Mapinduzi Mali: Jinsi ya kutatua kitendawili cha mapinduzi ya Mali

Kanali Assimi Goita (Katikati), Rais wa CNSP (National Committee for the Salvation of People)

Chanzo cha picha, AFP

Kwa mara ya pili katika miezi tisa, Kanali Assimi Goïta amechukua madaraka nchini Mali, akiwashikilia Rais wa mpito Bah Ndaw na Waziri Mkuu Moctar Ouane baada ya kuwatuhumu kwa kutotimiza majukumu yao na kujaribu kuhujumu mabadiliko ya kidemokrasia ya serikali ya nchi hiyo.

Aliongoza pia mapinduzi yaliyomuondoa mamlakani mkuu wa nchi aliyechaguliwa, Ibrahim Boubacar Keïta, mnamo Agosti 18 mwaka jana.

Lakini mapinduzi ya 2020 yaliungwa mkono sana na Umma na wanasiasa wa upinzani ambao walikuwa wamekasirishwa na uongozi 'dhaifu' wa Bwana Keïta, na kuufumbia macho ufisadi.

Ilichukua majadiliano ya wiki kadhaa kabla ya masharti ya kurudi kwa utawala wa kidemokrasia hatimaye kukubaliwa kati ya viongozi wa mapinduzi na wapatanishi kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Magharibi mwa Afrika (Ecowas), umoja wa kikanda ambao Mali ni mwanachama.

Kanali Goïta aliwekwa kama makamu wa rais wa mpito - ushawishi wa jeshi bado una nguvu. Tarehe ya mwisho ya miezi 18 ilikubaliwa kwa uchaguzi wa rais na wabunge kufanyika.

Picha kutoka juu ikionesha bandari ya Mopti nchini Mali

Chanzo cha picha, AFP

Lakini kutatua kitendawili kilichotokana na uingiliaji huu wa hivi karibuni wa kijeshi - ambao ulianza wakati wanajeshi walipowakamata Bw Ndaw na Bw Ouane Jumatatu - inaweza kuwa ngumu zaidi kwa Ecowas, ambaye mpatanishi mkuu, Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan, ambaye yuko Mali kusuluhisha mzozo huo.

Muda ni mdogo sana. Uchaguzi umepangwa katika kipindi cha miezi tisa na mabadiliko ya katiba yanayohitajika bado hayajakubaliwa, kutungwa sheria na bunge la mpito lililoteuliwa au kupitishwa na Umma katika kura ya maoni.

Na hali ya barabarani ni tofauti. Mwaka jana umma ulikatishwa tamaa na Bwana Keita na walikuwa na njaa ya mabadiliko. Lakini hakuna uhasama maarufu kama huo kwa Bwana Ouane, ambaye anachukua jukumu tu la muda. Asasi za kiraia zililaani mapinduzi ya hivi karibuni.

Tishio la vikwazo

Kwa kuongezea, imani ya kikanda na kimataifa kwa Kanali Goïta imevunjwa na maukio ya wiki hii - ambayo yamekemewa vikali ,huku Umoja wa Ulaya (EU) ukitishia kuweka vikwazo.

Mkataba ulijadiliwa mwaka jana kati ya wanajeshi na Ecowas ulitokana na uelewa kwamba, ingawa ushawishi wa jeshi utakubaliwa kupitia uteuzi wa wanajeshi kwa nyadhifa kadhaa kuu, mabadiliko hayo yangeongozwa na raia, kama Ndaw waziri na afisa mstaafu.

Mali ilianza kusonga mbele. Kulikuwa bado na shida kubwa - si jambo la kushangaza katika nchi inayojitahidi kudhibiti mashambulizi ya jihadi kaskazini mwa nchi na mikataba ya wafanyabiashara wa ndani kumaliza vurugu kati ya jamii ya wakulima na jamii za ufugaji katika mikoa yake ya kati.

Watoto wakivuna pamba wakati wa msimu wa mavuno kusini mwa Mali mwezi Novemba mwaka 2018

Chanzo cha picha, AFP

Kulikuwa na malalamiko juu ya utendaji wa serikali ya mpito, wakati vyama vya siasa vya upinzani vilipoona vimetengwa.

Hatahivyo, Bw Ouane aliandaa mpango kabambe wa mageuzi yaliyopangwa iliyoundwa kutayarisha urejesho wa mfumo wa kawaida wa demokrasia.

Alianza kushughulikia matatizo - kama vile ugatuzi - ambayo mara nyingi yalipuuzwa na Bwana Keïta.

Hatua wakati mwingine zilipungukiwa na maneno. Lakini kulikuwa na mwelekeo; ikiwa kuna chochote, kwa maoni ya wakosoaji wengine, mipango ya Waziri Mkuu kwa kile kinachoweza kufikiwa wakati wa mpito yalikuwa mategemeo makubwa sana.

Lakini, sasa, haya yote yametiliwa shaka. Imani kwa kujitolea kwa Kanali Goïta kuelekea uchaguzi huru imeharibiwa vibaya - tayari umetetemeshwa na uvumi kwamba anaweza kuwa na matamanio yake katika uchaguzi.

Kwa mara ya pili chini ya mwaka mmoja, viongozi wa serikali ya Mali waliwekwa kizuizini katika kambi huko Kati, mji wa ngome upande mwingine wa vilima kutoka Bamako.

Vikosi vya kigeni vimekuwa vikisaidia majeshi ya Mali kupambana na wanamgambo

Chanzo cha picha, AFP

Mwezi Machi 2012, wanajeshi wasioridhika walichukua madaraka baada ya wimbi la ghadhabu juu ya hisia kwamba wanajeshi wa kawaida walikuwa wameachwa peke yao kuteseka, na kufa, mbele ya mashambulizi ya jihadi katika jangwa la Sahara, wakati uongozi ulikaa salama huko mjini Kati na Bamako.

Hali ilitulizwa kupitia mazungumzo yaliyofanya kuanzishwa kwa utawala wa mpito wa raia.

Mwaka jana, shinikizo la mzozo wa muda mrefu na jihadi lilichukua hatamu, maandamano ya watu wengi katika barabara za mji mkuu, Bamako.

Map

Wakati huu, malalamiko ya jeshi ni kuondolewa kwa watu wawili waliokuwa kwenye mapinduzi kutoka kwenye nafasi za uwaziri na nafasi zao kuchukuliwa na maafisa wengine wa juu.

Jeshi, au angalau wale walio karibu na Kanali Goïta, wanaonekana kuzidi kuwa na msimamo katika haki yao ya kuweka masharti ya mpito ili kulinda maslahi yao, kisiasa na kiuchumi.

'Mapambano dhidi ya wanajihadi hatarini kudhoofishwa'

Kwa hivyo, kwa mara ya pili chini ya mwaka mmoja, Bw Jonathan anajikuta katika mji mkuu wa Mali, akijaribu kuwashawishi wanaume walio na uchovu wa jeshi kwamba nguvu lazima zirejeshwe kwa raia - na kujaribu kuwafanya waelewe ni kwanini serikali za Afrika Magharibi, na jamii ya kimataifa, hawatakuwa tayari kutambua serikali ya mapinduzi.

Na ikiwa hoja hii haiwezi kukubalika , ni nini basi kitakachofuata?

Vikwazo vya kiuchumi kwa Mali vinaweza kusababisha maumivu makubwa kwa watu na usumbufu na kuyumbisha uchumi ambao tayari umeumizwa na changamoto za usalama zilizodumu kwa muda mrefu na janga la corona

Je! Vikwazo vinavyolenga viongozi wachache wa mapinduzi kweli vina athari kubwa?

Kwa kuongezea, ikiwa Mali inatawaliwa na serikali ambayo haitambuliwi kimataifa kuwa halali, hiyo inaweza kudhoofisha ushirikiano kati ya jeshi la Mali na jeshi la Ufaransa na majeshi mengine ya Ulaya ambayo sasa yamepelekwa nchini humo katika operesheni dhidi ya wapiganaji wa jihadi.

line

Bwana Jonathan anajua kuwa Ecowas inaungwa mkono kabisa na Umoja wa Afrika, EU, Marekani, na UN, lakini ana kazi ngumu ya kufanya katika juhudi zake za kutatua mgogoro huo.

Itahitaji diplomasia yenye ustadi kupata njia ya kutegua kitendawili cha wiki hii, kuokoa mabadiliko ya kisiasa na njia ya kurudi kwa utawala wa kidemokrasia wa katiba.