'Niligundua babu yangu aliwauwa watu wengi nikiandika wasifu wake'

Silvia Foti hakumjua babu yake , Jonas Noreika , ambaye raia wengi wa Lithuania ambao walipigana dhidi ya Wakomyunisti wa Usovieti wakati wa vita ya pili ya dunia.

Alikuwa kiongozi wa wanamgambo , gavana , mawanaharakati wa kisiasa na mtu aliyejulikana sana.

Ili kuhifadhi sifa yake , Foti aliamua kumaliza kuandika wasifu wa babu yake ambao ulikuwa umeanza kuandikwa na mama yake marehemu.

Lakini hakujua kile ambacho alikuwa anakaribia kugundua , kitu ambacho kitabadilisha maisha yake kabisa.

"Sikujua ukweli kuhusu zama zake zilizojaa uchafu."

Kwa miongo kadhaa, Foti alisikia kuhusu vitendo vya kishujaa vilivyotekelezwa na babu yake kuwalinda raia wa Lithuania. Akikulia Marekani , ambapo mwandishi huyu anaishi , alijivunia zama za babu yake.

Mama yake na babu yake walimwambia kwamba Jonas Noreika aliuawa kwa kupinga uvamizi wa Sovieti nchini Lithuania 1947.

Shule na barabara za Lithuania zilipatiwa jina lake , na pia kuna mabango yaliowekwa kwa heshima yake kila sehemu nchini humo.

Hatahivyo , ni mkuu wa shule moja iliopatiwa jina la babu yake ambaye mara kwa mara alimwambia kwamba babu yake alituhumiwa kwa kuwauwa Wayahudi.

''Karibu nizirai aliposema hilo, kwasababu ilikuwa mara ya kwanza nilisikia hivyo'', anakumbuka Foti, ambaye alikuwa na umri wa miaka 38 wakati huo.

"Mama yangu alikuwa amefariki na Babu yangu pia alikuwa amefariki '' , aliambia kipindi cha BBC cha HardTalk.

"Nilidhani nitaandika kitabu chenye historia nzuri kuhusu babu yangu. Sikujua chochote kuhusu zama zake chafu'' , anaendelea.

"Nilidhani nilikuwa naandika historia ya shujaa wa vita ya pili ya dunia ambaye alipigana na Wakomyunisti''

Akishangazwa na kile alichosikia shuleni , na kufikiria kwamba ''ilikuwa propanganda ya Wakomyunisti, nilikataa kwa muongo mmoja''..

Mauji ya Wayahudi wengi

Mwandishi alikaa miaka 10 akitathmini habari yote kuhusu babu yake. Wakati huo , alipata nakala ya kurasa 30 ilioandikwa na Noreika mwaka 1933, wakati alipokuwa na umri wa miaka 22.

Foti anaelezea kwamba nakala hizo zilishirikisha mawazo dhidi ya Wayahudi ikiwemo kwanini raia wa Lithuania wanapaswa kuwasusia Wayahudi.

Nakala nyengine alizopata pia zilithibitisha kwamba babu yake alikuwa akimpenda Adolf Hitler na Benito Mussolini.

Jinsi nilivyogundua zama chafu za babu yangu

Lakini kile kilichojiri baadaye kilinishtua zaidi: Alipata ushahidi mwingi kwamba Noreika alihusika katika mauaji ya Wayahudi wengi , ijapokuwa hakuna ushahidi kwamba yeye mwenyewe alitekeleza mauaji hayo ya watu.

Kutokana na ushahidi wake , aliamua kubadilisha kichwa cha kitabu hicho kusoma

''Mjukuu wa Nazi''.

Zaidi ya asilimia 95 ya Wayahudi wa Lithuania waliuawa wakati wa utawala wa Nazi nchini humo.

Hii leo , pamoja na wanachama wa jamii ya Wayahudi na wajukuu wao ughaibuni , Foti anafanya kampeni ya kuliondoa jina la babu yake kutoka kwa orodha ya mashujaa wa Lithuania.

Lakini wale wanaomtetea Noreika wanasema kwamba , mtu huyo alikuwa akitetea taifa wakati ambapo raia wa Lithuania walikuwa katika tishio kutoka kwa Wanazi na Warusi.

Unazi katika familia yangu

Wanaomuenzi mtu huyu wanahoji kwamba Wanazi hawakumchukulia kama mwenzao, kwasababu alikamatwa na kupelekwa katika kambi moja na baadaye kuuliwa na Warusi.

Lakini Foti anasema kwamba aligundua nakala nyengine zinazoonesha Noreika alikuwa mwanachama wa vuguvu dhidi ya Usovieti na alishirikiana na Wanazi 1941 , wakati alipokuwa na umri wa miaka 30.

Babu yake aliongoza operesheni ya kuwafukuza Wayahudi kutoka katika makazi yao, ambao baadaye walipelekwa katika mitaa ya mabanda.

Na alipata ushahidi wa kutosha kwamba Noreika alisimamia mauaji ya kimbari ya Wayahudi 2000.

Ushahidi mkubwa wa kuthibitisha hayo yote upo katika kumbukizi ilioandikwa na katibu wa Noreik anayedai kwamba muajiri wake alimuagiza kuwaua Wayahudi.

''Hivyobasi alikuwa shahidi'', anasema Foti.

Huku akiendelea kufichua ushahidi zaidi kuhusu maasi ya babu yake , baadhi ya Wayahudi wa Lithuania walikuwa wakifanya kampeni dhidi ya Noreika , ikiwemo Grant Gochin, anayedai takriban watu 100 wa familia pia waliuawa na mtu huyo.

Niliweka wazi utafiti wangu. Na siku moja Silvia alinitumia ujumbe , akimkumbuka Gochin - raia wa Afrika Kusini na Mmarekani Myahudi - kizazi cha Lithuania ambaye ameshindwa kuwasilishwa kesi mahakamani dhidi ya serikali ya Lithuania.

''Nilikuwa nikimshuku sana ….aliniita na kusema, Nimesoma utafiti wako wote , lakini umefanya makosa makubwa''.

Aliniambia: Hujasajili waathiriwa 10,000 wa babu yako

Gochina anadai kwamba Noreika , anahusika na mauaji ya watu 15,000, kati ya Wayahudi 220,000 waliofariki nchini Lithuani ,kitu ambacho mamlaka ya Lithuaani inapinga.

Alipogundua kuhusu maisha ya zamani ya babu yake , foti amekiri kwamba hangeandika kitabu hicho iwapo mama yake au bibi yake angekuwa hai.

"Kisaikolojia nilikuwa nikipigana dhidi ya mapepo yake nilipokuwa nikiandaika kitabu hiki , yote yalikuwa juu yangu katika fikra zangu na mara nyengine nilikuwa nikilia ili kupigana nayo," anaelezea BBC..

Hatahivyo anaamini kwamba kile alichofanyia wasifu wa babu yake , kitaponya familia za waathiriwa na pia kuwaponya raia wa Lithuania.