Nawal El Moutawakel, mwanamke aliyebadili Ulimwengu wa Kiarabu kwa mkimbio mmoja

Kama wewe ni mwanamke wa Morocco na ndio umetimiza umri wa miaka 36, huenda ulikua karibu kupewa jina Nawal. Hii ni kwasababu ushindi wa Nawal El Moutawakel tarehe 8 Agosti 1984 katika michezo ya Olyimpiki mjini Los Angeles ulikuwa na maana kubwa sana kwa Mfalme wa Morocco Hassan II kiasi kwamba alitangaza kuwa watoto wote wa kike waliozaliwa siku hiyo waitwe jina lake. Hii ni hadithi yake.

Kila ushini ni wa kipekee. Lakini baadhi huwa wanajihusisha nao nao kuliko wengine, labda kwasababu kuna ushindi wa mambo mengi katika ushindi mmoja.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa ushindi wa Nawal El Moutawakel katika michezo ya Olyimpiki ya 1984 Los Angeles.

Hakuwa tu mwanamke wa kwanza kushinda mbio za mita 400- alikua ndiye mwanamke wa kwanza kuanza kukimbia mbio hizo katika mchezo ule-lakini pia alikuwa ni Mmorocco wa kwanza kuwahi kushinda medali ya dhahabu katika Olyimpiki, alikuwa ni mwanamke pekee wa Morocco katika aliyeshiriki katika michezo hiyo.

Labda hili lilimtia moyo mkimbiaji mwenzake wa kiume kutoka taifa Saïd Aouita ambaye siku chache baadae alifanikiwa kushinda mbiuo za mita 5000 kwa wanaume.

Lakini kile ambacho dunia inapaswa kukumbuka ni kwamba Nawal El Moutawakel alikua ni mwanamke wa kwanza Mwarabu Mwafrika kuwa mshindi wa mbio za Olyimpiki.

Usiku kabla ya Fainali, El Moutawakel alikuwa na ndoto mbaya za mashindano ya aina ile-kama vile kushindwa mbio zote.

"Niliogopa sana," El Moutawakel anakumbuka.

"Nilikua mwanariadha wa jinsia ya kike peke yangu katika ujumbe wote wa Morocco, na kila mtu alinitegemea.

"Usiku sikulala, nikifikiria juu yam bio, nikiziwaza katika ndoto zangu, katika ndoto zangu mbaya, kwasababu nilikua ninatoka jasho , na sikuweza kwenda kitandani, na nilikua ninajiangalia nikikimbia katika mwendo wa slow motion."

Ingawa hakuonekana kama mmoja wa watu waliopendwa, Wamorocco walijifunza kuamini uwezo wake wa kibinafsi na alinuwia kupata mafanikio fulani katika mbio hizo.

"Nilhisi inaweza katika fainali, kama vile miongoni mwa wanane wa kwanza, lakini wakufunzi wangu walikua wakinielezea jinsi ninavyopaswa kujiamini mwenyewe na kuwa na moyo wa kutokata tamaakwasababu waliamini kuwa ninaweza kushinda.

"Kanla ya fainali, tulikaa chini na makocha wangu na tulikua tunapitia kanda za video, si tu kwa ajili ya kutazama mbio zangu bali kuwatazama wakimbiaji wengine kama Judi Brown, PT Usha fkutoka India, Cojocaru kutoka Romania, na tulikua tunaangalia uwezo wao na udhaifu wao na juu ya pia uwezo na mapungufu yangu.

"Walisema nitahitajika kuongeza nguvu za kukimbia kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mbio, kwasababu ninaweza kushinda."

Akiwa mwenye imani kuwa anaweza kushinda kabla ya kukimbia ilikua ni muhimu kwa mafanikio ya El Moutawakel.

Alikua tayari kiakili, na alikua sasa anaangalia jambo moja:"Lazima uondoke katika nchi hii na kitu fulani."

"Hii ni mara yako ya kwanza, huu ni mji , huu ndio muda, huwezi kukosa ," yalikua ni baadhi ya mambo aliyokua akijiambia akilini .

Pamoja na Mmarekani -rafiki yake, Judi Brown-katika mbio, uwanja uliofurika umati wa mashabiki havingeweza kuzuwia nia ya Mmorocco mwenye umri wa miaka 22 kufikia lengo lake la ushindi. Hali uwanjani ilikuwa ya kuogofya na vyombo vya habari vilikua na ari kubwa ya kufuatilia mbio hizo.

Kuanza kimakosa kwa mbio awali - ambako El Moutawakel alidhani alisasababisha - kulimuongezea wasiwasi .

Wakati alipobaini kuwa hakua ni yeye aliyekwenda mapema, akatulia na , walipoanza mara ya pili "alikimbia kama risasi."

"Mzunguko wa kwanza, wapili , watatu nikaruka kwa mguu wa kushoto, na halafu nikaendelea nikibadilisha miguu kulia na kushoto hadi kwneye mstari wa kumalizia ," aliongeza. Alikua katika kiwango chake cha kipekee - akiwaacha wenzake mbali sana kiasi kwamba alishangaa na kujiuliza kama alianza vibaya kwa kukimbia kabla ya wenzake tena lakini hakusikia akiitwa arudi.

"Nilifikiria - 'wengine wako wapi, kwani imekuaje ni mimi peke yangu nayekimbia?'"

"Lakini ukweli ni kwamba nilikua nimewaacha sana. Na nikaanza kuangalia, kwenye mstari wa kumalizia mbio-Nikageuza kichwa , kushoto na kulia, kuhakikisha sikua ni mimi peke yangu ninayekimbia kuanzia mwanzo hadi mwisho . Lakini walikua pale, washindani wangu wote wengine ."

Kweli, walikuwepo pale-lakini nyuma yangu sana.

Pamoja na hata kupunguza kasi alipokua akikaribia kumalizia mbio, Nawal El Moutawakel aliweka rekodi binafsi kwa zaidi ya kutumia muda wa sekunde 54.61 , huku h Judi Brown akichukua medali ya shaba akitumia sekunde 55.20.

Ulikua ni ushindi mzuri kutoka kwa Nawal El Moutawakel, licha ya kwamba alikua na huzuni kwamba baba yake na mtu ambaye alikua shabiki wake mkubwa aliyemuunga mkono hakuwepo pale kushuhudia mafafanikio yake.

"Ilikua ni furaha wakati nilipovuka mstari wa kumaliza mbio, lakini pia huzuni kwasababu baba yangu, ambaye alikuwa shabiki wangu namba moja , alikuwa amefariki miezi kadhaa kabala na hakuweza kushuhudia ushindi wangu ", alisema.

Anatoka katika familia inayopenda michezo-baba yake alikua ni mchezaji wa zamani wa judoka na mama yake alikuwa mchezaji wa mpira wa wavu (volleyball ). Kila mara El Moutawakel alikuwa akishauriwa na wazazi wake kufuata ndoto zake za kuwa mwanariadha wa ngazi ya juu . Hivyo ndivyo alivyo tumwa Marekani kuendelea na kazi hiyo na wakati huo huo akiendelea na masomo.

Lakini je waliwahi kufikiria kuwa msichana wao mdogo atawahi kupata mafanikio kupitia mchezo?

"Kwan chi yangu kilikuwa ni kitu kikubwa kwa kweli ambacho hakuna mtu alitarajia, Mmorocco kijana, msichana ambaye alijaribu kupata nafasi miongoni mwa wanariadha hawa bora na sio kupata nafasi tu bali kushinda dhahabu na kuileta nyumbani… kilikua ni kitu ambacho kitaendelea kubaki akilini mwa kila Mmorocco" alisema El Moutawakel.

"Ulikuwa ni wakati wa kihistoria ambao utabaki daima katika moyo yangu ."

Kutoka pale, mlango mkubwa , mpana ukafunguka kwa wasichana wadogo, sio tu nchini Morocco bali katika mataifa mengine ambayo awali yalikuwa na vikwazo ya Kiarabu na kiisalamu.

"Kuanzia wakati ule, tumeshuhudia Wamoroco wanawake wengi wakiwa wasjhindi wa dunia -na vivyo hivyo katika mataifa ya Algeria, Tunisia, Misri, na Bahrain," alisema.

"Nchi ambazo wanawake wake hawajawahi kushiriki michezo ya Olyimpiki . Baadaye,walikuwa hawashiriki kuhudhuria, bali walishiriki kushinda ."