Vita vya Afghanistan:Je! Uhusiano wa Urusi utakuwaje baada ya Taliban kuchukua Afghanistan?

पुतिन और और तालिबान प्रवक्ता सुहैल शाहीन

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 6

Baada ya Taliban kuteka Kabul, mji mkuu wa Afghanistan, nchi nyingi, pamoja na India, zimeanza kuhamisha wafanyikazi wao wa ubalozi kutoka huko.

Lakini kuna watatu tu ambao balozi zao bado ziko wazi huko.

Nchi hizi ni Urusi, China na Pakistan.

Kama China, Taliban iliihakikishia Urusi kwamba haitakubali eneo la Afghanistan litumike kushambulia majirani zake.

Serikali yenyewe ya Afghanistan imekuwa ikiishutumu Pakistan kwa kuunga mkono Taliban.

Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi pia iliambia chombo cha habari kinachomilikiwa na serikali Jumapili, kwamba serikali haikuwa na mpango wa kuwafukuza wafanyikazi wa ubalozi.

Hata hivyo, alikuwa pia amesema kwamba atawaita nyumbani baadhi ya wafanyikazi wake wa ubalozi.

Jumanne, balozi wa Urusi Dmitry Zirnoff amepangiwa kukutana na viongozi wa Taliban.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Katika hali kama hiyo, urafiki wa China na Pakistan na Taliban ndio sababu kubwa ya wasiwasi kwa India wakati huu.

Lakini jinsi Urusi inavyowachukulia Taliban katika siku zijazo, macho ya India hakika yameelekezwa huko.

India ina uhusiano wa kirafiki na Urusi na katika miaka saba iliyopita uhusiano wa Russia na Taliban umezidi kuimarika.

Lakini pia sio kweli kwamba uhusiano wa Taliban umekuwa wa urafiki na Urusi kila wakati.

Urusi inaaminika kuwa na jukumu katika kuchipuka na kuimarika tena kwa Taliban.

Baada ya uadui wa awali kati ya hao wawili, na kisha hadi mpango wa mazungumzo ya amani ya Afghanistan - uhusiano wao ukoje, mwanahabari wa BBC Saroj Singh alizungumza na Profesa Sanjay Pandey katika Kituo cha Utafiti wa Rushin - JNU.

Ripoti hii imeegemea mazungumzo naye.

India ndio mwenyekiti wa baraza la usalama mwezi huu

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, India ndio mwenyekiti wa baraza la usalama mwezi huu

Maslahi ya Urusi kwa Afghanistan

Simulizi ya wawili hao ilianza karne ya 19.

Wakati huo Waingereza walikuwa wanaanzisha utawala wao katika bara ndogo la India na walikuwa wakielekea Afghanistan, wakichukua Punjab chini ya udhibiti wao.

Wakati huo Punjab na Afghanistan walikuwa karibu na kila mmoja.

Wakati huo Urusi ilikuwa na nguvu kubwa, ilikuwa ikiongeza ushawishi wake kwenye mpaka wake.

Kama alivyoanzisha utawala wake katika maeneo mengi ya China.

Alikuwa amechukua sehemu nyingi kutoka Iran.

Asia ya Kati, ambayo iligawanywa katika majimbo mengi madogo, iliunganishwa nao.

Baada ya hili, mipaka ya Urusi na Afghanistan iliongezwa.

Huu ndio wakati ambapo nia ya Urusi kwa Afghanistan ilianza kuongezeka.

Alihofia kwamba ikiwa Waingereza watafika Afghanistan, usalama wake (Urusi) unaweza kuwa katika hatari.

Hicho ni kipindi ambacho Afghanistan ilikuwa nchi iliyo kati ya mahasimu wawili, Uingereza na Urusi.

Mnamo mwaka wa 1839, wanajeshi wa Uingereza walipigana vita vya kwanza vya Afghanistan.

Halafu miaka 40 baadaye, vita ya pili ya Afghanistan vilipiganwa na mnamo mwaka 1919 vita vya mwisho vya Afghanistan vikapiganwa.

Lakini pamoja na hayo, kulikuwa na ushawishi wa Uingereza kwa Afghanistan, lakini hawakuweza kuanzisha ubabe wao kwa ukamilifu hapa.

Huu ndio wakati ambao mapigano kati ya mbeberu Uingereza na mbeberu Urusi yalikuwa likiendelea huko Ulaya pamoja na Asia ya Kati, ambayo yaliitwa Mchezo Mkubwa yaani 'Great Game'

Baadaye, wakati Milki ya Uingereza ilipomalizika kuanzia Asia Kusini, Afghanistan ilikuwa imeibuka kama serikali huru.

Kuanzia wakati huo Mohammad Zahir Shah akawa mtawala wa Afghanistan.

मिखाइल गोर्बाचोफ़

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mikhail Gorbachoff

Umoja wa Kisovyeti pia uliibuka kama nguvu kubwa yaani 'superpower ' baada ya Vita vya Kidunia vya pili.

Mipaka yake ilikuwa na Afghanistan na alikuwa inajaribu kuongeza ushawishi wake huko.

Mataifa huru ambayo leo ni - Turkmenistan, Uzbekistan na Tajikistan yalikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovieti wakati huo.

Mohammad Zahir Shah pia alianzisha uhusiano mzuri na Umoja wa Kisovyeti.

Mnamo 1973-74 kulikuwa na mapinduzi nchini Afghanistan.

Mohammad Dawood Khan, jamaa wa Mohammad Zaheer Shah, alijitangaza kuwa Rais wa Afghanistan.

Ushawishi wa Umoja wa Kisovieti ulianza kuongezeka zaidi juu ya Afghanistan wakati huo.

Kufikia mwaka 1978, utawala wa Dawood Khan nchini Afghanistan pia ulimalizika na chama cha People Democratic Party of Afghanistan (PDPA) kikaingia madarakani.

Lakini utawala wake pia haukuwa thabiti sana.

Kwa hivyo, mwaka mmoja baadaye mnamo 1979, Umoja wa Kisovyeti ulituma jeshi lake huko kuwaunga mkono wakomunisti.

Baada ya hapo, kutoka mwaka 1980 hadi mwaka 1988, jeshi la Umoja wa Usovieti lilibaki Afghanistan.

Kwa njia hii enzi mpya ya vita baridi ilianza katika sehemu hii ya Asia.

Marekani ilikuwa mpinzani wa Umoja wa Usovieti.

Aliunga mkono kundi la lililopinga Usoviet nchini Afghanistan'Mujahideen'.

Katika hili, Marekani pia ilipata msaada kutoka Pakistan.

Kwa msaada wa Marekani na Pakistan, kundi la Mujahideen waliendeleza vita vyao dhidi ya Umoja wa Usovyeti.

Mnamo mwaka 1985, Mikhail Gorbachev aliingia madarakani kama Rais wa Umoja wa Usovieti.

Chini ya sera yake mpya ya kigeni, alijaribu kusuluhisha maswala yoyote ambayo yalikuwa 'magumu' kwake.

Afghanistan ilikuwa imekuwa jeraha lile lile kwa Umoja wa Kisovyeti.

Mnamo mwaka 1988, Gorbachev aliamua kuondoa jeshi lake kutoka Afghanistan.

Mnamo Februari mwaka 1989, vikosi vya Usovieti vilijiondoa kutoka Afghanistan.

Lakini kwa miaka 3-4 ijayo utawala wa kikomunisti uliendelea kuwepo nchini Afghanistan.

Mnamo mwaka 1992, serikali ya Najibullah ilianguka na Mujahideen akateka mji wa Kabul. Lakini Mujahideen waligawanywa katika makundi kadhaa. Hawakukubaliana.

Kati ya hivyo kukaibuka kikosi kipya, ambacho kilipaswa kutunzwa na Pakistan, ambayo iliitwa Taliban.

Hapa ndipo alipozaliwa.

Kuanzia mwaka 1996-2001, Afghanistan ilitawaliwa na Taliban.

तालिबान

Chanzo cha picha, SERGEI SAVOSTYANOV\TASS VIA GETTY IMAGES

Uhusiano kati ya Urusi na Taliban ulivyoanza kuzorota

Zamani, Urusi ilikuwa inaogopa sana utawala wa Taliban.

Kulikuwa na kujitenga na ugaidi katika mkoa wa Chechnya nchini Urusi.

Taliban ilitambua makundi yenye msimamo mkali huko Chechnya.

Kwasababu hii, Urusi iliichukulia kama tishio kubwa kwa eneo lake.

Sio hivyo tu, Taliban pia ilisaidia makundi yenye msimamo mkali katika nchi zingine ndogo za Asia ya Kati kama Uzbekistan na Tajikistan, ili vikosi kama hivyo vizitawale nchi jirani.

Kwa njia yoyote ile, Taliban ilikuwa tishio kwa Urusi.

Kwasababu hii, wakati shambulio la 9/11 dhidi ya Marekani linatokea, Rais wa Urusi kwanza kabisa alimwita Rais George Bush wa Marekani na akampa msaada wake.

Urusi pia iliunga mkono Marekani katika vita dhidi ya ugaidi ambavyo Marekani ilikuwa imevitangaza kwa Afghanistan.

Kulikuwa na wakati ambapo njia ya Urusi ilitumika kupeleka bidhaa kwa jeshi la Marekani.

Kampeni hii tanzu ya Urusi dhidi ya Taliban ilidumu hadi karibu mwaka 2014.

Ni lini uhusiano kati ya Urusi na Taliban ulipungua

Mnamo mwaka 2014, Urusi ilichukua eneo la Crimea.

Mwanzoni, Crimea ilikuwa sehemu ya Ukraine.

Baada ya vita hivi vya wenyewe kwa wenyewe kuanza mashariki mwa Ukraine.

Kwasababu ya hili, nchi za Marekani na Ulaya ziliiwekea vikwazo vya kiuchumi kwa Urusi.

Tayari kulikuwa na mpasuko katika uhusiano kati ya Marekani na Urusi.

Lakini mnamo 2014, alikuwa ameshuka kwa kiwango kulingana na kihistoria.

Hii ilikuwa wakati ambapo Urusi ilifungua mlango wa Taliban kwa mara ya kwanza.

Urusi imeendelea kuwasiliana na Taliban kwa miaka saba mfululizo.

Mahusiano haya hayakuwa rasmi lakini polepole mahusiano haya yamekuwa nusu rasmi.

Mnamo Januari mwaka huu, ujumbe rasmi wa Taliban pia ulikwenda Moscow.

Kwa upande mwingine, tangu 2014, Urusi-Uchina pia zimejihusisha kwa karibu sana na masuala ya kimataifa.

Hata kwa wakati huu, nchi zote mbili zinaratibu nafasi zao sasa hivi kwa Afghanistan.

तालिबान की रूस में प्रेस कांफ्रेंस के दौरान लतीफ मंसूर (बाएं), शहाबुद्दीन दिलावर (केंद्र) और सुहैल शाहीन (दाएं).

Chanzo cha picha, DIMITAR DILKOFF/AFP VIA GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Latif Mansoor (kushoto), Shahabuddin Dilawar (katikati) na Suhail Shaheen (kulia) wakati wa mkutano na wanahabari na Taliban Urusi.

Masilahi ya Urusi nchini Afghanistan

Urusi haina uwekezaji mkubwa sana nchini Afghanistan.

Katika siku zijazo, Urusi inaweza kufikiria kuongeza uingiliaji wake wa kiuchumi katika mwelekeo huu.

Hivi sasa, Urusi inaelekeza maslahi yake kwa kiasi kikubwa tu kijiografia nchini Afghanistan.

Kuna sababu mbili muhimu kwa ukaribu Urusi na Taliban sasa hivi.

Urusi inataka Wataliban wasiunge mkono wanaotaka kujitenga na pia magaidi hapa na Asia ya Kati.

Mbali na hayo, nchi kama China, Urusi pia zinataka utawala wa Marekani usiongezeke katika sehemu hii ya Asia.

Ingawa Urusi bado haijatambua rasmi Taliban huko Afghanistan.

Lakini kwa hakika imesemekana kwamba Taliban inaweza au inatoa uthabiti zaidi kwa Afghanistan kuliko serikali ya Ashraf Ghani.

Kwa upande mwingine, wanajeshi wa Taliban wanahusika katika usalama wa ubalozi wa Urusi huko Kabul.

Lakini pia ni kweli kwamba Urusi haitaki kutambua Taliban kwa haraka.

Kwa sasa, Urusi haijui ikiwa Taliban itatimiza ahadi yake kwa Urusi au la.

Urusi pia ina tahadhari kidogo juu ya taswira yake ya kimataifa.

Ikiwa Urusi imeshawikika na Taliban katika masuala haya, basi inaweza hata kutangaza utambuzi rasmi wa Taliban.

Hata hvyo, wasiwasi unaibuka kimataifa juu ya Taliban kwamba chini ya utawala wao haki za binadamu za watu wa Afghanistan hazitalindwa.

Hasa haki za wanawake.

Lakini juu ya suala la haki za binadamu, Urusi haijawahi kuwa pamoja na nchi za Marekani na Ulaya.

Urusi inaamini kuwa kuingiliwa kwa masuala ya ndani ya nchi yoyote kwa jina la haki za binadamu hakukubaliki.

Uwezekano wa India kusaidia kutokana na hali ilivyo Afganistan

मोदी और पुतिन

Chanzo cha picha, Getty Images

Urusi inaweza kucheza kama 'mpatanishi ' kati ya India-Taliban, ili mazungumzo kati ya hao wawili yamalize kwa kutamatisha hali ya kutiliwa shaka iliyopo.

Hii ni kwasababu Urusi haitaki kamwe India iungane kabisa na Marekani juu ya suala la Afghanistan.

Hapo zamani, wakati jeshi la Marekani lilikuwa linaondoka Afghanistan na juhudi za makubaliano zilikuwa zikiendelea katika viwango tofauti, wakati huo, mara kadhaa, Urusi ilikutana na Taliban, lakini India haikualikwa.

Katika mwezi wa Machi mwaka huu, Urusi iliandaa mkutano kuhusu mazungumzo ya amani nchini Afghanistan.

Marekani, Pakistan na China walialikwa katika hili, lakini India haikualikwa.

Hata hivyo, kwa kufikia mwezi Julai, pia kulikuwa na mabadiliko kidogo katika mtazamo wa Urusi.

Mahusiano mazuri kati ya Pakistan na Urusi ndio sababu moja wapo ya hili.

Lakini Urusi pia haitaki uhusiano wake na India uzorote.

Katika hali kama hiyo, katikati ya uhusiano unaozorota, haya yote bado yanawezekana.