Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzozo wa Tigray Ethiopia: Jinsi askari alivyonusurika makabiliano ya risasi kwa saa 11
Mwanajeshi mmoja wa Ethiopia amesimulia BBC Afaan Oromo jinsi uvamizi wa nyakati za usiku unaohusishwa na wapiganaji wa utawala wa jimbo la Tigray ulivyofanywa dhidi ya kambi yao mwezi uliyopita.
Chama cha Tigray People's Liberation Front, TPLF- ambacho kilikuwa kikidhibiti serikali ya jimbo la kaskazini- kilisema kilitekeleza shambulio kama hatua ya kujilinda wakati ulimwengu ulikuwa ukiangazia uchaguzi wa Marekani, kwani kiliamini kuwa wanakaribia kushambuliwa na vikosi vya serikali.
Waziri Mkuu Abiy Ahmed alijibu mashambulio hayo kwa kuamuru oparesheni ya kijeshi ambayo kilele chake ilikuwa kupinduliwa kwa serikali ya jimbo hilo, kulazii wapiganaji wa TPLF kukimbilia milimani kupigana na kili walichotaja kuwa "wavamizi".
Imekuwa vigumu kupata taarifa sahihi kuhusu mzozo huo kwasababu mawasiliano yalikatizwa katika jimbo hilo.
Simulizi ya askari hao zinaashiria mgawanyiko wa kikabila katika jeshi la Ethiopia, huku baadhi ya wanajeshi wa jamii ya Tigraya wakilaumiwa kwa kwa kuunga mkono TPLF.
Sajini Bulcha:
Nilikuwa katika kambi moja karibu na mji wa Adigrat, uliopo karibu na mpaka wa Eritrea. Mwndo wa karibu usilu saa tano unusu Novemba 3, mimi na askari wengine tulipokea ujumbe mfupi kutoka kwa askari wenzetu waliko katika kambi ya mjini Agula - karibu kilomita 30 (18 miles) kaskazini mashariki mwa mji mkuu waTigray , Mekelle - ukisema: "Tumezingirwa. Ukiweza njoo utuokoe, njoo."
Muda mfupi baadae, kambi yetu pia ilizingirwa, na mamia ya vikosi maalum vya TPLF huku wanamgambo wakishika doria upande wa nje. Badhi ya wanajeshi wa Tigray - ambao walikuwa wameondoka kambini - walikuwa nao.
Tulimuendea kanali aliyekuwana ufunguo wa sehemu ya kuweka silaha nakumwambia afungue.
Alikataa akisema hana maelekezo ya kufanya hivyo. Alikuwa kutoka jamii ya Tigray, na hapo tukashuku alikuwa sehemu ya mpango wa kutushambulia.
Baadhi ya maaskari walibishana naye kumtaka afungue sehemu ya kuhifadhi silaha; wengine walijaribu kuvunja mlango. Hatimaye, tulifanikiwakupata silaha zetu. Kufikia wakati huo wapiganaji wa TPLF tayari walikuwa wameanza kupiga risasi.
Tilichukua nafasi zetu ndani na nje ya kambi, kwa kutumia miamba ya mawe, makontena na kuta za mijengo kama kinga. Ilikuwa kama saa saba usiku mapigano yalipoanza.
Kulikuwa na umbali wa mita 50 (164ft) kati yetu na wao.
Tuliwaua zaidi ya wapiganaji 100. Na wao waliua 32 kati yetu. Katika kitengo changu, mmoja alifariki na wengine tisa kujeruhiwa.
Wanajeshi wengi waliuawa na maafisa wa Tigray waliujiunga na wapiganaji hao.
Mapigano yalidumu wa kwa saa 11 hadi saa sita mchana wakati makomanda wetu wa ngazi ya juu walipotuamuru tukomeshe mapigano, turegeshe silaha zetu stoo na kwenda katika vyumba vyetu. Tilitii amri.
Muda mfupi baadaye wachungaji na wazee kutoka mji huo walikuja. Waliomba tujisalimishe. Karibu saa kumi jioni, tuliamrishwa kupeana silaha na vifaa vyetu vya kibinasi kwa vikosi vya TPLF. Kwa mara nyingine tena, tulitii amri.
Kisha tukaambiwa tukaambiwa tuchukuwe vitu vyetu na kuingia kwenye malori. Walizunguka pamoja nasi ndani ya magari. Tulilazimishwa kuwacha nyuma maiti.
'Nilitoa jina la uwongo'
Vikosi vya TPLF vilitusafirisha hadi kambi yao iliyopo mjini Abiy Addi, kilo mita 150 kusini magharibi mwa Adigrat.
Askari waliyojeruhiwa hawakupata huduma ya matibabu wakati huo wote.
Kila asubuhi walitaka tujitambulishe. Ilibidi tupeane majina yetu, kabila letu na jukumu letu katika jeshi. Nilikuwa nikitoa jina la uwongo.
Sehemu hiyo nadhani ilikuwa jangwani kwasababu kulikuwa na joto sana. Tulikuwa na maji kidogo ya kunywa. Kila asubuhi tulipewa chai bila sukari katika chupa za plastiki ambazo zimekatwa nusu. Chakula chetu cha mchana kilikuwa mkate.
Wanajeshi kutoka kambi yetu pia waliletwa Abiy Addi. Walituambia walishambuliwa. Baadhi yao walijisalimisha bila kupigana; wengine walijaribu kupigana kwa siku nne.
Kalashnikovs, nasilaha zingine za nguvu na hata maroketi ya masafa ya kadri zilitumika katik avita hivyo. Baadhi ya maaskari walikimbilia Eritrea.
'Sare kuchomwa'
Baada ya kama wiki mbili hivi, vikosi vya TPLF walitupatia chaguo tatu - tujiunge nao, tuishi Tigray kama raia ama turudi makwetu. Tuliamua kuchukua.
Lakini makomanda wetu wa ngazi ya juu, wataalamu wa radio, wanajeshi wanawake na wale ambao waliweza kutumia silaha walipewa chauo la kujiunga nao. Wote waliletwa Abiy Addi, kwa maelfu.
Tuliyosalia tualiambiwa tuvue sare zetu za kijeshi. Tulikata, na kusema tukotayari kufa - na kwamba maadili ya kazi haituruhusu kufanya hivyo; na kuongeza kuwa sare zetu zilikuwa fahari yetu.
Hatimaye tulikubaliana kwamba tutavua sare zetu na kuzichoma [ili zisitumiwe na watu wengine]. TPLF walirekodi kwenye video uchomaji wa sare hizo.
Walichukua vitu vyetu vya kibinafsi kama vile - pete , saa na pesa.
Maelezo zaidi kuhusu mzozo wa Tigray:
Ilikuwa karibu saa tisa alasiri siku ya Ijumaa tulipoambiwa sote tuingie kwenye malori. Kwa mara nyingine tena tuliwachukuwa wanajeshi wenzetu waliyojeruhiwa, lakini katika lori nililopanda halikuwa na yeyote aliyejeruhiwa.
Tulikuwa karibu wanajeshi 500 katika kila lori, kwa ujumla naweza kusema kulikuwa na karibu wanajeshi 9,000 katika malori yotekabla tuondoke Abiy Addi karibu saa tano usiku siku hiyo.
Tulisafiri kwa saa kadhaa katika nji aza ndani hadi vikosi maalum vya TPLF - vilivyokuwa vinatoa ulinzi kwa malori hayo - walipotuacha katika kingo za mto Tekeze katika mpaka wa kati ya Tigray na jimbo jirani la Amhara.
Malori yalifika hapo nyakati tofauti. Tulijigawanya katika makundi na kuvuka mto huo kwa kutumia maboti. Karibu saa sita zilipita kabla ya kundi langu kufika upande wa pili wa mto huo.
Baada ya hapo tulitembea kwa karibu saa 16 kufika mji wa Sekota katika jimbo la Amhara.
Sasa tuko katika kituo cha polisi mjini humo ambako tunalishwa na kutunzwa. Waliyojeruhiwa wanapewa matibabu hospitalini zaidi ya wiki tatu baada ya shambulio hilo.
Nasikia kwamba baadhi ya waliyojeruhiwa walifariki njiani, na miili yao kuachwa nyuma.