Chanjo ya Covid-19: Chanjo ya nyongeza inafanya kazi na je kuna haja ya kuzitoa sasa?

Chanzo cha picha, Reuters
Hofu ya kuambukizwa aina mpya ya virusi vya corona vinavyofahamika kama Delta variant imefanya baadhi ya nchi kutoa chanjo ya ziada kwa watu ambao tayari wamepewa chanjo kamili dhidi ya Covid.
Lakini kutokana na ushahidi mdogo wa kisayansi wa kuunga mkono hitaji na ufanisi wa "chanjo ya nyongeza" - suala hilo limeibua hisia mseto, wakati mataifa mengi duniani yanakabiliwa na uhaba wa chanjo.
Tunapanga kupeana kinga ya ziada kwa watu ambao tayari wana kinga ya maisha, wakati tunaacha watu wengine wazame, "alisema mtaalam wa magonjwa ya Shirika la Afya Duniani(WHO) Mike Ryan, wakati akilinganisha Covid-19 na meli inayozama.
Shirika la afya Duniani linatoa maoni ya kimaadili na linatoa wito kwa serikali kusitisha chanjo za nyongeza hadi watu zaidi wapate ulinzi wa chanjo.
Lakini je ushahidi wa kisayansi unasemaje? Wanaounga mkono chanjo ya ziada na wale wanaopinga wanahoji nini?
Je wakati umewadia wa kuanza kusambaza chanjo hizo – au tusubiri?
Ni nchi zipi tayari zinatoa chanjo ya nyongeza?

Chanzo cha picha, EPA
Licha ya ombi la WHO, nchi kadhaa tayari zimeanza kutoa chanjo za nyongeza kwa baadhi ya raia wao.
Marekani inatoa chanjo za nyongeza kwa mtu yeyote bila kujali umri au hali ya kiafya, miezi minane baada ya kupata dozi ya pili ya chanjo ya Moderna au Pfizer.
Huko Dubai, dozi za nyongeza pia zinatolewa kwa wote waliopewa chanjo ya pili, na watu walio katika makundi hatarishi na wanaostahiki kupata baada ya miezi mitatu tu.
Dozi ya tatu ya chanjo inatolewa nchini Israel kwa mtu yeyote aliye na miaka 40 au zaidi na ambaowalichomwa dozi ya pili ya chanjo walu miezi mitano iliyopit.
Chile, Uruguay na Cambodia zinatoa chanjo ya nyongeza kwa watu ambao walipatiwa chanjo ya Sinovac au Sinopharm, wakianza na wazee na makundi ya watu walio hatarini.
Thailand na Indonesia zimetoa dozi ya tatu ya chanjo tofauti kwa wafanyikazi wa afya waliopewa chanjo ya Sinovac, licha ya kuwa na viwango vya chini vya watu waliopewa chanjo (8% na 12% mtawalio).
Ufaransa na Ujerumani zitaanza kutoa chanjo ya nyongeza mwezi Septemba lakini Uingereza bado haijafanya uamuzi.
Brazil, South Korea na India ni miongoni mwa nchi zinazofikiria kuanzisha programu za chanjo ya nyongeza, ingawa bado hakuna mipango iliyotangazwa katika mataifa hayo.
Chanjo na Delta variant

Chanzo cha picha, Reuters
Kinachoshinikiza programu hizo ni hofu kusambaa kwa kirusi cha Delta cha ugonjwa wa Covid-19, ambayo inaonekana kuambukiza mara mbili zaidi ya zile za hapo awali, kulingana na Kituo cha Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC).
Katika mwongozo wake, CDC inasema "watu walioambukizwa na lahaja ya Delta, pamoja na watu walio chanjo kikamilifu […] wanaweza kuipeleka kwa wengine."
Hata hivyo inasema, watu waliochanjwa wana uwezo wa kusambaza virusi hivyo kwa haraka – ndio sababu Raia wa Marekani Joe Biden anatoa wito kwa watu kuchomwa chanjo hiyo, akisema ndio “njia bora ya kujikinga dhidi ya kirusi vipya”.
Lakini Oksana Pyzik, matafiti wa chuo cha UCL kitengo cha tiba, anasema uamuzi wa kuendelea mbele na chanjo ya nyongeza ni wa mapema na “haiambatani na sayansi”.
“Nyongeza ya chanjo ni hatua ya kurupuka dhidi ya kirusi cha Delta na ni sera ya 'haki ikiwa”, aliiambia BBC.
Hakuna ushahidi wa kuunga mkono hitaji au ufanisi wa nyongeza za nyongeza, Dk Pyzik anasema.
"Hivi sasa, kuna data kidogo juu ya kinga inayodhoofika, lakini katika hatua hii ya mapema data inaashiria kupungua kwa kinga kutoka kwa maambukizo dhaifu, sio magonjwa kali," anasema.
Tatizo la kimaadili

Chanzo cha picha, Reuters
Tafiti mbili nchini Israel zinashiria kwamba dozi ya tatu ya chanjo ya Pfizer inaongeza kinga dhidi ya maambukizi na magonjwa hatari yanayowakabili watu walio na miaka 60 na zaidi.
Tafiti zingine kutoka Pfizer na Moderna zimefikia hitimisho sawa.
Lakini Dkt Pyzik anasema kuongeza ulinzi kundi moja na kuchelewesha chanjo ya kundi lingine sio mkakati wa busara.
“Kirusi hiki sugu kitaendelea kuongezeka tukichelewa kuchanja watu ulimwenguni,” anasema.
Ikiwa nchi zote zenye kipato cha juu zitaamua kuwapa chanjo ya nyongeza raia wawalio na umri wa zaidi ya miaka 50, Dkt Pyzik anasema, hii inamaanisha dozi bilioni moja za ziada zitahitajikai.
Huku hayo yakijiri, shughuli ya kutoa chanjo haijaanza nchini Burundi na Eritrea, ni 0.01% pekee ya watu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao wamepewa chanjo kamili. Huko Tanzania, ni 0.37% na Nigeria ni 0.69%.

Chanzo cha picha, EPA
Misri na Vietnam, zimechanja karibu 2% ya raia wao. Idadi ya watu wote waliochanjwa barani afrika bado iko chini ya 2.5%.
“Katika kinyang'anyiro kati ya chanjo na aina mpya ya virusi vya corona, chanjo ya nyongeza itadhibiti virusi kwa muda uwe mfupi, wa kadri au mrefu, "Dk Pyzik anasema.
Takwimu za hivi karibuni juu ya uwezo wa Delta kuambukiza na kusambazwa na watu walio chanjo zinaonyesha chanjo inayotolewa sasa pekee huenda haitoshi kudhibiti virusi.
Badala ya kutegemea chanjo peke yake , wanasayansi wanasema ili kukabiliana na kirusi kipya cha Delta lazima tuchukue tahadhari ya kujilinda dhidi ya maambukizi – ambayo inatoa ulinzi wa ziada dhidi ya virusi.












