'Fahamu kifaa kinachomfanya rais wa Marekani kuwa mtu mwenye uwezo mkubwa zaidi duniani

Muda wa kusoma: Dakika 5

Joe Biden ni Rais wa Marekani Marekani. Yeye ndiye mtu mwenye nguvu zaidi duniani. Wapinzani wake mara nyingi husema kuwa mamlaka aliyo nayo rais Biden, kama raia wa Marekani yanaweza kutumika vibaya wakati wowote ule.

Kuwa rais wa Marekani, yeye ndiye kamanda wa ngazi ya juu zaidi wa jeshi la Marekani.

Kwa uwezo alionao anapomaliza muhula wake hukabidhi kadi muhimu ya plastiki kwa rais anayeingia madarakani , na hivi ndivyo alivyofanya aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump katika siku ya kuapishwa kwa Bw Joe Biden Januari 20 .

Hii sio kadi ya kawaida

Hii ni nambari ya siri ya kufyatua makombora ya Marekani ya nyuklia. Kutokana na kumiliki kadi hii, Joe Biden anaweza kufyatua baadhi ya maelfu ya makombora ya masafa marefu ya nyuklia wakati wowote ule anaotaka.

'Uchunguzi'

Makombora haya yana nguvu sana kiasi kwamba katika kipindi cha kufumba na kufumbua macho, yanaweza kuangamiza binadamu wote duniani.

Marekani sio taifa pekee duniani , ambalo lina silaha za nyuklia. Inasemekana nchi 9 dunaini zina mabomu na makombora ya masafa marefu.

India ni mojawapo ya nchi hizo.

Lakini je mabomu ya atomiki yanafyatuliwa vipi?

Mara hii katika kipindi cha redio cha BBC, 'The Inquiry', Ruth Alexander alijaribu kutafita jibu la swali hili.

Rais wa Marekani hasemekani tu kwamba ndiye mtu mwenye nguvu zaidi. Kwa sasa yeye ndiye mwenye idadi kubwa zaidi ya silaha za nyuklia, akisemekana kuwa na maelfu kwa maelfu ya silaha hizo.

Makombora ya nyuklia

Silaha hizi za nyuklia zimetengenezwa kwa muundo wa makombora na mabomu ya masafa na zimepelekwa kuanzia kwenye manuari za kijeshi hadi kwenye vilele vya milima mbali mbali katika maeneo mbali mbali ya dunia.

Hakuna taarifa yoyote kutoka kwa rais iliyodokeza kwamba kombora linaweza kufyatuliwa kuelekea kwenye eneo lolote linalolengwa kwa kipindi cha dakika moja. Bruce Blau ni afisa wa Marekani anayehusika na ufyatuaji wa makombora.

Amewahi kufanya kazi katika vituo vya ujasusi wa makombora ya nyuklia katika miaka ya sabini.

Bruce anasema kwamba watu walikuwa wakiitwa-Minutemen(watu wa dakika). Hiyo inamaanisha, kuwa kama atapewa amri, anaweza kufyatua kombora la nyuklia katika kipindi cha dakika moja.

Silaha za nyuklia

Kazi ya Bruce na wanajeshi wenzake ilikuwa ni kufuatilia kompyuta wakati wote, ambayo wakati wowote inaweza kutoa amri ya kufyatua kombora.

Nchini Marekani, ni Rais pekee mwenye haki ya kutoa agizo la shambulio la nyuklia.

Wataalamu wanasema kama Urusi au Uchina zitaishambulia Marekani kwa makombora, basi itachukua nusu saa kwa kombora lao kuifikia Marekani kutoka katika nchi zao.

Soka ya nyuklia

Kwa upande mwingine, iwapo adui atashambulia akitokea majini, basi Marekani inaweza kushambuliwa katika kipindi cha dakika kumi na tano.

Katika hali kama hiyo, Rais wa Marekani atakuwa na muda mfupi sana wa kuamua iwapo atafanya shambulio la nyuklia. Hii ndio maana kisanduku cha ngozi kila mara husafiri na rais wakati wowote .

Kisanduku 'briefcase' huitwa mpira wa miguu wa nyuklia.

Kisanduku hiki kina mashine ambayo rais huitumia kufanya mawasiliano na watu fulani, akiwemi mkuu wa makao makuu ya kimkakati pamoja na Makamu wa rais .Ili waweze kuamua shambulio lifanyike.

Bruce Blau anaelezea kuwa 'kisanduku' hicho pia kina ukurasa ambao uko kama kitabu cha vibonzo unaoelezea nguvu na athari za makombora ya nyuklia.

Karibu na rais

Rais anaweza kuchukua uamuzi kuhusu shambulio la nyuklia kwa kutathmini athari za makombora katika kipindi cha sekunde kadhaa.

Afisa wa ufyatuzi wa makombora lazima athibitishe utambulisho wake kwa Rais wa Marekani kabla ya kufyatua kombora la atomiki. Katika kazi yake, kadi hiyo ama biskuti ile ya plastiki ni ya muhimu, ambayo kila mara huwa na rais.

Mara nyingi huitwa Biskuti

Hii ni kadi ambayo humfanya Rais wa Marekani kuwa mtu mwenye nguvu zaidi duniani, kwasababu kwa msaada kadi hii anaweza kuamuru shambulio la atomiki.

Rais lazima wakati wote awe na kadi hii mahali popote alipo.

Kadi ya mashambulizi

Bruce Blau anasema katika miaka ya themanini, Rais Jimmy Carter alitoa kadi yake au Biskuti pamoja na suti yake, kwa ajili ya kufuliwa.

Baada ya kupokea amri kutoka kwa Rais, Minutemen, makombora yalipelekwa ardhini, kwenye manuari za kijeshi na yakafunguliwa wazi akiwa na namba ya siri na wakajiandaa kushambulia.

Kitu hiki kilikuwepo kuanzia 1973. Kulikuwa na vita baina ya Waarabu na Israeli. Wakati huo huo, Bruce na Timothy walimtumia amri walizopokea ili awe tayari. Ulikuwa ujumbe wa DEFCON 3.

Shambulio kutoka Muungano wa usovieti ?

Hii ilimaanisha kujiandaa kwa uwezekano wa vita vya nyuklia. Kufyatua wakati wowote ule , watu wawili wanahitajika, ambao hutoa namba zao za siri kila mmoja.

Kwangu mimi, watu hawa wawili ni funguo za ufyatuaji wa makombora. Bruce anakumbuka siku hizo wakati alifikiri Muungano wa Usovieti ulikuwa karibu kushambuliwa.

Amri ya shambulio

Swali ni, itakuwa vipi iwapo rais wa Marekani atakuwa mwendawazimu na kuamrisha shambulio la nyuklia bila sababu yoyote?

Bruce Blah anasema katika hali kama hii, mkuu wa kamati ya pamoja ya wakuu wa majeshi anaweza kukataa kukubali amri. Lakini, uwezekano wa hili kufanyika ni mdogo sana.

Kwasababu watu wa aina hii wanaofanya kazi chini ya Rais wamepata mafunzo ya kutii amri, sio kuamrisha. Kwa hivyo, kama Rais anatoa amri la shambulio la nyuklia, basi ni muhimu sana kuizuia.

Igor ni Searchegen ni mtaalamu wa silaha za nyuklia.

Serikali ya Urusi

Igor ni mkazi wa Urusi na wakati mmoja alifanyia kazi serikali ya Urusi.

Mnamo mwaka 1999, alifungwa gerezani kwa kutoa taarifa za ujasusi kwa maadui.

Baada ya karibu miaka 11 gerezani, Urusi ilimuachilia huru ambapo baadaye alihamia na kuishi London.

Sawa na Marekani, Urusi pia ina nguvu za nyuklia. Urusi pia ina maelfu ya makombora ya nyuklia.

Wakati shambulio linapotokea...

Linapotokea tukio la shambulio dhidi ya Urusi, kengele ya tahadhari hulia katika kijisanduku 'briefcase'.

Vimulimuli hung'ara, na kumlazimisha rais kulifikia sanduku hilo haraka na kuwasiliana na Waziri Mkuu na Waziri wa ulinzi .

Waziri Mkuu wa Urusi na Waziri wa Ulinzi pia wana masanduku sawa na aliyo nayo rais. Lakini ni Rais pekee anayeweza kuamuru shambulio.

Mazoezi ya nyuklia

Hatahivyo, baadaye ilibainika kuwa ilikuwa ni roketi kutoka Norway, ambayo ilikuwa ikienda kwenye kazi ya kisayansi.

Kengele ya tahadhari ya shambulio dhidi ya Urusi ililia ikidhani kuwa roketi hiyo ilikuwa ni kombora linalokuja kuelekea Urusi.

Nchini Urusi, mara nyingi mazoezi ya vita hufanyika mara kwa mara kujiandaa kwa ajili ya ufyatuaji wa makombora.

.