China yakana madai kwamba ni changmoto kubwa kwa jeshi la Nato

Members of the Communist Party of China (CPC) review the oath of joining the party in front of the party flag on April 13, 2021 in Luoyang, Henan Province of China

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nato amelionya jeshi la China katika kuimarika kwake, lakini haitaki vita nyingine ya baridi na China

China imeishutumu Nato kwa kusema mambo ya uongo kuhusu maendeleo ya amani baada ya viongozi wa muungano kuonya juu ya changamoto za kimfumo ambazo zinazotokea Beijing..

Hatua zilizochukuliwa na China, ikiwemo kuongeza nguvu zake za kinyuklia kunatishia muungano wa kimataifa , Nato ilisema.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Nato kuiweka China kuwa kitovu cha agenda.

Katika majibu yake, China ilitaja sera yake ya ulinzi kiuhalisi na kuitaka Nato kutotumia nguvu nyingi katika kuhamasisha mijadala.

"Uimara wa ulinzi na jeshi letu kuwa la kisasa ni suala ambalo linaweza kuthibitshwa kwa kuangalia uhalisia , uwazi, uwajibikaji na sababu zinazopelekea kuwa hivyo," China iliandika mpango huo katika taarifa yake kwa Umoja wa Ulaya.

Iliongeza kusema kuwa Nato inapaswa kuangalia maendeleo ya China katika mpangilio mzuri na kuacha kuchukua maslahi na haki halali ya China kwa minajili ya kisiasa katika mataifa mbalimbali, kuweka malumbano na kuchochea ushindani.

Taarifa ya Nato imekuja wakati wa mkutano wa siku moja huko Brussels uliofanyika Jumatatu.

Huu ni mkutano wa kwanza kwa Joe Biden kuhudhuria akiwa rais wa Marekani.

Umoja wenye nguvu wa kisiasa na jeshi kati ya mataifa 30 ya Ulaya na katika mataifa ya Kaskazini ya Marekani ambayo yanaona Urusi kuwa tishio.

Bwana Biden anatarajia kukutana na rais wa Urusi Vladimir Putin huko Geneva kesho Jumatano.

Kwanini Nato inaifuatilia China?

Kwa mujibu wa Mkutano na taarifa ya maandishi, Nato ilisema nia yake na tabia yake ya uthubutu imewasilisha changamoto za kimfumo katika sheria za kimataifa zilizowekwa na katika maeneo ambayo yanahusiana na usalama wa pamoja".

"Tuna wasiwasi na China kwa kushindwa kuwa wawazi mara nyingi na kutumia taarifa za kupotosha," kilisema.

Nato Secretary General Jens Stoltenberg holds a news conference ahead of the summit

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Katibu mkuu wa Nato Jens Stoltenberg anasema muungano huo hautaki vita baridi na China

Katibu mkuu wa Nato Jens Stoltenberg amewaambia waandishi kuwa: "Hatutaki kuingia kwenye vita mpya ya baridi na China kwani China sio wapinzani wetu wala adui zetu"

Lakini aliongeza kusema kuwa: "Tunapaswa kuliwasilisha hili kwa pamoja, kama muungano, kuwa changamoto ya kukua kwa China kuwa tishio la usalama".

China ni miongoni mwa nchi zinazoongoza duniani katika uimara wa jeshi na kukua kwa uchumi, ambapo chama tawala inahusisha sana kisiasa, maisha ya kila siku na katika jamii kwa ujumla.

Jeshi la China kwa sasa linaongoza kwa kuwa na jeshi kubwa zaidi duniani, lina wanajeshi zaidi ya milioni mbili kazini.

Nato imeanza kuwa na wasiwasi wa kuongezeka kwa uwezo wa jeshi hilo la China, ambalo linaonekana kuwa tishio katika usalama na miiko ya demokrasia katika wanachama wake.

Katika miaka ya hivi karibuni, Muungano huu umeongeza hofu ya shughuli ambazo China inazifanya barani Afrika, ambako wameweka kambi zao.

line

Nato ni nini?

  • Muungano wa kijeshi wa nchi za kimagharibi unaojulikana kama Nato, ni muungano wenye nguvu zaidi katika ukanda huo na duniani.
  • Ulianzishwa mwaka 1949, baada ya Vita ya Pili ya Dunia, kukabiliana na tishio la kuongezeka kwa ubepari.
  • Muungano huo ulianzishwa kwa kanuni za kujumuisha ulinzi wa pamoja kwa washirika
  • Ulianza na wanachama 12, lakini sasa una wanachama 30 - kutoka mataifa ya Ulaya na Marekani na Canada
  • Mpango wa Nato kwa sasa unajumuisha kutoa mafunzo, kulisaidia jeshi la Afghan, kuimarisha usalama Kosovo na kusaidia kukabiliana na ugaidi nchini Iraq
  • Pamoja na operesheni za kijeshi , Nato imekuwa ikisaidia pia katika majanga
line

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson alisema: "Ikija kwenye suala la China, sidhani kama kuna mtu katika meza hii anataka vita mpya ya baridi na China."

Ujumbe mkali wa Nato kwa China ulikuja baada ya taifa hilo kuwakosoa G7, katika mkutano wa mataifa tajiri uliofanyika wiki iliyopita.

UK Prime Minister Boris Johnson arrives to attend a Nato summit

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson

Katika mkutano wa viongozi wa G7 ambao ulikosoa China kwa madai ya kukiuka haki za binadamu, kutokuwa wasiwasi na kutaka chanzo cha Covid 19 kifanyiwe uchunguzi nchini humo. .

China ilijibu madai hayo kwa kuishutumu G7 kwa uongo, na shutuma zisizo na maana .