Je wajua ukomo wa hedhi pia huathiri ubongo?

Concept image: A woman with a cloud for a head, holding an umbrella

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwanzoni mwa taaluma yake, Daktari Gayatri Devi, ambaye ni mtaalamu wa neva katika hospitali ya Lenox Hill mjini New York, na wenzake walikosea: wakampatia tiba ya ugonjwa wa Alzheimer mwanamke aliyekuwa anakabiliwa na changamoto za kiafya zinazotokana na ukomo wa hedhi.

Baada ya msururu wa matibabu (ya mwisho ikijumuisha ya vichocheo au oestrojeni), afya ya mwanamke huyo iliimarika, na hapo ndipo Dkt Devi aligundua dalili za awali- kama vile kupoteza kumbukumbu, kuchanganyikiwa - kunaweza kusababishwa na kitu kingine.

Kupungua kwa uwezo wa utambuzi wa mgonjwa kumehusishwa moja kwa moja na kunapungua ghafla kwa viwango vya homoni ya oestrojeni, hali ambayo hujitokeza miaka ya kuelekea ukomo wa hedhi (kitaalamu ni mwaka mmoja baada ya hedhi ya mwisho).

Ufahamu huo ulimfanya Dkt Devi, kufanya utafiti kuhusu moja ya dalili za ukomo wa hedhi ambao haijulikani: tando na mifungamano kwenye ubongo unaosababisha ukungu kwenye ubongo kiingereza (brain fog).

Cha kushangaza ni kwamba wanawake wengi wanakabiliwa na hali hii lakini hawajui inasababishwa na nini.

"Wanawake wengi wanaokaribia kufika ukomo wa hedhi [kipindi kinachodumu kwa karibu miaka saba]- wanaanza kukosa uwezo wa kupata kumbumbu kama vile kukumbuka mambo yaliyofanyika hivi karibuni na kutatizika kwa lugha, au kufanya majukumu kadhaa kwa wakati mmoja," Dkt Devi aliiambia BBC.

"Huenda wakajipata wanatatizika katika ufasaha wa maneno, kitu ambacho wanawake ni wazuri sana," anasema.

ovari

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wakati ovari zinazalisha mayai machache wakati umri wa wanawake ukisogea, oestrogen kiasi kidogo huzalishwa mwilini

"Huenda wakajipata wanatatizika kwa ufasaha wa maneno, kitu ambacho wanawake ni wazuri sana," anasema.

Inaathiri aina ya kumbukumbu tunayotumia kwa mfano unapoenda dukani na kusahau ulikuwa unataka kununua nini, anasema Profesa Pauline Maki, Mhadhiri wa saikolojia katika Chuo Kikuu cha Illinois, Chicago huko Marekani.

Inaathiri uwezo wetu wa kusimulia hadithi, kushiriki kwenye mazungumzo mikutanoni. Na baadaye kukumbuka kilichojadiliwa, aliongeza.

Tatizo hili ni kubwa kuliko ilivyodhaniwa awali

"Katika tafiti zetu tuligugundua, wanawake wengi wanakabiliwa na hali hii huku asilimia 10 kati ya wale walioshiriki utafiti wakishindwa kukumbuka mambo ambayo wanatarajiwa kujua katika umri wao, anasema Prof Maki.

"Lakini changamoto hiyo sio kubwa sana kiasi cha kuwafanya washindwe kutekeleza majukumu yao kazini, japo wataona tofauti."

Kulingana na Dkt Devi, "karibu asilimia 60 ya wanawake wanaokaribia kufika ukomo wa hedhi na wale ambao tayari wamefika ukomo wa uzazi wanakabiliwa na tatizo la utambuzi, lakini hili linaweza kuthibitishwa kupitia uchunguzi wa kimatibabu.

Wakatii viwango vya vichocheo vya oestrogen vinaposhuka ghafla, baadhi ya shughuli za hippocampus zinaathiriwa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wakatii viwango vya vichocheo vya oestrogen vinaposhuka ghafla, baadhi ya shughuli za hippocampus zinaathiriwa

Mabadiliko haya huletwa na nini?

Moja ya masuala muhimu ni kwamba ubongo una vipokezi vya estrogeni na nyingi ziko kwenye eneo la hippocumpus -kiungo kidogo cha ubongo ambacho ni muhimu kwa ajili ya kutunza kumbukumbu.

"Wakatii viwango vya vichocheo vya oestrogen vinaposhuka ghafla, baadhi ya shughuli za hippocampus zinaathiriwa," Dkt Devi anaeleza.

Uchunguzi ambao washiriki waliokuwa mayai/ovari [ambazo zilikuwa na tezi nyingi za estrojeni] zilitolewa, walionesha kuwa uwezo wa utambuzi wao kuimarika mara tatu mara walipopewa virutubisho vya estrojeni, anasema Prof Maki.

Lakini sio wanawake wanaokaribia ukomo wa hedhi wanakabiliwa na ukungu wa ubongo - kwanini?

Hiii ni kwa sababu athari za kupanda au kushuka kwa vichocheo vya estrojeni zinatofautiana kutoka mwanamke mmoja hadi mwingine.

Kutokwa na jasho usiku kunahusiana na kumbukumbu?

"Lakini sio kupungua kwa vichocheo hivyo pekee kunasababisha hali hiyo. Kuna vitu vingine vya kuzingatia kama vile, kupotea kwa usingizi," anasema Rebecca Thurston, Mhadhiri wa Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Pittsburgh.

"Wakati wa mabadiliko ya kuelekea ukomo wa hedhi, hadi asilimia 60 ya wanawake wanalalamikia ukosefu wa usingizi- hali ambayo inahusishwa na kumbukumbu , anasema mtafiti huyo.

Ukosefu wa usingizi unavuruga mfumo wa kumbukumbu katika ubongo, sawa na inavyofanya hisia ya ghafla ya joto kali ambayo inaenea mwili mzima, na kusababisha uwekundo wa ngozi na joto jingi.

Everlyne alimua kutowasalimu watu kwa mikono kutokana na kwamba mikono yake ilikuwa inatoka jasho jingi

Kando na kukosa usingizi (baadhi ya wanawake wameripoti kuamka usiku na kubadilisha nguo za kulala baada kulowa jasho), hali ambayo ni tatizo la kivyake.

"Tulikuwa tukifikiria joto hilo ni daliliza ukomo wa hedhi ambayo wanawake wanaweza kuvumilia lakini utafiti umebaini kuwa inaweza kuwa tishio kwa moyo na akili, kwani inaathiri uhusiano kati ya hippocampus na mabadiliko katika kumbukumbu," Prof Thurston anasema.

Oestrogen inaathiri hisia pia?

Ndio, inaweza kuwa hivyo.

Pia upungufu wa oestrogen unaweza kuathiri ngozi, inamfanya mwanamke ahisi ngozi ni kavu na kuhisi kama wadudu wanatembea ndani ya ngozi.

Kubadilika kwa hisia kutokana na msongo wa mawazo kabla ya kufika ukomo wa hedhi pia kunaathiri kumbukumbu.

Mwiko na ukosefu wa kujua

Ikiwa hali hii inawaathiri watu wanawake wengi, kwa nini haijulikani?

Inaonekana kuna ukusefu wa ufahamu, kwanikukoma kwa hedhi bado ni suala ambalo ni mwiko katika tamaduni nyingi.

"Tatizo ni kwamba hali hii imekuwa ikiwakabili wanawake kwa miaka mingi, na huenda hawana habari ikiwa inatokana na dalili za awali kuelekea ukomo wa hedhi.

Línea

Daliliza ukomo wa hedhi ni zipi?

  • Mabadiliko katika muda wa mzunguko wa hedhi
  • Mabadiliko katika mtiririko wa hedhi (Nzito au nyepesi)
  • Ukavu wa uke
  • Kushindwa kulala
  • Moyo kwenda mbio
  • Kuumwa na viungo vya mwili
  • Mhemko wa hisia
  • Kupoteza nguvu ya misuli
  • Kupatwa na maambukizi ya njia ya mkojo mara kwa mara (UTCs)

Chanzo: Huduma ya afya ya kitaifa Uingereza

Línea
Mifupa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mifupa huwa dhaifu baada ya kukoma kwa hedhi

Tiba

Wataalamu wanasema kuwa kuna namna nyingi na taarifa nyingi za kusaidia wanawake kuishi na mabadiliko ya kimwili na kihisia yanayosababishwa na ukomo wa hedhi.

Tiba ya kuweka vichocheo mbadala ni tiba nzuri inayoweza kupatikana kuondokana na dalili za ukomo wa hedhi.

Na ukomo wa hedhi ni sababu moja wapo kuwafanya wanawake waishi maisha mazuri ya afya kwa:

  • Kula chakula bora, kuepuka mafuta na kula chakula chenye madini ya chuma ili kuimarisha mifupa na kuzuia maradhi ya moyo.
  • Kufanya mazoezi, ili kupunguza hali ya wasiwasi, msongo wa mawazo na kuepuka maradhi ya moyo.