi humkanyaga nyoka au kumsumbua bila kujua. Russell's Viper hushambulia ghafla wakati anapohisi kutishiwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Muda mfupi baada ya kuumwa na nyoka huyu, mwathiriwa anahisi uchungu wa ajbu. Kando na hilo eneo lililoumwa huvimba kwa haraka ndani ya saa moja, na sehemu zingine za mwili zinazokaribiana na mahali palipoumwa na na nyoka huyo pia huvimba kivyake.
Mtu asipopata matibabu kwa haraka anaweza kupatikana na matatizo ya kiafya ikiwa ni pamoja na shinikizo la damu na figo kuacha kufanya kazi.
Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani mwaka 2016, karibu watu milioni 5.4 ulimwenguni huumwa na nyoka kila mwaka, na wengine milioni moja hufariki kila mwaka.














