'Ni wasichana, sio kinamama': Nchi ambayo wasichana sita huavya mimba kila siku

Msichana mja mzito

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hospitali za umma Brazil huwafanyia huduma ya uavyaji mimba wasicha karibu sita kila siku walio na miaka kati ya 10-14

Hatua ya kumtoa mimba mtoto wa miaka 10 wiki hii, imezua mjadala mkali Brazil, ambapo suala la uavyaji mimba linakumbwa na mgawanyiko mkubwa.

Lakini Melania Amorim, daktari ambaye amekuwa akiwasaidia waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia kwa miaka 30, ameiambia BBC kuwa visa kama hivyo vinaendelea kuongezeka na kuelezea kwanini kutoa mimba ndio nji asalama kwa wasichana hao kuliko kujifungua

Melania Amorim alikuwa anaanza taaluma yake daktari bingwa wa wanawake aliposhuhudia kisa cha kwanza cha mimba za utotoni nchini Brazil.

Ilikuwa kisa cha msichana aliye na miaka 13 ambaye alikuwa amebakwa wakati mama yake alipokuwa akifanya kazi za ndani.

Alikuwa amepelekwa hospitali katika eneo la kaskazini -magharibi mwa Brazil ili akatolewe mimba - lakini hakuna daktari yeyote aliyekuwa zamu ambaye alitaka kumfanyia huduma hiyo.

"Mamake msichana huyo alikuwa mfanyakazi wa ndani na alikuwa amemuacha nje kuota jua. Alipata ujauzito baada ya kushambuliwa," Dkt Amorim aliambia BBC.

"Hospitalini, hakuna mtu aliyetaka kumhudumia, kila mmoja alisema anapinga utoaji mimba."

"Nilikuwa mdogo lakini nilikubali kumhudumia. Niliamini kuwa kufanya hivyo ni kuokoa maisha ya mtoto na kwamba ilikuwa haki yake kama mhasiriwa wa ubakaji," daktari alisema, kwa sauti ya masikitiko.

Dkt Amorim amefanya kazi ya kuwahudumia watoto na kushughulikia masuala ya mimba za utotoni kwa zaidi ya miaka 30, hususan wasichana waliopata ujauzito kutokana na ubakaji.

Visa vinne vya ubakaji kwa siku

Brazil imetikiswa na kisa cha kutatanisha cha uavyaji mimba dhidi ya msichana wa miaka 10 ambaye alibakwa na mjomba wake mara kadhaa. Kisa hicho kilifanyika katika mji wa Sao Mateus, katika jimbo la kusini la Espirito Santo.

Dkt Melania Amorim akihojiwa na BBC Brazil kupitia Zoom

Chanzo cha picha, Reprodução

Maelezo ya picha, Dkt Amorim amefanya kazi ya kuwahudumia watoto na kushughulikia masuala ya mimba za utotoni kwa zaidi ya miaka 30

Kisa hicho kiligongwa vichwa vya habari baada ya taarifa za kibinafsi za mtoto aliyepelekwa jimbo jirani kutolewa mimba kuvujishwa mitandaoni na wanaharakati wanaopinga suala la uaviaji mimba.

Pia kumekuwa na jaribio la kupinga utoaji mimba kotini kutoka kwa waandamanaji wa makundi ya kidini - baadhi ya wanaharakati walijaribu kuvamia hospitali alikolazwa msichana huyo.

Sheria ya Brazili inaruhusu utoaji mimba ikiwa mimba hiyo imetokana na ubakaji ama maisha ya mwanamke yako hatarini.

Mahakama ilikuwa imetoa idhinii mtoto huyo wa miaka 10, ambaye alidhulumiwa na mjomba wake tangu akiwa na miaka sita kutoa mimba.

Dkt Amorim anasema kuwa hali ya kimatibabu kama hiyo imekuwa ikiendelea kila siku na huenda isikomeshwe hivi karibuni akiangazia visa alivyoshuhudia yeye binafsi katika kazi yake.

Mfumo wa afya ya umma nchini Brazil, unarekodi karibu visa sita vya uavyaji mimba kila siku unaohusisha wasichana wa umri wa kati ya miaka 10 na 14.

Takwimu za unyanyasaji wa kijinsia ni za kushangaza: kwa mujibu wa data iliyokusanywa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Public Safety Forum ambalo linajishughulisha usalama wa umma, wasichana wanne walio na umri wa chini ya miaka 13 wanabakwa kila baada ya saa moja kila siku.

Athari za mimba kwa wasichana wadogo

"Wanafika hospitali, wakiwa wamechanganyikiwa wasijue la kufanya huku wakiwa bado wanakabiliwa na hofu ya mazingira waliyopatia mimba hizo," daktari anaelezea.

A pregnant lady moves around her accommodation in Brazil

Chanzo cha picha, Marcello Casal Jr./ABr

Maelezo ya picha, "Mimba hukabiliwa na hatari wakati wowote," Amorim anasema. "Lakini hitari zaidi kwa wasichana wadogo."

Dkr Amorim anasema kuwa "nashangazwa, kusikitishwa na kuchukizwa" na jaribio la kumzuia mtoto wa miaka 10 kutoa mimba.

Mimba za umri huo zinasadikiwa kuwa hatari mno. Utafiti uliofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto, Unicef, umebaini kuwa wasichana wanaojifungua kabla ya kufikisha miaka 15 wanakabiliwa na hatari ya kufariki kutokana na matatizo ya uzazi ikilinganishwa na wanawake wanaojifungua wakiwa na miaka 20 au zaidi.

Utafiti uliochapishwa katika jarida la Marekani la afya ya uzazi uliyoangazia mimba za utototoni miongoni mwa wasichana wa Amerika Kusini, Uulibaini kuwa wasichana walio na miaka 15 ama chini ya miaka hiyo huenda wakapatikana na tatizo la ukosefu wa damu kutokana na athari za kujifungua wakiwa na umri mdogo

Hatari kwa mtoto

Pia kuna hatari ya mtoto kufariki.

Melania Amorim anasema kuwa mimba za utotoni miongoni mwa wasichana wenye umri wa miaka 10 hadi 15 hukabiliwa na hatari ya mama kupatikana na shikizo la damu au hata kupoteza fahamu.

"Watoto waliozaliwa na wasichana hawa huenda wakapatikana na changamoto ya kuwa na uzani mdogo. Hali ambayo itapunguza kasi ya kukuwa(kutokana na umbo la miili ya wasichana hao) na, hivyo basi kuwafanya wengine kuzaliwa kabla ya muda wao wa kuzaliwa kufika," anasema daktari.

Mimba kwa wasichana waliona umri wa miaka 13 ama chini ya hapo ni hatari zaidi kwasababu miili yao badoo inaendelea kukuwa.

"Viungo vya ndani vya miili yao haijamalizaka kuumbika. Itakuwa vigumu kwao kujifungua kwa njia ya kawaida," anaelezea.

"Kutoa mimba ndio njiasalama zaidi kuliko kujifungua kwa wasichana hawa"

Dkt Amorim, ambaye pia ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Campina Grande, anasema kuwaruhusu wasichana hawa kutoa mimba ni bora na salama kwao kuliko kujifungua.

"Kuzaa ni hatari kwa mwanamke yeyote, wakati wowote. Kwa msichana mdogo, ni hatari zaidi," anasema

Msichana mjamzito

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mimba kwa wasichana walio na miaka 13 ama chini ya hapo ni hatari sana kwasababu miili yao bado inakuwa

Melania Amorim pia anafanya kazi na waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia.

Kama daktari bingwa wa wanawake, amekuwa akiwasaidia waathiriwa wa ubakaji wa umri wa kati ya miezi sita hadi miaka 92.

"Hakuna umri ambao unamkinga mtu dhidi ya ubakaji. Sisi wanawake hatupo salama katika umri wowote," alilalamika.

"Mwanamke akiwa mdogo sana hawezi kupata. Lakini visa vya unyanyasajai vinaanza katika umri huo na kuendelea hadi msichana anapobalehe, na matokeo yake ni kushika mimba ," Dkt Amorim anaongeza kusema.

"Wasichana wengi hawajui wana haki kisheria kuavya mimba"

Sio mimba zote za utoto zinaishia kutolewa. Madaktari wanasema waathiriwa wachanga wa ubakaji wanafika hospitali muda mfupi kabla ya kujifungua.

"Wasichana wengi hawana habari kwamba wanaruhusiwa kisheria kuavya mimba ."

Amorim anakumbuka kushuhudia kisa cha kwanza cha kifo kilichotokana na changamoto ya uzazi akiwa na miaka 17 bado akiwa mwanafunzi.

"Ilikuwa msichana mdogo wa miaka 13 ambaye alifariki akijaribu kuavya mimba. Na cha kusikitisha ni kwamba alikuwa na haki ya kisheria kufanya hivyo kwa njia salama katika kituo cha afya," anasema.