Wanasayansi kutegua kitendawili cha 'komputa ya kale zaidi duniani'

Image shows a model of the device

Chanzo cha picha, Prof Tony Freeth / UCL

Maelezo ya picha, Wanasayansi wametumia uundaji wa chombo hicho tata cha zamani kutengeneza komputer inayotumia mfumo wa aina hiyohiyo

Chombo kilichotengenezwa miaka 2,000-iliyopita ambacho hutajwa kama 'komputa ya kale zaidi' duniani imetengenezwa na wanasayansi wakijaribu kuelewa jinsi inavyofanya kazi.

Utendaji kazi wa chombo hicho uliwaumiza kichwa wataalamu tangu ilipopatikana katika ajali ya meli ya warumi nchini Ugiriki mwaka 1901.

Kifaa hicho cha kale kilichopatikana Ugiriki kilidhaniwa kuwa kilitumika kutabiri kupatwa kwa jua na matukio mengine ya angani.

Lakini ni theluthi tu ya kifaa hicho kilibaki , na kuwaacha watafiti kuhangaika kujua namna kilivyokuwa kinafanya kazi na namna kilivyokuwa kinafanana.

Sehemu ya nyuma ya chombo hicho ilitengenezwa na wanasayansi wa awali lakini uhalisi wa jinsi inavyofanya kazi katika sehemu ya mbele ilibaki kuwa kitendawili.

Wanasayansi wa chuo kikuu cha London (UCL) wanaamini kuwa hatimaye wamefanikiwa kujua namna komputa hiyo ilivyokuwa inafanya kazi.

Wameweza kutengeneza sehemu ya mbele na sasa wanategemea kutengeneza komputa ya aina hiyo kwa kutumia vifaa vya kisasa.

Image shows a piece of the Antikythera Mechanism at museum in Greece

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Ni theluthi tu ya sehemu ya kifaa hicho ndio kipo sawa, huku chombo hicho kikiwa na vipande zaidi ya 80

Siku ya Ijumaa, gazeti lilichapisha ripoti ya wanasayansi ikionesha muonekano mpya na jinsi ilivyoundwa .

"Jua, mwezi na sayari zinaonekana kwa kupendeza katika chombo hiki cha kale kilichopatikana Ugiriki ," kiongozi wa utafiti, Profesa Tony Freeth, alisema.

"Huu ni mfano wetu wa kwanza unaodhihirisha ushaidi wote wa kifizikia ambao unalingana na vielelezo vya kisayansi vilivyopo kwenye chombo hiki ," aliongeza.

Mfumo huu unaeleza kuwa ndio ulitumika kama komputa ya kwanza kutumika duniani.

Ilitengenezwa kwa shaba na inajumuisha gia kadhaa.

Sehemu ya nyuma ina maelezo yanayoonesha ulimwengu , ambapo inaonesha mwendo wa sayari tano ambazo zilijulikana wakati kifaa kilipotengenezwa.

Lakini sehemu 82 zilizoharibika- zilizunguka theluthi ambayo ilikuwa nzima katika kifaa hicho, hii ina maanisha wanasayansi waliunganisha hivyo vipande kwa kupiga picha kwa data za X-Ray na mfumo wa mahesabu ya kigiriki .

line