Kuponea kifo wiki moja Afghanistan

Razia aliponea kifo baada ya bomu la kutegwa garini kulipuka kando ya shule yake ya lugha ya ishara

Chanzo cha picha, Maroof Saeedi

Maelezo ya picha, Razia aliponea kifo baada ya bomu la kutegwa garini kulipuka kando ya shule yake ya lugha ya ishara

Ilimchukua Hussain Haidari saaa tatu kumpata ndugu ya mke wake, Latif Sarwari lakini kabla ya hapo aliona nyuso nyingi za watu waliofariki.

Latif alikuwa na miaka 20 na mwanafunzi wa gredi ya 12, ndoto yake ilikuwa kuwa daktari. Sawa na wanafunzi wenzake alikuwa amehamia Kabul miezi mitatu iliyopita kujiandaa kwa mtihani wa kujiunga na chuo kikuu.

Jumamosi mchana, Latif aliondoka kituo cha mafunzo cha Kawsar-e Danish kwa masomo yake ya kila siku ya masaa nne. Lakini alifariki muda mfupi baada ya shumbulio la bomu lililowaua watu 25 na kuacha barabara za mji huo na vumbi na mosho mkubwa

Hapakuwa na njia ya kufikia wazazi wa Latif kwa 's parents by phone, so Hussain prepared himself to travel in person to their remote village in Ghazni province, many miles to the south.

Tunaenda kupeleka mwili wa Latif kijijini kwao ambako aliondoka kwenda kufuatilia ndoto yake," alisema. "Tutakutana vipi na wazazi wake tukiwa mail wa mtoto wao wa kiume ?"

Siku ya Jumatatu jamaa wa familia waliwasilisha binafsi taarifa hiyo ya kifo.

Latif Sarwari
Maelezo ya picha, Ndoto ya Latif Sarwari, ilikuwa kuwa daktari

Wiki iliyopita kila siku kulishuhudiwa mauaji ya kikarili. Wazai wa Latif ni wawili kati ya watu wa familia kadhaa zilizoachwa na majonzi kufuatia ghasia hizo, licha ya kuendelea kwa mazungumzo ya amani.

BBC inatathmini wiki moja ya mauaji Afghanistan, kwa kuwaangazia waliofariki na wale walioponea.

Jumapili Oktoba 18

Razia, dada yake Marzia na ndugu yake Nayeb hawana uwezo wa kusikia. Walijiunga na shule ya lugha ya ishara katika mkoa wa Ghor kujifunza namna ya kuwasiliana kwa lugha ya ishara. Ndugu hao watatu walikuwa wameanza masomo yao siku ya Jumapili Oktoba 18 wakati shambulio la bomu lilifanywa dhidi ya jengo la shule waliyokuwa wakisomea

"Ilikuwa mara ya kwanza katika maisha yangu kusikia ," alisema Razia, mwenye umri wa miaka 16. "It was harrowing. Masikio yang hayakuwa na uwezo wa kusikia lakini siku hiyo nilisikia makelele kwenye sikio moja."

Karibu wa tu 16 waliuawa na wengine zaidi ya 150 kujeruhiwa. Mlipuko huo uliharibu majengo yaliyopakana na shule. Razia na ndugu zake pamoja na watoto wengine 19 walikuwa darasani.

"Kwa muda nilidhani nimekufa," alisema. "dada yangu alikuwa anapepesuka lakini nilidhani kaka yangu huenda pia amekufa. Kwa bahati nzuri wote waliponea."

Marzia, 18, pia alisikia mlipuko, alisema. "Ilikuwa mara ya kwanza Kwangju kusikia chochote. Nilisikia mlio mkubwa wa ajabu ulioshtua moyo wangu."

From left Marzia 18, Razia 16 and Nayeb 22

Chanzo cha picha, Maroof Saeedi

Maelezo ya picha, Kutoka kushoto Marzia, 18, Razia, 16, na Nayeb, 22, wakiwa nyumbani kwao mkoa wa Ghor

Wiki moja baada ya shambulio hilo, Marzia bado anapata tabu kulala hadi anaamka kwenda chumbani kwa mama yake mjani kujifariji. Anaogopa kutoka nyumbani.

Ndugu hao watatu ni miongoni mwa watu walioponea shambulio hilo. Waathiriwa wengi wa shambulio hilo la bomu walikuwa wafanyakazi ambao walikuwa na familia zinazowategemea.

Jumatatu Oktoba 19

Katika mji wa Khost, pikipiki iliyokuwa imebeba vilipuzi ililipuka karibu na eneo watu walikuwa wanashrehekea harusi, kuua watu wanne na kuwajeruhi watu wengine 10.

Katika mkoa wa Uruzgan, Maafisa wawili wa polisi waliuawa katika shambulio la Taliban na wengine wanne kujeruhiwa

Jumanne Oktoba 20

Maafisa watano waliuawa naw engine wawili kujeruhiwa baada ya bomu la kutegwa arching kulipuka kando ya barabara iliyokuwa inatumiwa na msafara wa magari wa maafisa hao katika mkoa wa Nimruz.

Mmoja wa watoto wa maafisa waliuawa aliambia vyombo vya habarikwamba atalipiza kisasi kifo cha baba yake kilichotekelezwa na Taliban atakapokuwa mkubwa . "Nasema hivi ili Ashraf Ghani afahumu machungu yangul," alisema, akielekeza tamko lake kwa rais.

"Baba yang alifariki kwa maslahi ya Ashraf Ghani ambaye anastahili kujua majonzi nyanayonikabili."Tuesday 20 October

Baadae siku hiyo, bomu lengine la kutegwa ardhini lilipuka Kabul katika mkoa wa Wardak, kuwaua watu 11 na kuharibu magari kadhaa ya abiria

Jumatano Oktoba 21

Mapema Jumatano asubuhi, wanamgambo wa Taliban walishambulia akambi ya usalama na kuwaua zaidi ya maafisa 30 wa kikosi maalum cha polisikatika mkoa wa Takhar kaskazini mashariki mwa nchi.

Mkuu wa polisi katika eneo hilo, kanali Abdullah Gard, alimpoteza mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka 25 katika shambulio hilo. "Hajafariki, mwanangu bado yuko hai," Kanali Gard aliambia BBC. "Hatutamsahau. Nafasi yake daima itasalia mioyoni mwetu."

Farid alikuwa amefuata nyayo za baba yake kuwa polisi.

Kanali Abdullah Gard na mwanawe wa kiume, Farid Ahmad Gard

Chanzo cha picha, Gard family

Maelezo ya picha, Kanali Abdullah Gard na mwanawe wa kiume, Farid Ahmad Gard

Baadae usiku wa Jumatano hiyo, ndege za vita za Afghanistan zilitumwa katika eneo la tukio kulipiza kisasi shambulio la Taliba. Wanajeshi walishambulia kutoka angani msikiti katika mkoa huo huo, ambako vijana wadogo walikuwa wanasoma katika chuo cha mafunzo ya kidini.

Wavulana 12 waliuawa na wengine zaidi ya 12 kujeruhiwa vibaya miongoni mwao mwalimu, Abdul Wali.

Ghasia nchini Afghanistan, hunuathiri kila mtu kwa njia moja au nyingine. Ghasia hizo zimewafanya raia wengi kutoroka makwao, na hata nchi yao, kutafuta hifadhi kama wakimbizi , kufanya kazi au kutoa huduma ya afya.

Siku hiyo hiyo, katika sehemu nyingine ya nchi - mkoa wa Nangarhar mashariki - raia wasiopungua 15 wakiwemo wanawake 11 waliuawa katika mkanyagano wakati watu wakipanga foleni ya kutoa maombi ya visa katika mji wa Jalalabad.

Wanawake wa Afghanista wakisubiri kutoa maombi yakupata hati visa ya Pakistan visa, Octoba 21, 2020.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wanawake wa Afghanista wakisubiri kutoa maombi yakupata hati visa ya Pakistan visa.

Mapema asubuhi hiyo, Niaz Mohammad aliye na umri wa miaka 60 alikuwa amerudi nyumbani kutoka kazini zamu ya usiku na kitu cha kwanza alichogundua ni kwamba mke wake hakuwepo, japo alikuwa ameondok anyumbani saa nane usiku kwenda kupiga foleni ya kutafuta visa katika ubalozi mdogo wPakistani.

Kwanza Niaz Mohammad alipokea simu kutoka kwa msamaria mwema aliye mfahamisha kuwa mke Bibi Ziwar, 55, amegongwa na gari.

Alienda hospitali kumtafuta alkini alielekezwa katika chumba cha kuhifadhi maiti, ambako alipata mwili wake. Alifariki katika mkanyagano wa watu.

Alhamisi Oktoba 22

Katika mji wa Badghis kaskazini magharibi mwa nchi , ndugu wawili waliuawa na bomu lililotegwa kando ya barabara. Maafisa katika mji wa karibu wa Herat walisema bomu hilo lilitegwa na wanamgambo katika barabara kuu inayotumiwa na wanajeshi,lakini waathirika ni vijana wawili mmoja wa alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu.

Katika mkoa wa kaskazini mwa Faryab, watu wasiopungua wanne waliuawa na wengine 14 kujeruhiwa kkatika kile maafisa wa eneo hilo walisema ni shambulio la roketi lililotekelezwa na Taliban.

Ijumaa Oktoba 23

Karibu wanajeshi 20 waliuawa katika shambulio la Taliban mkoani Nimruz kusini magharibi mwa Afghanistan. Maafisa katika eneo hilo walisema watu kadhaa waliojeruhiwa wakiwemo wanajeshi sita walishikwa mateka.

Picha katika mitandao ya kijamii zilonesha ' maiti ilivyotapakaa katika eneo hilo la jangwani, pamoja na picha za watu waliojeruhiwa wakati wa shambulio hilo.

Bomu lilivyoharibu taasisi ya Kawsar-e Danish tuition, ambako vijana walilengwa

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Bomu lilivyoharibu taasisi ya Kawsar-e Danish tuition, ambako vijana walilengwa

Hafizullah Maroof, Bashir Paiman na Zuhal Ahad wamechangia taarifa hii.