Waridi wa BBC: Safari ya Rahab Mwangi ya kutoka kuwa mraibu hadi mchungaji kanisani Uingereza

Rahab sasa ni mchungaji nchini Uingereza

Chanzo cha picha, RAHAB

Maelezo ya picha, Rahab licha ya kuingia katika uraibu wa mihadarati sasa ni mchungaji nchini Uingereza
    • Author, Anne Ngugi
    • Nafasi, BBC Swahili

Mchungaji Rahab Mwangi anakumbuka vyema jaribio lake la kwanza la kuvuta sigara .

Wakati huo alikuwa amehamishwa kutoka nchini Kenya alikozaliwa na kuanza maisha mapya nchini Uingereza , ambapo wazazi wake waliamua kuanza maisha mapya nchini humo .

Asijue kuwa jaribio hilo la kwanza lilikuwa mwanzo wa pandashuka za uraibu wa sigara, pombe na dawa nyingine za kulevya.

"Nilipoanza shule ya msingi nchini Uingereza nilianza urafiki na rafiki mmoja aliyenifundisha kuvuta sigara , siku ya kwanza nilikohoa mno, ya pili vile vile , ila mwisho wa juma hilo nakumbuka nikiwa mraibu,"alisema Rahab.

Mwanzo wa uraibu

Mwanamke huyu anasema kuwa alikuwa akivuta sigara shuleni wakati walipokuwa nje ya darasa.

Mwanamke huyu anasema kuwa alikuwa akivuta sigara shuleni wakati walipokuwa nje ya darasa.

Chanzo cha picha, Rahab

Maelezo ya picha, Mwanamke huyu anasema kuwa alikuwa akivuta sigara shuleni wakati walipokuwa nje ya darasa.

Rahab anakumbuka kuwa uraibu huo ulimpatia starehe tofauti lakini hakujua kwamba ungemsababishia madhara ya aina yake.

Hatahivyo siri yake ya uraibu huo haikuchukua muda kwani iligunduliwa akiwa na umri wa miaka 13 alipoanza kuwa na matatizo ya pumu , pamoja na uchungu uliotokea kwenye sikio lake moja .

Mama yake alimpeleka hospitali kwa uchunguzi zaidi . Akiwa hospitalini madaktari waligundua kuwa alikuwa na moshi katika mapafu yake .

"Uchunguzi ulionyesha uwepo wa moshi wa sigara kwenye mapafu yangu, wakati ambapo nilikuwa nikivuta sigara 20 kwa siku.Vilevile kutokana na uvutaji wa bangi madaktari waligundua kwamba nilikuwa na ugonjwa wa kifua kikuu (TB)" anakumbuka Rahab

Ni wakati huo ambapo wazazi wake waligundua kuwa mwanawao alikuwa kwenye uraibu.

Kumbuka kwamba katika kipindi chote hicho aliwaonyesha wazazi wake kwamba alikuwa ameacha tabia hii .Ila mwanamke huyu anakiri kuwa alikuwa mateka.

Akiwa hospitalini madaktari waligundua kuwa alikuwa na moshi katika mapafu yake .

Chanzo cha picha, RAHAB

Maelezo ya picha, Akiwa hospitalini madaktari waligundua kuwa alikuwa na moshi katika mapafu yake .

Wakati mwingi amekiri kutoroka shule ili kuendelea na urabi wake .

Mwisho wa masomo yake ya upili matokeo yake hayakuwa ya kuridhisha na anaamini kuwa iwapo angesikia la mkuu asingevunjika guu.

Chanzo cha uraibu

Mwanadada huyu anasema kuwa safari ya mtu mwenye uraibu hutokana na sababu mbalimbali .

Bi Rahab anasema utotoni mwake hakuwwahi kuamini kuwa alikuwa mrembo , aidha anasema kuwa ilikuwa vigumu kwa mtu yeyote kumuelezea kuwa alikuwa na umbo zuri , hivyobasi aliishi akijichukia na kuwa na mawazo kwamba maumbile yake yalikuwa duni.

Ilimlazimu kujiingiza katika uraibu wa dawa baada ya kuhisi kwamba dawa hizo zilibadili fikra zake na kumpatia ujasiri.

Wakati huo wazazi wake walikuwa viongozi wa dini , na kwamba yeye mwenyewe alikuwa na uelewa wa dini.

"Licha ya kuwa nilikuwa na uraibu bado nilijihusisha na maombi pamoja na shughuli mbali mbali za kanisani , kila wakati nikijiambia kuwa ni muhimu kuwa karibu Mungu''.

Cha kushangaza ni kwamba ni katika mazingira yake ya kawaida ya uraibu ndiposa alikutana na mume wake wakati huo akiwa mchumba wake.

Chanzo cha picha, RAHAB

Maelezo ya picha, Cha kushangaza ni kwamba ni katika mazingira yake ya kawaida ya uraibu ndiposa alikutana na mume wake wakati huo akiwa mchumba wake.

Hatahivyo habari za kifo cha ndugu yake zilimtumbukiza zaidi kwenye uraibu "anasema Rahab

Asijue la kufanya alijipata akitumia dawa za kulvya kama vile cocaine na heroinę.

Kufunga ndoa

Cha kushangaza ni kwamba ni katika mazingira yake ya kawaida ya uraibu ndipo sasa alikutana na mume wake wakati huo akiwa mchumba wake.

Hatahivyo mume wake ambaye hakuwa mraibu alielewa kuhusu hali yake na kila siku alikuwa anamzungumzia kuacha uraibu huo .

Licha ya hayo yote mume wake alikubali kumchumbia na hatimaye wakafunga ndoa .

"Wazazi wangu , pamoja na mume wangu walitembea nami katika kipindi hicho kizito na hata usiku wa mwisho kabla ya sisi kufunga ndoa, mama yangu aligundua bangi , sigara na madawa mengine ya kulevya mkobani mwangu'',anakumbuka.

''Nilikuwa nimewaandalia chakula cha jioni , hiyo siku nakumbuka niliapa kuwacha utumizi wa dawa za kulevya'',anasema.

Siku ya kufunga ndoa Rahab hakutumia madawa yeyote , anakumbuka alipokuwa akitembea mbele ya kanisa ili kufungishwa ndoa alililia sana , huku akimuomba Mungu kumpa ujasiri wa kusahau yaliyompata .

Alipohisi kwamba Mungu alikuwa na mpango wa kumtumia , hapo ndipo alianza kurudi nyuma na kuanza kutumia dawa za kulevya, "Rahab anakumbuka

Chanzo cha picha, RAHAB

Maelezo ya picha, Alipohisi kwamba Mungu alikuwa na mpango wa kumtumia , hapo ndipo alianza kurudi nyuma na kuanza kutumia dawa za kulevya, "Rahab anakumbuka

"Unajua wakati mwingi unapowaona bibi harusi wakidondokwa na machozi , usidhanie tu ni kutokana na umuhimu wa siku hiyo tu , wengine hutokwa na machozi kwa sababu tofauti , kwa mfano wanapokumbuka safari ya maisha yao "aliongezea Rahab

Safari ya mwisho

"Mwanzo wa ndoa mambo yalikuwa shwari, mume wangu ambaye pia ni Mchungaji alinipa ushauri na kunipatia nguvu ya kuishi bila utumiaji wowote wa madawa hayo .

Kama mke wa mchungaji pia mimi nilijitosa katika shughuli za kanisa , ila sikutamani kuwa mchungaji au kuwa na majukumu ya kuwa mtumishi kama mume wangu.

Alipohisi kwamba Mungu alikuwa na mpango wa kumtumia , hapo ndipo alianza kurudi nyuma na kuanza kutumia dawa za kulevya, "Rahab anakumbuka

Mwanamke huyo alirejelea maisha yake ya uraibu akitoroka majukumu ya uchungaji wa kanisa.

Mwanamke huyo alirejelea maisha yake ya uraibu akitoroka majukumu ya uchungaji wa kanisa.

Chanzo cha picha, RAHAB

Maelezo ya picha, Mwanamke huyo alirejelea maisha yake ya uraibu akitoroka majukumu ya uchungaji wa kanisa.

Anasema alianza kutumia bangi pamoja na madawa mengine wakati huo wote mume wake akiwa kazini.

Siku nyingine anasema kuwa aliamua kuwaacha wanawe wachanga nyumbani ili kwenda kutumia dawa hizo.

Kilikuwa ni kipindi kizito katika ndoa yake ,hadi mume wake alianza kuhisi iwapo alikuwa ameoa mwanamke ambaye sio sawa au la?

Anasema kwamba kama mke wa mchungaji alikumbana na changamoto chungu nzima si haba ikiwemo ile ya watu kuzungumzia tabia yake mbaya.

Kuacha dawa za kulevya

Cha ajabu mno , na ambacho sio kitu cha kawaida kutokea , mume wake hakumuacha wala kumtelekeza. .

Nyakati nyingi Rahab anasema kuwa walikuwa wanatembea na kushinda mchana kutwa pamoja na mume wake ili asije akateleza tena na kuanza uraibu.

Haijakuwa safari rahisi kwa Rahab ambaye amepigana na uraibu wa bangi pamoja na madawa mengine .

Akiwa mwanamke ambaye alizaliwa na wazazi wachungaji wa kanisa , na hatimaye kufunga ndoa na mwanaume ambaye pia aliingia kwenye kazi za uchungaji , hatimaye pia yeye alikubali wito wa kutumikia kanisa.

Baada ya kubadilika na kuamua kuwa mtumishi wa Mungu wengi walishangazwa na hatua yake ambapo aliweza kusimama kwenye madhabahu ya kanisa na kuhubiri.

Baada ya kubadilika na kuamua kuwa mtumishi wa Mungu wengi walishangazwa na hatua yake ambapo aliweza kusimama kwenye madhabahu ya kanisa na kuhubiri.

Chanzo cha picha, RAHAB

Maelezo ya picha, Baada ya kubadilika na kuamua kuwa mtumishi wa Mungu wengi walishangazwa na hatua yake ambapo aliweza kusimama kwenye madhabahu ya kanisa na kuhubiri.

Lakini kulingana na Bi Rahab uamuzi wake umekuwa chanzo cha kuwasaidia wengi waliopo kwenye uraibu wa madawa ya kulevya .

Anasema kuwa kama mwanamke ambaye alikuwa kwenye uraibu, na bado ni mtoto wa mchungaji , hali kadhalika mke wa mchungaji imekuwa sio rahisi kwake .

Rahab anasema kuwa mtu yeyote anaweza kujikuta kwenye uraibu kutokana na sababu tofauti katika jamii kama vile matukio mabaya ya maisha kwa mfano kifo cha mpendwa, magonjwa , ajali au kuchukiwa na watu, kuonekana kufeli katika maisha , kushirikiana na watu ambao wana uraibu , kupoteza mali au kazi mbali na kufeli katika mahusiano ya kimapenzi.

Hatahivyo anasema kuwa kila mtu ana uwezo wa kujinasua katika minyororo ya tatizo hilo huku akiongezea kwamba jamii haipaswi kuwahukumu waathiriwa wa janga hilo , bali kutafuta njia za kuwaleta karibu.

Kwa sasa Rahab Mwangi , mbali na kuwa mchungaji ni mtoa nasaha na mshauri dhidi ya uraibu wa madawa ya kulevya nchini Uingereza .

Kwa sasa Rahab Mwangi , mbali na kuwa mchungaji ni mtoa nasaha na mshauri dhidi ya uraibu wa madawa ya kulevya nchini Uingereza .

Chanzo cha picha, RAHAB

Maelezo ya picha, Kwa sasa Rahab Mwangi , mbali na kuwa mchungaji ni mtoa nasaha na mshauri dhidi ya uraibu wa madawa ya kulevya nchini Uingereza .