Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Caron Nazario: Afisa wa polisi aliyempulizia pilipili mwanajeshi wa Marekani afutwa kazi
Afisa wa polisi huko Virginia amefutwa kazi baada ya kumnyooshea bunduki, na kumpulizia pilipili, Luteni mweusi wa jeshi la Marekani wakati alipomsimamisha barabarani
Luteni wa Pili wa Jeshi Caron Nazario amevaa sare yake katika picha za video za kamera ya polisi wakati wa tukio hilo la mwezi Diesemba mwaka jana.
"Ninaogopa kutoka nje," anawaambia maafisa wawili wa polisi. "Ndio, unapaswa kuogopa," afisa anasema.
Polisi walisema alisimamishwa kwa kushindwa kuonyesha nambari za usajili lakini inaonekana kwenye video.
Luteni Nazario alifungua kesi dhidi ya maafisa hao wawili, Joe Gutierrez na Daniel Crocker, wiki hii.
Katika taarifa, maafisa katika mji wa Windsor huko Virginia walisema tukio hilo limesababisha "hatua za kinidhamu, na mahitaji ya idara nzima ya mafunzo ya ziada yalitekelezwa kuanzia Januari na kuendelea hadi sasa".
"Tangu wakati huo, Afisa Gutierrez pia alisimamishwa kazi," iliongeza.
"Mji huo pia umeomba uchunguzi wa tukio hilo na Polisi wa Jimbo la Virginia, na unajiunga na maafisa waliochaguliwa ambao wametaka tathmini kamili vitendo vya maafisa hawa kufanywa."
Siku ya Jumapili, Gavana wa Virginia Ralph Northam alisema kuwa tukio hilo "lilikuwa la kusumbua" na "lilikuwa limemkasirisha".
Ni kipi kilichofanyika?
Wakati wa tukio hilo askari huyo, ambaye alikuwa amefungwa pingu wakati gari lake likikaguliwa , aliuliza ni kwanini nguvu ilikuwa ikitumika dhidi yake. Aliambiwa na afisa wa polisi: "Kwa sababu haushirikiani."
Baadaye aliachiliwa bila kufunguliwa mashtaka.
Mapema wiki hii Luteni Nazario aliwasilisha kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Marekani ya Norfolk, Virginia, dhidi ya maafisa hao wawili wa Idara ya Polisi ya Windsor.
Kulingana na kesi hiyo, Luteni Nazario alinyunyiziwa pilipili na kugongwa chini na maafisa hao. Picha za kamera ya mwilini zinaonyesha maafisa hao wakionesha bunduki zao kwa Luteni.
Kesi hiyo inadai ukiukaji wa haki zake za kikatiba, na inajumuisha kushambuliwa, upekuzi haramu na kuwekwa kizuizini kinyume cha sheria.
Kesi hiyo inakuja wakati wa pana uchunguzi zaidi juu ya madai ya ukatili wa polisi kwa watu wachache na weusi.
Afisa wa polisi wa zamani Derek Chauvin kwa sasa anakabiliwa na kesi ya mauaji ya George Floyd. Picha za Bw Chauvin, ambaye ni mweupe, akiwa amepiga goti kwenye shingo ya Mr-Floyd ambaye ni Mmarekani mweusi wakati wa kukamatwa ilisababisha maandamano ya ulimwengu dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Ni kipi kingine tunachofahamu?
Luteni Nazario, ambaye ni Mlatino mweusi , alikuwa amevaa sare na alikuwa akiendesha gari na karatasi ya leseni ya muda kwenye dirisha lake la nyuma mnamo Desemba 5, alipoambiwa asimame alipokuwa akiingia mji wa Windsor.
Kisha akasimama katika kituo cha mafuta na kuweka mikono yake nje ya dirisha, huku akiwauliza polisi kwa nini alikuwa akisimamishwa.
Wakili Jonathan Arthur, anayemwakilisha Lt Nazario katika kesi hiyo, alisema kwamba afisa wa jeshi alijua ni muhimu kuitoa nje mikono yake
" Kujifungua mkanda wake au kufanya lolote -alihofia angeuawa' Bw aliiambia CBS.