Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
China inajenga mitambo ya ufyatuaji wa makombora, wanasema wanasayansi wa Marekani
China inatengeneza kiwanja cha hifadhi ya makombora magharibi mwa nchi, wanasema wanasayansi wa Marekani.
Picha za setilaiti kutoka jimbo la Xinjiang zinaonesha kuwa kiwanja hicho kinaweza kuhifadhi mitambo 110, kitakapomalizika, inasema ripoti kutoka kwa Shirikisho la wanasayansi wa Marekani (FAS).
Maafisa wa ulinzi wa Marekani wameelezea hofu yao juu ya kuongezeka kwa nyuklia ya China.
Huu ni uwanja wa pili mpya wa kuhifadhia makombora ulioripotiwa kujengwa eneo la magharibi mwa Uchina katika kipindi cha miezi miwili.
Mwezi uliopita, gazeti la Washington liliripoti kuwa mitambo 120 ilionekana kwenye eneo la jangwa la Yumen, katika jimbo la Gansu.
FAS limesema katika ripoti yake siku ya Jumatatu kwamba eneo jipya lililopo katika la Hami, yapata kilomita 380 (maili 240) kaskazini-magharibi mwa Yumen, lilikuwa katika hatua za mwanzo za ujenzi.
Mwaka 2020 makao makuu ya ulinzi ya Marekani Pentagon yalisema kuwa China iko tayari kulimbikiza maradufu vilipuzi vya makombora.
Taarifa hii inakuja wakati Marekani na Urusi zikijiandaa kwa mazungumzo ya udhibiti wa silaha.
Mazungumzo baina ya naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Wendy Sherman na mwenzake wa Urusi Sergei Ryabkov, yanaonekana kama hatua ya kwanza ya kufufua mazungumzo yaliyokwama juu ya kupunguza silaha za nyuklia.
Lakini China hadi sasa haijashiriki katika mazungumzo yoyote ya udhibiti wa silaha.
Idara ya mkakati ya Marekani, ambayo ni sehemu ya wizara ya ulinzi yenye jukumu la kuzuia mkakati , ilipaza sauti yake juu ya taarifa za hivi karibuni kuihusu China katika ujumbe wake wa twitter.
"Hii ni mara ya pili katika kipindi cha miezi miwili umma umegundua kile ambacho tumekuwa tukisema wakati wote juu ya kuendelea kuongezeka kwa tisho linaloikabili dunia na usiri unaolizingira," ilisema.
Uwanja huo wa mitambo katika jimbo la Xinjiang uligunduliwa kwa kutumia picha za setilaiti, lakini picha zilizoonesha wazi eneo hilo zilitolewa na kampuni inayochukua picha za setilaiti ya Planet.
Mnamo mwaka 2020 China ilikuwa na hifadhi ya nyuklia yenye mitambo yenye uwezo wa kulipua makombora zaidi ya 200 na ililenga walau kuongeza uwezo huo mara mbili, ilisem Pentagon.
Marekani ina mitambo takriban 3,800 ya kulipua makombora, wachambuzi wanasema.