Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ulinzi : Fahamu kwanini Marekani, Uingereza, Iran, Australia, Uchina na Urusi zinazidi kuboresha majeshi yake
- Author, Yusuf Jumah
- Nafasi, BBC Swahili
Mataifa mengi yenye nguvu duniani na hata yasio na uthabiti wa kiuchumi yamezidi kununua zana za kivita katika hali ambayo imeanza kuzua maswali kuhusu kinachosababisha nchi hizo kujihami kwa kasi na wakati huu .
Tathmini ya bajeti za ulinzi za nchi kubwa kama vile Marekani , China na Urusi zinaonyesha kwamba mataifa hayo yamezidi kutanua uwezo wake kujilinda dhidi ya vitishi mbali mbali .Hatua hiyo pia imezifanya nchi ambazo hapo awalia hazikuwa na bajeti kubwa ya Ulinzi kama vile Japan na Australia kuimarisha zana zake na kuendelea na mipango ya kujiboresha ,ardhini ,majini na angani kwa zana za kisasa .
Licha ya kutokuwepo vita vikubwa vinavyoendelea , baadhi ya nchi zimekuwa zikiendelea na mipango kabambe ya kununua zana za kila aina .
Marekani kwa mfano inatumia kiasi kikubwa sana cha fedha za bajeti yake ya ulinzi kuziliko nchi kumi za kwanza zenye bajeti kubwa. Bajeti yake ya ulinzi sasa ni dola milioni 738 (£557bn) kwa mwaka
Marekani
Aliyetangulia kutoa ishara kwamba Marekani inalenga kuendelea na mpango wa kuzidisha bajeti yake ya ulinzi ni aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump mwaka wa 2016 alipochukua madaraka na kusema taifa hilo lilikuwa na mpango wa ' kuzidisha uwezo wake wa kinyuklia'. Alisema Marekani ilifaa kuchukua hatua hiyo hadi ulimwengu 'ufahamu hatari ya na nguvu za nyuklia'.
Hatua hiyo ilizitisha nchi nyingi hasa ambazo hujipata zikilumbana na Marekani kama vile China ,Urusi na Iran ambazo pia zilizidisha mipango ya kujihami hata zaidi .
Marekani ina silaha 7000 za nyuklia ,Urusi ina 7300 kulingana na shirika la US nonpartisan Arms Control Association.
Uingereza
Ingawaje Uingerza imetangaza kwamba inalenga kupunguza idadi ya maafisa wake katika jeshi kufikia mwaka wa 2025 , imekuwa vigumu kuichukua hatua hiyo kwa njia rahisi kwnai raslimali Zaidi zimetolewa kwa mipango mingine ya kuboresha uwezo wa Ungereza kujilinda na kuwapa kinga washirika wake katika hali yoyote ya kivita .
Ingawa idadi ya wanajeshi itashuka, bajeti ya ulinzi ya kila mwaka ya Uingereza itakuwa Pauni 7bn kwa mwaka kuliko ilivyokuwa hapo awali, ifikapo 2024-25.
Ilikuwa imeripotiwa sana kwamba serikali ingekuwa ikitangaza kupunguzwa kwa wanajeshi 10,000 kwa ukubwa wa Jeshi, lakini hilo sio litakalotokea kabisa .
Kinachokatwa ni shabaha ya idadi ya watu waliofunzwa kikamilifu katika Jeshi
Wakati Uingereza inaingia 10 bora kwa matumizi, inakuja chini kwenye orodha kwa suala la idadi ya wanaohudumu katika jeshi
Takwimu kutoka Benki ya Dunia za mwaka wa 2018 inaiweka Uingereza katika nafasi ya 42, nyuma ya India, China, Korea ya Kaskazini, Urusi na USA kwa matumizi .
Katika mwaka wa 2019 Uingereza ilitumia 2.1% ya Pato la Taifa kwa ulinzi.
Tangu 2014, Nato imeweka lengo kwa wanachama wake kutumia 2% ya Pato la Taifa kwa ulinzi.
Walakini, kumekuwa na ukosoaji unaozingira mbinu inayotumiwa kuhesabu nambari hizi, kama vile pensheni za vita zinahesabu kama matumizi ya ulinzi.
China
Mnamo mwaka wa 2017 China ilisema itazidisha bajeti yake ya ulinzi kwa asilimia 7 muda mfupi tu baada ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kutangaza kwamba alilenga pia kuongeza matumizi ya fedha katika jeshi la Marekani .
China imekuwa ikifanya jeshi lake kuwa la kisasa hivi karibuni wakati uchumi wake unapanuka.
Bajeti ya ulinzi ya China iliyotangazwa inabaki ndogo kuliko ile ya Marekani . Lakini wachunguzi wengi wa China wanasema kuwa takwimu halisi inaweza kuwa kubwa zaidi.
Tangazo hilo linaashiria mwaka wa pili mfululizo kwamba ongezeko la matumizi ya ulinzi ya China imekuwa chini ya 10% kufuatia karibu miongo miwili .Inamaanisha kuwa jumla ya matumizi yatashughulikia karibu 1.3% ya Pato la Taifa lililokadiriwa mnamo 2017, kiwango sawa na miaka ya hivi karibuni, alisema msemaji wa serikali wakai huo Fu Ying.
Beijing imekuwa ikijenga visiwa vya kujitengezea kwenye miamba katika bahari zinazopakana na mjairani zake na katika mataifa mengine kwenye Bahari ya Kusini ya China.
Kutetea haki yake ya kujenga, China ilisema hapo zamani kuwa haina nia ya kupigania visiwa, lakini imekiri kujenga kile inachokiita vituo muhimu vya jeshi kwa sababu za kujihami.
Kumekuwa na matukio ya hapa na pale kati ya meli za Marekani na Wachina katika Bahari ya Kusini ya China.
Meli za Wachina pia zimehusika katika mapigano na uchokozi na meli kutoka Vietnam na Ufilipino.
Japani ilitia saini bajeti kubwa zaidi ya ulinzi miaka miwili iliyopita huku ikikabiliwa na mizozo maeneo na Uchina katika Bahari ya China ya Mashariki na vitisho vya nyuklia na makombora ya Korea Kaskazini.
Australia
Australia itatumia $ 580m kuboresha vituo vinne vya kijeshi kaskazini mwa nchi hiyo na kupanua mazoezi ya vita na Marekani , Waziri Mkuu Scott Morrison anatarajiwa kutangaza Jumatano, kulingana na dondoo za tangazo lililotazamwa na shirika la habari la Reuters.
Uwanja wa ndege katika eneo la Kaskazini utapanuliwa kusaidia ndege kubwa, safu za kurusha zimebadilishwa na vifaa vipya vya mafunzo vilivyowekwa kwa wafanyikazi wa ulinzi na majini kutoka Marekani .
Australia na Marekani hufanya mazoezi ya kivita ya kila baada ya miaka miwili, ambayo inayofuata imepangwa kuanza mnamo Agosti.
Australia pia inatarajiwa kujiunga na mazoezi ya kijeshi ya mataifa mengi yanayojumuisha Marekani, Uingereza, Japani, India na nchi nyingi.
Kwa kawaida, zaidi ya wanajeshi 30,000 hushiriki katika mazoezi hayo kutoka pwani ya mashariki mwa Australia.
Australia na China pia zimetofautiana juu ya Hong Kong, na Canberra ikionyesha kupinga sheria ya usalama wa kitaifa ya Uchina iliyowekwa kwa koloni hiyo ya zamani ya Uingereza na hatua hiyo imezua hali ya hofu ya uwezekano wa mgogoro wa kivita baina ya nchi hizo mbili.
Iran
Uwezo wa Iran kujihami kwa kiwango na kasi kama ya nchi nyingine umeathiriwa na vikwazo vya muda mrefu lakini hilo halijaizuia kuendelea na mipango ya kuboresha jeshi lake na kujitayarisha dhidi ya vitisho kutoka nchi nyingine .
Iran imejitambua kwa kuunda makombora mbali mbali katika miaka ya hivi karibuni mengine yenye uwezo wa kufika hata katika nchi ya Israel ambayo hulumbana nayo mara kwa mara . Baada ya kuuawa kwa kamanda wa jeshi lake nchini Iraq Jenerali Qasem Soleimani ,Iran ilijibu kwa kurusha makombora kadhaa ndani ya Iraq ikizilenga kambi za kijeshi zinazotumiwa na Marekani
Iran ina makombora yapi?
Mifumo ya makombora ya Iran ni sehemu muhimu ya silaha zake za kijeshi kutokana na ukosefu wake wa nguvu za anga.
Wapinzani wake kama Israeli na Saudi Arabia wana teknolojia ya kufanya mashambulio ya angani.
Iran kwa kiasi kikubwa haina uwezo huu na kwa hivyo inategemea kuzindua makombora.
Ripoti ya Idara ya Ulinzi ya Marekani inaelezea vikosi vya makombora vya nchi hiyo kuwa kubwa zaidi Mashariki ya Kati.
Haiwezekani kutoa takwimu sahihi lakini Kituo cha Kimkakati na Mafunzo ya Ulinzi cha Marekani kinasema Iran ina maelfu ya makombora ya aina zaidi ya dazeni tofauti.
Chombo cha habari cha Irani kiliripoti kuwa makombora ya Fateh na Qiam yalitumika katika shambulio hilo kwenye kituo cha Marekani.
Wachambuzi wa kijeshi pia wameelezea utumiaji wa aina hizi kulingana na picha za tovuti za mashambulio.
Kombora la Qiam-1 limetengenezwa sana tangu 2011, lina uwezo wa kufika umbali wa kilomita 700 pamoja na vilipuzi. Ilitumiwa na Iran dhidi ya wapiganaji wa IS mnamo Juni 2017.
Tofauti za kombora la kati la Shahab-3 la kati lina uwezo wa kubeba uzani wa kilo 750 na upeo wa zaidi ya kilomita 1,500.