Fahamu kundi linaloihangaisha Nigeria licha ya kuwa na jeshi kubwa

Nigeria imekuwa ikipambana na kundi la kigaidi la Boko Haram tangu mwaka wa 2009 bila mafanikio .Je Boko Haram linasimamia nini na mbona linaihangaisha serikali ya Nigeria na mataifa mengine yanayopakana na nchi hiyo ?

Chimbuko

Kundi hilo lilianzishwa mwaka wa 2009 na linafanya maasi dhidiya serikali ya Nigeria ili kuanzisha utawala wa kijihadi wenye kutegemea mafunzo ya itikadi kali za kidini .

Kundi hilo limekuwa likifanya mashambulizi dhidi ya raia na maafisa wa usalama wa Nigeria kaskazini mwa nchi hiyo na pia kuwaacha maelfu ya watu bila makao .

Kati ya mwaka wa 2014 na 2015 idadi ya watu waliouawa na mashambulizi ya kundi hilo ilipungua kabisa kabla ya kuongezeka baada ya msururu wa makabiliano na maafisa wa usalama wa Nigeria .

Imechukua juhudi za majeshi ya nchi kadhaa zinazopakana na Nigeria kujaribu kupunguza makali ya nchi hiyo kama vile Benin , Cameroon, Chad na Niger lakini juhudi hizo zimetuliza tu mashambulizi ila hazijamaliza kabisa nguvu za kundi hilo la kigaidi .Mojawapo ya sababu zinazotajwa na wadadisi kusababisha Nigeria kushinda kuimaliza nguvu Boko Haram ni madaiya ufisadi jeshini .

Kumekuwa na ripoti za wanajeshi wa Nigeria kutoroka wakati wanapopata ripoti za uwezekano wa kushambuliwa na magaidi ya Kundi hilo hatua ambayo imelipa nguvu kundi hilo katika miaka ya nyuma .

Utekaji nyara

Kundi hilo lilibadili mtindo wake wa oparesheni kwa kuanza kuwateka nyara wanafunzi katika majimbo ya kaskazini mwa nchi hiyo na mwaka wa 2018 liliwateka nyara wanafunzi 100 wa shule moja walioachiliwa baada ya mwezi mmoja.

Makabiliano kati ya majeshi ya serikali na Boko Haram yamekuwa yakitokea katika jimbo la Borno na mwaka wa 2018 Nigeria ilitangaza kwamba imefaulu kuwarejesha makwao maelfu ya watu waliokuwa wametoroshwa na machafuko ya Boko Haram .

Mwaka wa 2014 kundi hilo liliwateka nyara wanafunzi zaidi ya 200 katika shule yao na baadaye Zaidi ya 100 waliachiliwa baada ya serikali kutafuta msaada wa shirika la msalaba mwekundu .

Rais Muhammadu Buhari aliyemshinda Goodluck Jonathan alichaguliwa mwaka wa 2015 kupita ahadi ya kulangamiza kundi hilo lakini hadi sasa hajafaulu kulizima nguvu Boko haram ambalo februari mwaka huu limewateka nyara makumi ya wanafunzi wavulana kutoka shule moja ya serikali .

Ripoti zaashiria kwamba Boko Haram imekuwa ikifanya ushirikiano na makundi mengine ya kijihadi katika kanda hiyo na hata mwaka wa 2015 liliapa kuliunga mkono kundi la Islamic State hatua iliyofanya Nigeria kuitisha usaidizi zaidi wa kijeshi kutoka kwa Marekani ili kukabiliana na hatari ya kundi hilo .

Usalama wa Nigeria ni muhimu sana kwani kama nchi inayozalsha mafuta kwa wingi Afrika ,kutegemewa kwake na nchi nyingi na maslahi ya Marekani ni jambo lenye uzito wa kipekee .