Alexei Navalny: Saa mbili zilizookoa maisha ya mkosoaji mkuu wa serikali ya rais Putin

Alexei Navalny

Chanzo cha picha, Reuters

Mpinzani maarufu nchini Urusi Alexei Navalny yupo katika hali mahututi katika hospitali moja mjini Berlin , akiwa mwathiriwa wa kile ambacho serikali ya Ujerumani inasema kwamba lilikuwa jaribio la sumu kwa jina Novichok.

Navalny alianza kuhisi vibaya alipokuwa ndani ya ndege ambayo ilimsafirisha kutoka Siberia hadi Moscow, na kuilazimu ndege hiyo kutua kwa dharura katika eneo la Omsk.

Idhaa ya Urusi ya BBC imeandaa ripoti ya jinsi wafanya kazi wa ndege na madaktari walitumia kila njia ili kuokoa maisha yake katika anga ya Siberia. Ifuatayo ni orodha ya yaliotokea katika kipindi cha saa mbili.

Mapema tarahe 20 mwezi Agosti , Alexei Navalny aliabiri ndege ya kampuni ya S7 kutoka Tomsk kuelekea Moscow

Kulingana na katibu wake wa habari , Kira Yarmysh, mapema asubuhi hali wala kunywa chochote isipokuwa kikombe cha chai alichonunua katika uwanja wa ndege wa Tomsk ,Bogashevo.

Alexei Navalny akitabasamu katika uwanja wa ndege wa Ilya Ageev

Chanzo cha picha, ILYA AGEEV

Maelezo ya picha, Alexei Navalny akitabasamu katika uwanja wa ndege wa Ilya Ageev

Abiria mwengine wa ndege hiyo , Ilya Ageev, anamuona Navalny akinywa chai saa moja kabla ya ndege kuondoka

Mkosoaji huyo mkubwa wa Kremlin baadaye anafanya mzaha na abiria aliyemtambua.

Saa kumi na dakika moja

Navalny anaanza kuugua katika nusu ya kwanza ya safari hiyo ya ndege.

Wakati wahudumu wa ndege wanapogawanya maji miongoni mwa abiria , anakataa. Baadaye anaamka kwenda msalani.

Saa kumi na nusu

Abiria mmoja anajaribu kwenda msalani , lakini Navalny amekuwa ndani kwa zaidi ya dakika 20. Kunakuwa na foleni ndefu ya kutaka kuingia chooni.

Saa kumi na dakika 50

Kufikia sasa wafanyakazi wanne wa ndege tayari wamegundua kwamba mmoja wa abiria hajisikii vyema

Saa kumi na moja

Dakika chache baadaye , muhudumu mmoja wa ndege anauliza kwa kutumia kipaza sauti iwapo kuna madaktari ndani ya ndege hiyo.

Abiria wengine wanagundua kwamba hali sio nzuri. Wafanyakazi wa ndege wanamwelezea rubani wa ndege na kujaribu kumfanyia Navalny huduma ya kwanza.

Msaidizi wake, Ilya Pakhomov, anatembea ndani ya ndege hiyo akiomba usaidizi wa kimatibabu. Mwanamke ambaye hajatambulishwa anajitambulisha kuwa muuguzi.

Kulingana na ndege ya kampuni ya S7 , mwanamke huyo na wengine katika kipindi cha saa moja akishirikiana na wafanyakazi wa ndege wanamuhudumia Navalny hadi pale rubani wa ndege atakapotua kwa dharura.

''Hakuzungumza alipiga kelele''

Wakili Sergey Nezhenets alikuwa ameketi katika viti vya mwisho vya ndege karibu na mahali ambapo Navalny alikuwa akitibiwa.

Alilazimika kuelekea Moscow kabla ya kurudi na kuelekea Krasnodar, kusini mwa Urusi.

''Nilianza kutaka kujua ni nini kilichokuwa kikiendelea wakati mfanyakazi mmoja wa ndege alipowauliza maafisa wa afya kujitambulisha'', Nezhenets alisema.

Maafisa wa afya walivyojitokeza ili kuokoa maisha ya Navalny

Chanzo cha picha, ILYA AGEEV

Maelezo ya picha, Maafisa wa afya walivyojitokeza ili kuokoa maisha ya Navalny

Kulingana na Nezhenets, ni wakati huo ambapo muuguzi mmoja alijitambulisha na kutoa usaidizi wa kimatibabu.

''Sijui alifanya nini, sikuona. Lakini niliwasikia wakisema mara kwa mara Alexei kunywa , kunywa Alexei vuta pumzi'', alisema wakili.

''Wakati alipopumua , wengine wetu tulihisi vyema , kwasababu hiyo ilimaanisha kwamba alikuwa hai. Wakati huo sikujua kwamba ni Navalny'', alisema. Wasaidizi wawili wa Navalny walikuwa naye.

Mmoja wao alikuwa katibu wake wa habari , Kira Yarmysh. Nilikuwa na wasiwasi, Nezhenets alisema. Daktari alimuuliza ni nini kilichomfanya hivyo, na Kira akasema , sijui, nadhani alipewa sumu.

Saa kumi na moja na dakika ishirini.

Wafanyakazi wa ndege walipata ruhusa ya kutua kwa dharurar katika eneo la Omsk. Lakini ndege hiyo ililazimika kutua baada ya dakika 30 bada ya hatua hiyo kuelezewa abiria.

''Wafanyakazi wa ndege waliendelea kutazama madirisha na kulalama kwamba kulikuwa na mawingu mengi, na ilikuwa inachukua muda mrefu kutua ilihali hali ya Navalny ilikuwa mbaya'', alisema Nezhenets. Wakili anasikia sauti za kumlazimu Navalny kunywa kitu.

Picha ya Navalny akihamishwa katika ambyulansi

Chanzo cha picha, IlYA AGEEV

Maelezo ya picha, Picha ya Navalny akihamishwa katika ambyulansi

''Iwapo wakishuku kwamba alipatiwa sumu , wafanyakazi wa ndege wangejaribu , anasema mtaalamu wa wagonjwa waliopo katika chumba mahututi Mikhail Fremderman.

lakini hilo lisingemsaidia kutokana na sumu ya Organophosphate ambayo ndio kile ambacho Ujerumani inakizungumzia sasa.

Na iwapo chakula ama kinywaji cha Navalny kiliwekwa sumu , kutapika kungesababisha hatari kwa wale ambao walikuwa wakimsaidia kimatibabu mbali na wale ambao wangesafisha ndege hiyo baadaye.

Saa kumi na mbili na dakika moja

Ndege inatua mjini Omsk asubuhi.

Saa kumi na mbili na dakika tatu

wafanyakazi wa afya katika kampuni hiyo ya ndege wanaabiri ndege hiyo dakika mbili tu baada ya kutua

''Lakini mara tu walipomchunguza Navalny , madaktari walisema hiki sio kisa chetu, anahitaji kuwekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi'', anakumbuka Nezhenets.

Wakili huyu baadaye anasikia mmoja wa maafisa wa afya wakiitisha ambyulansi. Wanamwambia kwenda moja kwa moja katika eneo la ndege kutua , akisema kwamba mgonjwa huyo yuko katika hali mbaya.

Muda mfupi , anasikia Daktari mmoja akielezea kuhusu rangi ya ndege hiyo katika simu na kumwambia dereva kuegesha gari lake karibu na ngazi.'

'Tulisubiri dakika nyengine 10 kwa ambyulansi hiyo kuwasili' , anasema.

Wakati huo, madaktari walichunguza shinikizo la damu la Navalny na kumwekea maji katika mishipa yake ya damu.

Abylansi katika uwanja wa ndege

Chanzo cha picha, SIBIR.REALII

Dkt. Sidorus anasema kwamba hakumtibu Alexei Navalny yeye mwenyewe, lakini wenzake walifanya kila kitu walichoweza kuokoa maisha yake .

''Ilikuwa vigumu kuelewa kile kilichokuwa kikifanyika kwasababu sikuweza kuzungumza'', anasema.

Walifanya kila uwezo wao kukoa maisha ya mwanamume huyo na kuhakikisha kwamba alisafirishwa katika hospitali nzuri.

Abiria tuliozungumza nao wanaamini kwamba madaktari walitumia kati ya dakika 15 hadi 20 kumchunguza Navalny akiwa ndani ya ndege hiyo

Saa kumi na mbili na dakika 37

Navalny anatolewa katika ndege hiyo na kupelekwa katika ambyulansi ambayo inampeleka moja kwa moja katika kitengo cha dharura cha hopsitali ya Omsk.

Ndege hiyo inawekwa mafuta na inaendelea na safari yake ya nusu saa.

Wafanyakazi wa uwanja wa ndege wakiabiri ndege hiyo

Chanzo cha picha, DJPAVLIN

"Tulipotua katika uwanja wa ndege wa Domodedovo mjini Moscow maafisa kadhaa wa polisi na wanaume waliokuwa wamevalia nguo za raia waliingia katika ndege hiyo ," Nezhenets aliambia BBC.

"Waliwauliza abiria waliokuwa wakiabiri ndege hiyo karibu na kiti cha Alexei kusalia , huku wengine wakitakiwa kuondoka .. Alexei alikuwa ameketi katikati ya ndege hiyo'', alisema.

Wakili huyo alishangazwa na jinsi ambavyo maafisa wa polisi waliingia katika ndege hiyo .

''Wakati huo kesi hiyo haikuonekana kuwa ya uhalifu . Lakini maafisa wa usalama walikuwa wameingia'', alisema.

''Alipewa sumu ya Novichok''

Kwa siku mbili , hospitali ya Omsk ilimweka katika idara ya watu waliopewa sumu . Hawakukubali apelekwe Ujerumani kutokana na hali yake mbaya.

Hatahivyo tarehe 22 Agosti , alisafirishwa hadi mjini Berlin. Siku mbili baadaye , madaktari wa Ujerumani walisema kwamba vipimo vilionesha kwamba amepewa sumu.

Navalny anatibiwa katika hospitali moja mjini Berlin Ujerumani

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Navalny anatibiwa katika hospitali moja mjini Berlin Ujerumani

Madaktari wa Omsk akiwemo mwanafizikia mkuu kutoka katika kitengo cha dharura na mtaalamu mkuu wa sumu , walisisitiza kwamba hakuna kitu chochote cha sumu kilichopatikana katika mwili wa Navalny wakati alipokuwa chini ya usimamizi wao.

Idhaa ya BBC Urusi iliwauliza maafisa afya wa Omsk kutoa tamko lao mbali na kutoa maelezo ya Navalny katika hospitali hiyo lakini hawajatoa tamko lolote