C-17: Ndege ya kijeshi ya Marekani iliyowabeba mamia ya Waafghanistan salama

Chanzo cha picha, US Air Mobility Command
Tarehe 15 Agosti , wakati Taliban walipokuwa wakiingia katika mji mkuu Kabul, ndege ya Air Force uliwakomboa raia wa Afghanstan 823 -wakiwemo watoto 183.
Idadi hiyo ilikuwa ndio idadi kubwa kurekodiwa ya abiria waliowahi kuchukuliwa na Boeing C-17 Globemaster III -ndege yenye injini nne ya usafirishaji ambayo imekuwa ikiwasafirisha watu kutoka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hamid Karzai.
Ndege hiyo ambayo ilitengenezwa katika miaka ya 1980 na kupaa kwa mara ya kwanza katika miaka ya 1990, kwa sasa inatumiwa na nchi mbali mbali duniani kusafirisha wanajeshi, mizigo na wakati mwingine hutumika kuwaokoa watu waliomo hatarini.
Mmoja wa wanawake wa Afghanstan hata alijifungua mtoto wake wa kike angani ndani ya C-17 Jumapili. Alipata uchungu wa uzazi ndege ilipokuwa njiani kuelekea kwenye ngome ya kijeshi ya Ramstein, na daktari mmoja alimsaidia kujifungulia kwenye eneo la mizigo la ndege na ndege ilikuwa imetua.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, EPA

Kwa mujibu wa rekodi ya Air Force One kuihusu ndege hii, imeundwa kubeba mzigo wa hadi uzi to kilo 77,516 .
Vifaru vya kijeshi, malori na hata, makombora ya M1 Abrams vyote vinaweza kuingia ndani yake na kusafirishwa.
Mataifa ya Ghub yametoa ngome zao za kijeshi kwa ajili ya kutumiwa na Marekani na mataifa mengine ili kuwasafirisha raia wanaohitaji kuokolewa kutoka Afghanastan.

Chanzo cha picha, Getty Images

Marekani ililazimika kusitisha kwa muda mfupi safari zake za uokozi Ijumaa wakati vituo vyake vya kuwapokea Waafghanstan waliookolewa vilipopokea watu zaidi ya uwezo wake.
Uingereza imeahidi kuwachukua wakimbizi Waafghanstan 20,000 kwa kipindi cha muda mrefu, huku Canada ikiwa na mpango wa kuchukua idadi sawa hiyo.
Hatahivyo nchi nyingi -ikiwa ni pamoja na Marekani na Ujerumani-bado hazijasema ni wakimbizi wangapi hasa watakaowachukua kutoka Afghanistan.
Maafisa wanajaribu kuingilia kati kuwaokoa watu. Taarifa ya Pentagon ya Jumapili ilisema kuwa Marekani itatumia ndege 18 za kibiashara kusaidia kuwasafirisha watu nje ya nchi.












