Je ilikuwaje mwanamke huyu akaomba kukusanywa kwa mbegu za kiume za mume wake?

Picha ya mfano

Chanzo cha picha, EPA

Hospitali ya Vadodara- Sterling Hospital imetunza mbegu za kiume za wagonjwa wanaoumwa Covid-19 kufuatia amri ya Mahakama ya juu zaidi ya Gujarat nchini India .

Mahakama ilitoa agizo hili kutokana na ombi lililowasilishwa na mke wa mgonjwa huyu. Hatahivyo, baada ya kutunza mbegu za kiume za mgonjwa, alifariki dunia siku ya Alhamisi.

Awali, wakili wa mwanamke huyo, Nilay H Patel aliiambia BBC kwamba "hali ya afya ya mume wa mwanamke huyo inaendelea kuzorota kutokana na Covid-19 na mwanamke huyo alitaka mbegu za kiume za bwana yake zihifadhiwe. Mwanamke huyo alitoa ombi hilo akiwa hospitalini.

Hospitali ilisema idhini ya mwanaume ni muhimu kwa ajili ya kutekeleza hilo. Lakini tatizo lilikuwa ni kwamba mume wake hakuwa katika hali ya kumpatia idhini mke wake. Katika hali hii, mwanamke huyo alikuwa tayari amegonga kwenye mlango wa mahakama.

Kulingana na wakili Nilay Patel, mume na mke huyo walikuwa wameoana kwa karibu miezi minane na waliishi nchini Canada. Kutokana na afya mbaya ya baba yake mtu huyu, wote mama na mke ilibidi wakae Vadodara kutoka Canada, ambako watu hawa walipata maambukizi ya Covid. Umri wa mwanaume huyo ulikuwa ni miaka 30.

Pich ya mfano

Chanzo cha picha, EPA

Mkurugenzi wa eneo lilipo hospitali ya Sterling Hospital, Anil Nambiar aliiambia BBC kwamba wagonjwa hawa wa corona walikuwa wamefika katika hospitali hiyo takriban siku 45 ziilizopita.

Alisema , "Hivi karibuni viungo vyao vingi vya mwili vilikuwa havifanyi kazi.

''Tulikuwa tumeifahamisha familia ya mgonjwa kuhusu hili. Uwezekano wa kupona kwa mgonjwa ni mdogo sana.Baada ya hayo mke wa mgonjwa alituuliza iwepo tunaweza kuchukua mbegu za mgonjwa za kiume? Wakati swali hili lilipofika mbele yetu, timu ya madaktari iliangalia iwapo upasuaji huu unawezekana na iwapo ni sahihi kisheria''.

Anil Nambiar

Chanzo cha picha, ANIL NAMBIAR

Alielezea kuwa hilo litakuwa ni kosa kufanya hivyo bila idhini ya mgonjwa.

Baada ya kujadiliana, tulifikia uamuzi kwamba mbegu za kiume zinaweza kutolewa kutoka kwa mwili wa mgonjwa kwa kutumia upasuaji unaoitwa TESE, lakini sasa swali lilikuwa ni kwa vipi itakavyoruhusiwa, baada ya mwanamke huyu kwenda mahakamani na mahakama kuruhusu hilo kufanyika kwa muda wa dakika chache na hatujachelewesha utoaji wa mbegu za uzazi na kumaliza mchakato wa kuzihifadhi.

Sasa inategemea ni lini mwanamke huyo atataka kufanyiwa uzazi wa kusaidiwa kwa kukutanisha mayai yake ya uzazi na mbegu za mume au IVF.

Kwa njia ya teknolojia ya IVF, yai la uzazi la mwanamke na mbegu za uzazi za mwanaume huchanganywa ndani ya chupa maalum(test tube) kwenye maabara. .Kiini tete kinachoundwa baada ya mchakato huu huingizwa ndani ya mfuko wa uzazi wa mama ili kuwezesha ukuaji wa mtoto.

Picha ya mbegu za kiume

Chanzo cha picha, Getty Images