Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Milima ya dhahabu DR Congo: Tunachojua kuhusu kanda ya video iliosambazwa sana
Serikali ya DR Congo ililazimika kutuma maafisa wa polisi ili kuimarisha usalama katika eneo ambalo kanda moja ya video iliwaonyesha wanavijiji wakichimba dhahabu kwa wingi, kwa miujibu wa mtandao wa BBC Pidgin.
Je mlima huo wa dhahabu uko wapi?
Mwandishi wa BBC nchini DR Congo Byobe Malenga anasema kwamba mlima huo uliovamiwa na wanavijiji upo kilomita 35 kaskazini mwa eneo la Bukavu ndani ya mji mkuu wa mkoa wa Kusini mwa Kivu.
Habari za hivi karibuni zinasema kwamba serikali ililazimika kutuma maafisa wa polisi ili kuweka amani na kuchukua dhahabu ambayo wanaviji hao walikuwa wakichimba kwa wingi.
Taifa la DR Congo lina utajiri wa madini ikiwemo dhahabu na mlima uliokuwepo ndani ya video hiyo ni eneo lililosajiliwa ambapo lina wafanyakazi wake.
'Sio wote waliokuwa katika kanbda hiyo ya video walikuwa wafanyakazi wa mgodi huo'', alisema Byobe Malenga.
Ijapokuwa kanda hiyo ya video ilianza kusambaa siku ya Jumanne , Malenga anasema tukio hilo lilijitokeza wikendi iliopita siku ya Jumamosi.
Anasema kwamba mlima huo una kati ya asilimia 60 hadi 90 ya dhahabu.
Je video hiyo ilikuwa inaonesha nini?
Kanda hiyo ya sekunde 30 iliwaonesha wanaviji wengi juu ya mlima wakikusanya vipande vidogo vya dhahabu kutoka ardhini .
Upande mwengine wa kanda hiyo kuna watu wanaoonekana wakiosha dhahabu inayotoka katika mchanga mwekundu .
Idadi ya wakaazi hao ilidaiwa kufikia mamia
Mzozo wa dhahabu DR Congo
Shirika la Human Rights Watch linasema kwamba dhahabu ndio raslimali kubwa inayotegemewa na taifa hilo lakini kwasababu ni watu wachache wanaojinufaisha na madini hayo raia wengi wanasema hakuna usawa.
Hali hiyo imesababisha ujio wa makundi ya wapiganaji ambayo yamekuwa yakizozana na kusababisha maafa makubwa.