Mzozo wa Tigray: Kufufuka kwa uasi kunamaanisha nini kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia?

Wapiganaji wa waasi wakisherehekea kuukomboa mji wa Mekelle wiki iliyopita

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wapiganaji wa waasi wakisherehekea kuukomboa mji wa Mekelle wiki iliyopita

Tukio la waasi kuuteka mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekelle ni hatua muhimu katika mzozo wa miezi nane uliokumba eneo hilo la kaskazini mwa Ethiopia, ambao ulisababisha maelfu ya watu kuuawa na mamilioni ya wengine bila chakula na misaada mingine.

Je hatua hiyo itageuza mkondo wa vita?

Serikali ya Ethiopia iliondoa wanajeshi wake baada ya miezi kadhaa ya mapigano, hatua ambayo ilishangiliwa katika barabara za mji huo.

Waziri Mkuu Abiy Ahmed awali alisema kuondoka kwa vikosi vya seriklai ni hatua ya kimkakati kwasasabu mji huo haukuwa tena "kitovu cha mgogoro huo", lakini baadaye alisema ilikuwa hatua ya kuzua maafa zaidi.

"Tumeona mabadiliko makubwa na muhimu katika vita hivyo," anasema Will Davison, mchambuzi wa ngazi ya juu waw a Ethiopia katika shirika la kimataifa la kushughuliki mizozo.

"Inaashiria huenda serikali haikuweza kuendelea kushikilia mji wa Mekelle, amailionelea ni vyema kuondoka Tigray kwa maslahi yao. Hiyo ni baada ya kutafakari kilochofikiwa vitani na vikosi vya waasi watiifu kwa Tigray People's Liberation Front (TPLF).

Ramani

Baada ya kuondoka eneo hilo, serikali ilitangaza "kusitisha mapiganokwa maslahi ya watu " wa Tigray, ikisema kusitisha uhasama kulihitajika ili kutoa nafasi ya kufanyika kwa shughuli za kilimo na misaada kuwasilishwa kwa wakazi.

Lakini tangu wakati, wapiganaji wa TPLF waliendelea na mapigano, kuteka maeneo zaidi ukiwemo mji Shire.

Waasi wa Tigray sasa wanaonekana kuwa ushawishi mkubwa katika mzozo huo wa muda mrefu. Mkondo watakaochukua ni swali ambalo wengi wanasubiri kupata jibu.

Darubini yaelekezwa kwa mzozo unaotokota Amhara

Wataalamu wanasema viongozi wa Ethiopia sasa wanaangazia kile kitakachofanyika magharibi mwa Tigray, na mzozo kati ya waasi wa Tigray na vikosi vya jimbo jirani la Amhara.

Wengi hawawana budi ila kukimbilia kambi za muda kuepuka mapigano

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wengi hawawana budi ila kukimbilia kambi za muda kuepuka mapigano

Amhara ni eneo linalokaliwa na kabila kubwa nchini Ethiopia.

Ardhi yenye rutuba inayozunguka mipaka ya jimbo hilo Tigray haizozaniwi tena na vikosi vya kimaeneo vya Amhara na wanamgambo wanajaribu kuchukua baadhi ya maeneo hayo ambayo wanasema ni yao kihalali.

"Mrengo wa Amhara wa chama cha Prosperity ni moja ya matawi mawili yaliyo na ushawishi mkubwa ndani ya chama tawala cha Abiy," anasema Iain McDermott, mcjambuzi wa shirika la kimataifa la kushughulikua masuala ya usalama.

Bw. Davison anasema kuna sababu nyingine iliyoifanya serikali kuu kuelekeza mtazamo wake katika eneo la Amhara ambayo inapakana na Sudan upande wa Tigray.

Anasema hatua hiyo ingezuia wapiganaji wa Tigray kutumia eneo hilo kuingiza misaada ya kimataifa ikiwa njia zingine zote zitakatizwa.

Map

Kile ambacho hakijajitokeza wazi ni kiwango ambacho majeshi ya Ethiopia ililemewa katika mapigano hayo ya miezi minane.

Kundi la waasi limedai hivi karibuni kuwa "kiliwajeruhi" maelfu ya wanajeshi wa Ethiopia katika makabiliano yao ya mwezi Juni.

Hawakubainisha ikiwa wanajeshi hao waliuawa au kuzuiliwa kama wafungwa wa kivita, lakini kwa kwa njia moja au nyingine, athari kwa upande wa vikosi vya ulinzi vya Ethiopia inaonekana kuwa kubwa.

Swali la majeshi ya Eritrea

Vikosi vya Eritrea vimekuwa vikishirikiana na majeshi ya Ethiopia tangu vita vilipoanza. Lakini mzozo huo umechukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa na nchi hizo mbili.

"Swali ni ikiwa Eritrea itaamua kuondoa wanajeshi wake," Bw. De Waal anasema.

Mzozo huo umeathiri uhusiano kati ya nchi hizo mbili, kulingana na mchambuzi wa masuala ya usalama Bw. McDermott. "Uhusiano kati ya Addis na Asmara umeyumbishwa," anasema.

"Sasa [Bw.] Abiy anatakiwa kuwa mwangalifu asitengane na washirika wake wa Amhara, kwani wamekuwa kiungo muhimu katika oparesheni hiyo muhimu.."

2px presentational grey line

zaidi kuhusu mzozo wa Tigray:

2px presentational grey line

Kwanini kulikuwa na mapigano Tigray?

Mwezi Novemba mwaka jana serikali ya Ethiopia ilitangaza kufanya mashambulizi kwa waasi wa waliokuwa chama tawala , the Tigray People's Liberation Front (TPLF).

Chama hicho kilikuwa na wafuasi wengi kilitofautiana na waziri mkuu Abiy Ahmed juu ya mabadiliko ya kisiasa katika taifa ambalo linategemea mfumo wa shirikisho m - ingawa pia TPLF ilivamia ngome ya jeshi Tigray.

Bwana Abiy, ambaye ni mshindi wa tuzo za Amani za Nobel alitangaza kuwa mgogoro umeisha mwishoni mwa Novemba lakini mapigano yalikuwa yanaendelea.

Maelfu ya watu waliuawa. Makumi maelfu walikimbia makazi yao na kuwa wakimbizi nchi jirani ya Sudan.

Pande zote mbili zinashutumiwa kukiuka haki za binadamu.

TPLF iliungana na kikundi kingine cha wapiganaji Tigray na kutengeneza jeshi la ulinzi Tigray.

Hofu ya njaa

Juni 10 , UN ilielezea hali ya njaa ilivyo kaskazini mwa Ethiopia.

Utafiti wa UN-ulisema watu 350,000 walikuwa katika janga kutokana na vitailiyotokea Tigray.

Kwa mujibu wa utafiti huo, chakula hakuna na ufikaji wa chakula katika eneo hilo umekuwa mgumu, hivyo hali ni mbaya watu wanakufa na njaa katika eneo kubwa.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia chakula (WFP),na la watoto Unicef lilitaka hatua za haraka kuchukuliwa ili kukabilana na janga hilo.

Lakini serikali ya Ethiopia ilikanusha madai hayo ya njaa katika taifa lake.