Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Barua kutoka Afrika: Wanawake wengi hawaukubali muonekano wa mvi kichwani
Katika msururu wa barua zetu kutoka kwa waandishi wa habari wa Kiafrika, Mwandishi Mghana Elizabeth Ohene alitumia fursa ya janga la virusi vya corona kuunga mkono mwenendo wa urembo wa kisasa
Hivi karibuni nilichukua uamuzi mkubwa kuhusu muonekano wangu.
Hapana, sijafanya upasuaji wa kutumia kisu wa kunyoosha makunyanzi , wala sikujaribu kukuza makalio.
Badala yake, ninatembea na nywele zangu za mvi -zenye rangi nyeupe- zikionekana.
Katika umri wa miaka 76, sio jambo jipya kwamba ninapaswa kuwa na nywele nyeupe, lakini amini usiamini, umekuwa ni uamuzi mgumu.
Kulikuwa na wakati ambapo ungeweza kujua ni hatua gani katika maisha ambayo mwanamke wa Ghana amefikia kwa jinsi anavyochana nywele zake.
Hadi takriban miaka 16 au 17, msichana alikuwa na nywele fupi. Kuanzia pale kupanda juu, angeweza kuzisuka au kuongezea nywele za bandia au kufanya vitu vyovyote vya kuvutia ambavyo angetaka kwa ajili ya nywele zake.
Mwisho wa mvi
Wavulana na wanaume walitunza nywele fupi, mtindo wa nywele wa "Afro" bila shaka ulikua wa kipekee.
Inapokuja katika suala la rangi, nywele ya kila mmoja ilikuwa nyeusi kuanzia anapozaliwa, hadi anapokuwa mtu mzima, wakati kila mtu anapokuwa na mvi.
Lakini katika wakati fulani hilo lilibadilika.
Sina uhakika wakati rangi nyeusi ya nywele(kanta) ilipoanzishwa katika jamii ya Waghana- wakati fulani katika miaka ya 1950, Nilisikia ikisema-lakini ikaja. Ilipewa jina "yoomo b3 Ga", au kwa kifupi "yoomo", ambalo ni jina la mwanamke mkongwe katika lugha ya Ga nchini Ghana
Jina kamili la rangi nyeusi ina tafsiri ya "hakuna mwanamke mzee katika Accra".
Maneno hayo yanaashiria asili ya ushawishi wa asili kuingia kwa rangi nyeusi ya nywele ndani ya mitindo na utamaduni wa Ghana.
Muonekano wa kipekee unaoonekana zaidi wa mtu mkongwe, bila shaka, zimekua ni mvi au nywele nyeupe, lakini sasa, kutokana na rangi nyeusi inayopakwa kwenye nywele, hapakuwa na mwanamke mkongwe katika mji mkuu wa Ghana, Accra.
Rangi ya nywele ya wanawake wa Ghana ikabakia kuwa nyeusi, kuanzia wanazaliwa hadi wanapozikwa.
'Suluhu rahisi ' kwa muonekano wa uzee
Inapaswa kusemwa kwamba shauku ya kutokuwa na nywele za mvi haikuwa kwa wanawake wenye umri mkubwa tu . Taratibu, wanaume walianza kuwa nayo pia na hatimaye usingeweza kumpata yeyote mwenye mvi, popote, mwanaume au mwanamke, hata awe na umri gani.
Mabadiliko ya jinsi wanaume wa Ghana walivyokuwa wakichana nywele zao ulikuwa hata wa kufurahisha zaidi. Sio wote ambao walipaka rangi nyeusi, walikuwa na suluhu rahisi kuepuka muonekano wa uzee.
Hawakutaka kuruhusu nywele yao hata moja ibakie vichwani mwao-vipara vikawa ndio mtindo
Walinyoa nywele zao na kutatua tatizo la kupotea kwa nywele. Vichwa vilivyonyolewa pia vilitatua tatizo la kupoteza nywele
Usingeweza kubashiri ni wanaume wangapi, hasa wanaume vijana, waliochukia kuwa na vipara.
Siku hizi huwaoni wanaume wengi wenye vipara wakiwa na sehemu ya nywele iliyobaki. Kila mtu amenyolewa safi, vijana na wazee.
Safari yangu binafsi ya nywele haijawa ya kusisimua kusema kweli.
Nywele zangu nyeusi, sawa na kila msichana wakati ule, zilikuwa fupi hadi nilipofikia umri wa miaka 16.
Nilikuwa na nywele nyingi, ndefu na nyeusi hadi nilipotimiza umri wa miaka 50 wakati mvi zilipotawala kichwa change na nikashawishiwa kupaka rangi nyeusi na imesalia kuwa hivyo.
Nilipojihoji mwenyewe kuhusu ni kwanini upakaji wa rangi , nilijiliwaza mwenyewe kwamba sikutaka kuwakanganya maafisa uhamiaji kwa kujiwasilisha mbele yao na nywele za mvi wakati inaonesha kwenye paspoti kwamba nina nywele nyeusi.
Katika mwaka huu uliopita wa Covid, nilipoenda katika saluni kwasababu ya tatizo, niliacha kupaka nyele zangu rangi nyeusi na kuamuia kuvaa kilemba kichwani.
Wiki mbili zilizopita, nilitoka nje na nywele zangu mpya nyeupe.
Sina uhakika kama nimeanza mwelekeo mpya, lakini haimaanishi kuwa sasa utapata mwanamke mmoja mkongwe mwenye - yoomo - mjini Accra