Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Lisa Montgomery: Utafutaji majibu katika maisha ya muuaji
Wanasheria wa Montgomery wamesema watawasilisha ombi kwa majaji kutafakari uamuzi wao wakidai kuwa mteja wao ni mwathirika wa matatizo ya akili kutokana na unyanyasaji aliopitia kwa hiyo anahitaji huruma.
Kwa Diane Mattingly, kuna wakati mmoja katika utoto wake ambao anahisi kushukuru lakini pia mwenye kujihukumu.
Kipindi hiki, anajipongeza kwa maisha ambayo kidogo yalikuwa kawaida - katika nyumba ndogo, akiwa na uhusiano mzuri na watoto wake na kwa karibu miongo miwili amekuwa akifanyakazi katika jimbo la Kentucky.
Vilevile, analaumu kipindi hicho kwa kilichomtokea dada yake wa kambo, Lisa Montgomery.
Montgomery amepangiwa hukumu ya kifo Jumanne kwa njia ya kunyongwa kwa makosa ya kumyonga mwanamke aliyekuwa na ujauzito wa miezi 8.
Desemba 2004, Montgomery, ambaye alikuwa, 36, wakati huo, alimkata tumbo Bobbie Jo Stinnett na kumtoa mtoto aliyekuwa amembeba tumboni na kumteka nyara. Stinnett alivuja damu hadi akafariki dunia.
Mattingly na Montgomery waliishi pamoja hadi Mattingly alipokuwa na umri wa miaka minane na dada yake wa kambo akiwa na umri wa miaka minne.
Ilikuwa ni nyumba yenye kuogofya, anasema, ambapo walipitia unyanyasaji wa kimwili na kiakili mikononi mwa Judy Shaughnessy, mama yake Montgomery na mchumba wake na maisha hayo yakawa kama jambo la kawaida.
Baba mzazi wa wasichana hao alihama na kwenda kuishi kwingine na baada ya muda, Mattingly akaondolewa kwenye nyumba hiyo na kupelekwa katika nyumba ya kutunza watoto huku Montgomery akisalia na mama yake nyumbani.
Ilichukua miaka, 34, kabla ya dada hao kuonana tena. Na hapo ilikuwa ni mahakamani ambapo mawakili wa serikali ya Marekani walikuwa wanajaribu kushawishi jopo la mahakimu kutoa hukumu ya kifo dhidi ya Montgomery.
"Dada mmoja aliondolewa ndani ya nyumba hiyo na kupelekwa katika nyumba iliyokuwa na upendo ambapo alituzwa na kupata muda wa kuponya moyo wake," amesema Mattingly. "Dada mwingine alisalia kwenye nyumba hiyo na hali ikaendelea kuwa mbaya zaidi. Na mwisho wake akavunjwa moyo kabisa."
Ikiwa hatua hiyo ya kunyogwa itatekelezwa, Montgomery atakuwa mmoja kati ya wafungwa 10 ambao watakuwa wamenyongwa chini ya utawala wa Trump chini ya kipindi cha mwaka mmoja.
Desemba mwisho, timu yake ya wanasheria iliwasilisha ombi la kukata rufaa kwa Donald Trump ambalo inasema baada ya unyanyasajia aliopitia - ambao wanasema ni mateso - ameathirika sana kiakili na badala ya kunyongwa anastahili kuonewa huruma.
Hata hivyo, katika mji mdogo wa Skidmore, Missouri, ambapo uhalifu huo ulitekelezwa, jamii hii haina huruma naye.
Wengi katika eneo hilo wanaamini kuwa dakika za mwisho za Bobbie Jo Stinnett zilikuwa za kuogofya na machungu mengi, na hukumu ya kifo ni sawa
Lisa Montgomery na Bobbie Jo Stinnett walijuana mtandaoni kwasababu wote walikuwa wanapenda mbwa.
Walikuwa wamewasiliana kwa wiki kadhaa na Montgomery alimuambia Stinnett kuwa pia yeye anatarajiwa kupata mtoto na wanawake hao wakawa wanashirikishana simulizi zao za ujauzito.
Desemba 2004, Montgomery alisafiri kutoka Kansas hadi nyumbani kwa Bobbie Jo Stinnett huko Missouri, umbali wa kilomita 281.5, kwa madai kwamba ameenda kununua mbwa, kulingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Sheria.
Lakini Stinnett hakuwa anamtarajia Montgomery ila Darlene Fischer kwasababu hivyo ndivyo Montgomery alivyojitambulisha kwake.
Hilo ndio jina ambalo Montgomery alilitumia wakati anawasiliana na Stinnett katika barua pepe tofauti akiuliza kuhusu namna ya kununua mbwa kutoka kwake.
Wakati Stinnett alipofungua mlango, Montgomery alimshambulia na kumnyonga kwa kamba Bi. Stinnett - aliyekuwa na ujauzito wa miezi nane - hadi mwathirika akapoteza fahamu na kumkata tumbo lake na kumtoa mtoto aliyekuwa amembeba tumboni.
Lakini wakati wa uchunguzi, wachunguzi walibaini mara moja kwamba hakukuwa na mtu aliyejulikana kama "Darlene Fischer", na wakaanza kumtafuta Montgomery siku iliyofuata kupitia barua pepe na anwani aliyokuwa anatumia.
Montgomery alipatikana akiwa amemshikilia mtoto mchanga aliyekuwa amezaliwa akidai amejifungua siku iliyotangulia.
Mara moja simulizi yake ikaanza kujikanganya na baada ya kubanwa akakiri alichotenda.
Mwaka 2007, jopo lilimpata Montgomery na hatia ya kuteka nyara kulikosababisha kifo kulingana na sheria za serikali nchini Marekani, na kwa kauli moja wakapitisha hukumu ya kifo dhidi ya mtuhumiwa.
Na tangu mwaka 2008, Montgomery amekuwa akizuiliwa gerezani huko Texas katika gereza la wanawake lenye mahitaji maalum ya kimatibabu na kisaikolojia ambapo amekuwa akipokea matibabu ya akili.
Na tangu hukumu yake ya kunyongwa ilipotangazwa amekuwa akifuatiliwa ili asijitoe uhai katika gereza lililotengwa.
Hata hivyo wakili wa Montgomery wanasema ubongo wa mteja wake uliathirika kwasababu ya kichapo alichopigwa akiwa mtoto hivyobasi hayuko sawa kiakili na kutokana na hilo mteja wake hastahili kuhukumiwa kifo.
Hukumu ya kifo ilipigwa marufuku katika ngazi ya majimbo na serikali kuu kulingana na uamuzi ulitolewa na mahakama ya juu zaidi mwaka 1972 iliofuta hukumu zote za kifo zilizokuwa zimetolewa kufikia wakati huo.
Aidha mwaka 1976 mahakama ya juu zaidi Marekani iliruhusu majimbo kurejesha tena hukumu ya kifo na mwaka 1988 serikali ikapitisha sheria iliyoruhusu tena utekelezaji wa adhabu hiyo kwa ngazi ya serikali kuu.
Kulingana na takwimu za Kituo cha taarifa za hukumu ya kifo, watu 78 walihukumiwa kifo katika ngazi ya serikali kuu kati ya mwaka 1988 na 2018 lakini ni watatu tu waliotekelezewa hukumu hiyo.
Hukumu ya Montgomery na Bernard zitakuwa za nane na tisa ambazo serikali kuu ya Marekani imetekeleza mwaka huu.
Kwanini hukumu hiyo inaanza kutekelezwa tena sasa?
Mwaka jana utawala wa Trump ulisema kuwa utaanza tena kutekeleza hukumu ya kifo baada ya kusitishwa kwa muda mrefu.
Taarifa iliyotolewa wakati huo, mkuu wa sheria alisema: "Chini ya utawala wa vyama vyote, wizara ya sheria imeamua kutekeleza tena hukumu ya kifo kwa wanaotekeleza uhalifu mbaya zaidi.
"Wizara ya sheria inaunga mkono sheria hiyo - na waathirika na familia zao wanatudai tuendelee kuitekeleza sheria iliowekwa na mfumo wetu wa haki.
Wafungwa wengine wanaotarajiwa kunyongwa
Cory Johnson alihukumiwa kwa mauaji ya watu saba, kuhusiana na kuhusika kwake na biashara ya dawa za kulevya huko Richmond, Virginia. Timu ya kisheria ya Johnson imesema kuwa ana shida ya kiakili, inayohusiana na unyanyasaji wa mwili na mihemko aliyopitia akiwa mtoto. kifo chake kimepangwa kutekelezwa tarehe 14 Januari.
Dustin John Higgs alihukumiwa baada ya kuhusika na vitendo vya utekaji nyara na mauaji ya wasichana watatu mnamo mwaka 1996 Washington, DC.
Higgs hakuua mwathiriwa wake yeyote, lakini alimwagiza mshtakiwa mwenzake Willis Haynes kufanya hivyo.
Haynes amesema katika nyaraka za mahakama kwamba Higgs hakumtishia, au kumlazimisha afyatue risasi.
Higgs amepangiwa kunyongwa tarehe 15 Januari.