Ramadhan: Wasio Waislamu wanaofunga mwezi wa Ramadhan

Nadyne Parr (kulia) na rafiki yake Soraya Deen,

Chanzo cha picha, Handout

Maelezo ya picha, Nadyne Parr (kulia) na rafiki yake Soraya Deen,

Rehan Jayawickreme, mwanasiasa kijana anayewakilisha chama cha' upinzani nchini Sri Lanka, alitangaza kile kilichowashutua wengi Aprili 13.

"Mimi ni wa dini ya kibudha na najitahidi kwa kila namna kufuata falsafa ya maisha ya Kibudha," alisema kwenye mtandao wa Twitter.

"Baada ya kusema hivyo, nasubiri kwa hamu na ndugu zangu Waislamu kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan. Itakuwa mwezi wangu wa kwanza naomba munitakie kila la kheri."

Ni mwenyekiti wa Baraza la Mijini la kusini mwa Sri Lanka mji wa Weligama na tangu Ramadhan ilipoanza Aprili 14, amekuwa akijizuia kula na kunywa nyakati za mchana.

Ni sadfa isiyo ya kawaida mwaka huu, Waislamu huko Sri Lanka, nchi ambayo waumini wake wengi ni wa Kibudha walianza kufunga siku ya kwanza ya mwezi wao, siku moja na jamii za Sinhala na Tamil wakisherehekea mwaka wao mpya.

Lakini chama cha wenye imani tofauti tofauti cha Sri Lanka kilipata mshutuko mkubwa karibu miaka miwili iliyopita pale wanamgambo wa Kiislamu walipotekeleza mashambulizi makanisani wakati wa sherehe za sikukuu ya pasaka na kusababisha vifo vya watu karibu 270.

Mwanasiasa wa imani ya Kibudha anasema uamuzi wake wa kuungana na Waislamu katika kufunga mwezi wa Ramadhan unalenga kukabiliana na matamshi ya kupinga Uislamu yaliyosemwa na washambuliaji hao.

Mtandao wa Twitter wa Rehan Jayawickreme ulipokea maoni mengi ya watu waliojibu ujumbe wake ambao wanaunga mkono anachofanya lakini pia aliweka wazi kuwa kusherekea mwezi wa Ramadhan ingawa yeye sio Mwislamu halikuwa jambo la kipekee kwake.

Marianne David, mwanahabari mwenye makao yake Sri Lankan katika mji wa Colombo, alisema kwamba amekuwa akifanya hivyo kwa muda sasa.

"Mimi ni Mkatoliki na huwa ninafunga wakati wa Ramadhan pia. Inaleta uwazi, hamasisho, rehema na nidhamu. Kila la Kheri!" alisema.

Anuradha K Herath, Mkurugenzi Mkuu wa masuala ya kimataifa katika ofisi ya Waziri Mkuu, alisema kuwa pia yeye aliwahi kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan mara moja.

"Nakumbuka kufanya vivyo hivyo siku zangu nikiwa chuo kikuu cha Moratuwa miaka mingi iliyopita," aliandika kwenye mtandao wa Twitter.

"Rafiki yangu @sifaan alikuwa akiamka mapema kila asubuhi kula chakula na kuwapa wengine vitafunio wakati anatoa mhadhara kwa wanafunzi nyakati za mchana kwa ajili ya kufungua. Nafkiri itakuwa tajriba nzuri."

Rehaan Jayawickreme [wa pili kutoka kushoto) anakamlisha siku yake na marafiki zake Wasialmu

Chanzo cha picha, Handout

Maelezo ya picha, Rehaan Jayawickreme [wa pili kutoka kushoto) anakamlisha siku yake na marafiki zake Wasialmu

Kukemea ubaguzi

"Nilifikiria kufanya hivi kama ishara ya kupinga ubaguzi kunakoendelezwa na baadhi ya viongozi nchini mwetu," amesema Rehan Jayawickreme. "Sio kwamba nimebadilika na kuwa Mwislamu lakini ninapinga ubaguzi."

Alizungumza na BBC kuwa jamii ya waliowachache ya Waislamu. Sri Lanka imeingiwa na hofu tangu kulipotokea mashambulizi sikukuu ya pasaka.

Karibu asilimia 70 ya idadi ya watu Sri Lanka ni waumini wa Kibudha. Waliosalia ni Wahindu, Waislamu na Wakatoliki.

"Nitakapoonesha Waislamu kuwa kama tulio wengi, tunawajali, tunatarajia kuwa watatambua nia ya lengo fulani na kuhisi usalama. Na kuwaonesha kwamba tunawajali."

Baadhi ya wakosoaji wake wamemshutumu Rehan Jayawickreme kwa kufuata fuata Waislam ili wakubali anachofanya na kumuunga mkono. Na kama njia moja ya kujibu, mwanasiasa huyo anakumbuka maneno ya mfuasi wake mmoja kwenye mtandao wake wa Twitter:

"Ni kheri zaidi kupata kura kwa njia ya kuendeleza umoja wa kidini badala ya kusababisha chuki."

'Lisha wengine'

Mwanahabari Marianne David, Mkatoliki, amekuwa akifunga mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa zaidi ya miaka 15. Anasema hutumia muda huu kujiakisi tena kuhusiana na masuala yenye umuhimu mkubwa maishani mwake.

Kufunga kunaondoa mchakato wa kila saa kufikiria juu ya chakula utakachokula, au kukosa utulivu kwasababu ya chakula na kula bila malengo yoyote kila wakati, kwasababu tu mtu ni mvivu au ametamani kula kitu hicho. Ina leta nidhamu zaidi na utaratibu kwa siku hiyo."

Anaamini kuwa utamaduni huo ulimfanya awe mwangalifu zaidi na kumfanya ahisi kuwa na afya njema zaidi.

"Sio kwamba ni vigumu sana kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa wale ambao tayari wanafurahia mambo fulani kwa misingi ya kiwango chao cha maisha na kazi wanazofanya," aliiambia BBC.

"Ni mtihani mkubwa sana kwa wanaofanya kazi za dhorubu au kufanyakazi nje kipindi cha joto kama hiki huku watu wakiwa hawana pesa za kula chakula kizuri, chenye afya kipindi hiki."

Kwake yeye, cha msingi wakati wa Ramadhan ni kufikiria kuhusu wale wasioweza kupata chakula nchini Sri Lanka.

Kutoa ni muhimu sana, anasema. "Nafikiri kile kilicho muhimu wakati tunajinyima ni kusaidiana kadiri ya uwezo wetu, kulisha wengine wale wasio na chochote na kuwasaidia kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa kusaidia kukimu mahitaji yao."

Mshikamano

Upande mwingine wa dunia, Nadyne Parr kutoka Marekani ni mwengine asiye Mwislamu ambaye anafunga mwezi mtukufu wa Radhaman. Mkristo mcha Mungu, alitambulishwa kwenye Uislamu na rafiki yake, Mwislamu mwanamke.

"Ni kitendo cha mshikamano kutoka kwa rafiki zangu Waislamu pamoja na kwamba ni tabia ya kawaida kwa imani yangu yenyewe, nikiwa mfuasi wa Yesu, ninapochagua kufunga mwezi wa Ramadan."

Nadyne ni mwandishi, mtaalamu wa biashara na mwalimu wa shule katika jimbo la Michigan.

Marianne David

Chanzo cha picha, Handout

Maelezo ya picha, Mwandishi wa habari Marianne David, ambaye ni makatoliki amekuwa akifunga Ramadan kwa zaidi ya miaka 15

"Imekuwa muda sasa, lakini kwa kipindi cha miaka saba nimekuwa nikifuatilia kwa karibu masharti ya kunywa maji, nimekuwa nikifuatilia kwa karibu miongozo ya mwezi wa Ramadhan... kupata kiamsha kinywa kabla ya jua kuchomoza na kujizuia kula chakula hadi jua litakapo tua," amesema

Wakati wa kuja pamoja

Nchini Sri Lanka, Marianne David anapenda kusisitiza kuwa "sio tu kuhusu kujinyima na nidhamu, pia ni wakati wa kuja pamoja, kushikamana na kusherehekea na wapendwa wako ".

"Tunapokwenda kufurahia au tukiwa na familia wakati wa kufungua, huwa ni kama kula pamoja chakula cha jioni, isipokuwa huwa tu hakuna kinywaji cha pombe," amesema, "Huwa tunakula chakula kipya na kufurahia hata kama kiwango unachokula kinapungua baada ya siku kadhaa.

Chakula cha Iftar cha Marraiane wakati anapofungua jioni

Chanzo cha picha, Handout

Maelezo ya picha, Chakula cha Iftar cha Marraiane wakati anapofungua jioni

Kwa Nadyne, kufunga kumekuwa sehemu muhimu ya maisha yake ya kiroho.

Anaamini kukaa bila kula kwa muda wala kunywa maji kunafanya imani yake kuwa na mtazamo mpya.

"Tunaangazia zaidi ya mahitaji yetu. Mahitaji yetu yanapitiwa tena na pia tunapitia kipindi muhimu na Mungu wetu."

Sio rahisi

Lakini kwa Rehan Jayawickreme, anasema tajriba mpya haijakuwa rahisi vile.

Nadyne Parr

Chanzo cha picha, Handout

Maelezo ya picha, Nadnye Parr amekuwa akifunga mwezi wa Ramadan katika kipindi cha miezi saba iliopita

"Nina amka saa kumi asubuhi na kula tende kidogo, maziwa ya mtindi na matunda kama kiamsha kinywa. Na si kula chochote hadi saa kumi na mbili unusu jioni," aliiambia BBC.

"Nitaendelea kadiri ninavyoweza," amesema mwanasiasa wa Kibudha. Lakini akaongeza kuwa, "ni vigumu sana kukaa bila kunywa maji"