Tiger Woods apata majeraha kadhaa, afanyiwa upasuaji kufuatia ajali mbaya

Tiger Woods amekuwa akifanyiwa upasuaji baada ya kupata ''majeraha kadhaa ya mguu'' katika ajali ya gari mjini Los Angeles.
Mshindi mara 15 wa mchezo wa gofu, mwenye miaka 45 ''alitolewa kwenye eneo la ajali'' na wahudumu wa zima moto na wahudumu wa afya. Mkuu wa polisi Alex Villanueva baadae alisema kuwa Woods ''alikuwa hai na mwenye fahamu'' katika eneo la ajali.
Kisha alipelekwa hospitalini kwa gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya cha UCLA huko West Carson, California.
Wakala wa Woods, Mark Steiberg alithibitisha kuwa alikuwa akifanyiwa upasuaji siku ya Jumanne na kutoa taarifa kuhusu majeraha yake.
Woods was at the Riviera Country Club in Los Angeles at the weekend as host of the Genesis Invitational tournament.
Woods alikuwa katika klabu ya Riviera mjini Los Angeles mwishoni mwa juma akihodhi
Katika mkutano na wanahabari , mkuu wa idara ya zimamoto ya kaunti ya LA Darlyl Osby alisema kuwa Woods aliondolewa kwenye gari aina ya GV80 luxury SUV kwa kutumia shoka.
Aliongeza: ''ninaelewa kuwa ni majeraha mabaya kwa miguu yake yote. Hakukuwa na majeraha mengine yaliyohatarisha maisha yake ninavyofahamu.''
Villanueva alisema kuwa gari la Woods "eneo lilivuka katikati ya barabara iliyogawanywa kisha ikasimama umbali wa mita mia ikionesha kuwa walikuwa wakienda kwa kasi kubwa kuliko kawaida".
Alisema gari iligonga kigingi, mti kisha ikapinduka mara kadhaa.
''Tumekuwa tukiwasiliana na meneja wake na hawajataka nizungumze chochote kuhusu hali yake. Tunachokijua ni kuwa hali ni mbaya kutokana na ajali hiyo,'' aliongeza.

Chanzo cha picha, Getty Images
Naibu Carlos Gonzalez, kutoka idara ya polisi wa LA , alikuwa wa kwanza kufika kwenye eneo la tukio na kusema kuwa Woods ''hakuwa na uwezo wa kusimama mwenyewe'' kabla ya kuondolewa kwenye gari.
Alisema kuwa Woods alikuwa amevaa mkanda wake na "alikuwa bado mtulivu " alipomwambia jina lake.
"Ni bahati sana kwamba Bw Woods aliweza kutoka kwenye gari akiwa hai," aliongeza.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Mchezaji bora nambari tatu duniani Justin Thomas alisema ''tumbo linauma, unajua inaumiza kuona mmoja wa marafiki zako wa karibu akipata ajali. Nina matumaini anaendelea vizuri. Nina wasiwasi na watoto wake , nina hakika wanapitia kipindi kigumu .''
Kamishna wa Shirikisho la mchezo wa gofu Jay Monahan alisema: '' Tunasubiri taarifa zaidi atakapotoka kwenye upasuaji.
''Kwa niaba ya shirikisho na wachezaji wetu, Tiger yuko kwenye maombi yetu na tutampa ushirikiano wakati akirejea katika hali yake.''
Woods alihusika katika ajali ya gari mnamo Novemba mwaka 2009 ambayo mwishowe ilisababisha kukiri kwa kutokuwa mwaminifu na kuvunjika kwa ndoa yake. Kisha akapumzika kucheza gofu lakini akarudi muda mfupi baadaye.
Kufuatia ushindi mara tano mwaka 2013, Woods alianza michezo 24 katika kipindi cha miaka 4 kwa sababu maumivu makali ya mgongo na upasuaji wa mara kadhaa.
Mnamo mwaka wa 2017 Woods alikamatwa kwa tuhuma za kuendesha gari chini ya ushawishi wa pombe alipopatikana amelala kwenye gari lake. Baadaye alikutwa na hatia ya kuendesha gari hovyo.












