Silaha za Urusi: fahamu silaha zinazomilikiwa na Uturuki ambazo ni hatari kwa usalama wa Marekani?

Onyesho la silaha aina S-400

Chanzo cha picha, Reuters

Marekani imeiwekea vikwazo Uturuki , mwanachama wa shirika la NATO , baada ya Uturuki kununua silaha zilizotengenezwa na Urusi.

Marekani inasema kwamba silaha hizo za Urusi aina ya S - 400 haziambatani na teknolojia ya NATO na kwamba ni hatari kwa muungano huo wa mataifa ya Ulaya.

Vikwazo vilivyotangazwa na wizara ya masuala ya kigeni vinalenga idara ya ununuzi wa silaha nchini Uturuki. Hatua hiyo ilishutumiwa na Urusi pamoja na maafisa wa Uturuki.

Tayari Marekani imeondoa ndege zake aina ya F-35 kutoka Uturuki ili kujibu hatua ya Uturuki kununua silaha za Urusi.

Je ni kwanini Marekani inapinga ununuzi huo?

"Marekani imekuwa wazi kwa Uturuki kwamba silaha aina ya S-400 inahatarisha usalama wa teknolojia ya Marekani mbali na usalama wa majeshi yake na kwamba Uturuki inapokea ufadhili mkubwa wa kijeshi kutoka kwa Urusi' , alisema waziri wa masula ya ulinzi nchini Marekani Mike Pompeo.

''Licha ya haya yote Uturuki imeamua kununua S-400 na kufanyia majaribio'', aliongezea. Vikwazo hivyo vnamlenga mkuu wa wizara ya ulinzi Ismail Demir na wafanyakazi wengine.

Vikwazo hivyo vinashirikisha marufuku ya Kuingia Marekani mbali na kupiga tanji mali yao nchini Marekani

Je Uturuki inasema nini kuhusu hatua hiyo?

File photo: Afisa wa Urusi akitembea mbele ya silaha aina ya S-400 tarehe 22 Agosti 2017

Chanzo cha picha, EPA

Serikali ya Ankara inahoji kwamba sababu ya kununua silaha hizo kutoka kwa Urusi ni baada ya Marekani kukataa kuiuzia silaha yake aina ya patriot.

Afisa huyo wa Uturuki alisema kwamba hatua ya Ugiriki ambaye pia ni mwanachama wa NATO - kumiliki silaha aina ya S-300 ijapokuwa haikutengenezwa moja ka moja na Urusi .

Wizara ya masuala ya kigeni imeitaka Marekani kubadili msimamo wake unaotaja kuwa usio wa haki .

Wizara hiyo pia imesema kwamba , Uturuki ilikuwa tayari kuzungumzia suala hilo kupitia njia za kidiplomasia kulingana na sheria za NATO.

Wizara hiyo ilionya vikwazo vya Marekani vitakuwa na athari mbaya dhidi ya uhusiano wa mataifa hayo mawili , huku ikiiwaacha Ututruki kulipiza kisasi wakati wake ukifika.

Waziri wa masuala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov pia aliishutumu hatua hiyo ya Marekani , akiitaja kuwa dhihirisho jingine la tabia ya kiburi ya Marekani ambayo ni kinyume na sheria za kimataifa

Je Uturuki ina umuhimu gani kwa Nato?

Jeshi la Uturuki

Chanzo cha picha, RT

Maelezo ya picha, Jeshi la Uturuki

Uturuki ni ya pili kwa idadi ya wanajeshi katika shirika la NATO lenye wanachama 30.

taifa hilo vilevile vilevile ni mojawapo ya washirika muhimu wa Marekani na lipo eneo muhimu la kimkakati. Uturuki inapakana na Syria, Iraq na Iran.

Pia ni mshirika muhimu katika mgogoro wa Syria , akitoa silaha kwa makundi ya upinzani .

Hatahivyo uhusiano wa Uturuki na washirika wa NATO umeendelea kudorora huku wanachama wa Muungano wa Ulaya wakimshutumu Erdogan kwa kutumia uongozi wa kiimla kufuatia kufeli kwa mapinduzi ya 2016. Uturuki huimarisha uwezo wake wa kijeshi kupitia silaha inazonunua kutoka UIngereza.

Nato ilibuniwa mwaka 1949 kwa lengo la kuikabili Urusi kujipanua hadi kuingia Ulaya huku shirika hilo likiwa na jeshi lenye uwezo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nato ilibuniwa mwaka 1949 kwa lengo la kuikabili Urusi kujipanua hadi kuingia Ulaya huku shirika hilo likiwa na jeshi lenye uwezo

Nato ilibuniwa mwaka 1949 kwa lengo la kuikabili Urusi kujipanua hadi kuingia Ulaya huku shirika hilo likiwa na jeshi lenye uwezo

Je silaha hiyo ya S-400 ilionunuliwa na Uturuki inafanya kazi vipi?

mchoro wa kombora aina ya S-400 na jinsi linavyofanya kazi

•Rada ya uchunguzi wa mbali huangalia vilipuzi na ndege, na hupeleka habari kwa vifaa vya ulinzi, ambavyo hutathmini malengo yanayowezekana

•Lengo linapogunduliwa linaamuru gari kurusha kombora

•Takwimu za kurusha kombora zinatumwa kwa gari la kurusha kombora ambalo hurusha kombora hilo mara moja angani

•Rada husaidia kuongoza kwa urahisi makombora kufikia malengo yake.