Uchaguzi Marekani 2020: Kanye West azindua rasmi kampeni yake ya urais Marekani

Kanye West amezindua rasmi kampeni yake kwa ajili ya uchaguzi wa urais Marekani 2020, kwa kufanya mkutano wa kampeni huko Charleston, South Carolina ambao haukukubalika.

West, 43, anawania urais kama mgombea kupitia chama chake cha "Birthday Party".

Katika mkutano huo, mwanamuziki huyo wa mtindo wa kufoka foka alionekana kufanya maamuzi ya kusthukiza ya kisera na kuonekana kuzungumzia masuala kadhaa ikiwemo uavyaji mimba na mwanahakati anayependelea uavyaji mimba Harriet Tubman.

Mashabiki wanahoji ikiwa kujiingiza kwenye kinyang'anyiro cha kuingia Ikulu ya White House ni njia ya kujitafutia umaarufu.

Katika mkutano wa Charleston hakuonesha kuwa kujitoa kwake katika kampeni ni kwa kumaanisha. Lakini katika ujumbe ambao sasa hivi umeondolewa katika akaunti ya Twitter ya West alioandika Jumamosi, ulionesha nyimbo za albamu anayotaka kutoa, jambo ambalo limeongeza maswali.

Kanye West alisema nini kwenye mkutano?

West alijitokeza sehemu ya nyuma ya kichwa chake kikiwa kimenyolewa '2020' huku akiwa amevalia fulana ya kumkinga kiusalama na kuhutubia hadhara bila ya kipaza sauti.

Hakukuwa na kipaza sauti cha watu waliokuwepo pia, na hilo likafanya West kila wakati awe anaomba watu kunyamaza ili aweze kusikia swali analoulizwa.

Wakati mmoja alianza kulia alipokuwa anazungumzia suala la uavyaji mimba, akisema wazazi wake karibu tu watoe mimba yake: "Leo hii hakungekuwa na Kanye West, kwasababu baba yangu alikuwa na shughuli nyingi."

Aliongeza: "Kidogo tu nimuue binti yangu... hata kama mke wangu [Kim Kardashian West] angenipa talaka baada ya hotuba hii, alimleta North hapa duniani, hata kama sikuwa tayari."

Hata hivyo aliongeza kwamba anaamini kuwa uavyaji wa mimba unastahili kuendelea kukubalika kisheria lakini pia kina mama wanaopitia wakati mgumu wapate usaidizi wa kifedha - na kupendekeza kwamba kila mwenye mtoto atapata madola ya mamilioni.

"Kile kinachoweza kutuweka huru ni kuheshimu sheria tulizowekewa na waanzilishi wa taifa hili," alisema. "uavyaji mimba unastahili kuruhusiwa kisheria kwasababu unajua nini? Sheria hiyo sio ya Mungu, kwa hiyo uhalali wake uko wapi?"

Wakati mwingine alionekana kutoa hotuba ambayo haikutarajiwa ya karne ya 19 kuhusu mwanahakati aliyependelea uavyaji mimba Harriet Tubman.

Tubman alizaliwa katika utumwa, lakini alifanikiwa kutoroka mashamba ya Maryland 1849 akiwa na umri wa miaka 27. Kisha alirejea Kusini kunusuru watumwa wengine na kuhatarisha maisha yake mwenyewe kuongoza wengine katika upatikanaji wa uhuru.

West pia alibubujikwa na machozi alipozungumza kuhusu marehemu mama yake aliyekufa 2007 baada ya upasuaji wa urembo kwenda mrama.

Watu wamechukuliaje mkutano wake?

Hotuba hiyo imepokelewa kwa hasira na baadhi ya watu - hasa kwa maoni yake kuhusu Tubman - lakini pia kumeibuka wasiwasi kuhusu suala la ustawi wa jamii kwa mtazamo wa West.

Profesa Jason Nichols, mhariri mwandamizi wa masomo ya Wamarekani Waafrika chuo kikuu cha Maryland, ameiambia BBC anahofia kujitokeza kwa West kulionekana kama amechanganyikiwa - ingawa anakubali kwamba yeye sio mwanasaikolojia

"Amekubali kwamba kipindi cha nyuma aliwahi kuwa na matatizo ya akili na kwamba wakati mwingine hapati matibabu.

"Alionekana akiwa muwazi zaidi kuliko nyakati nyingine... anapokuwa kwenye mikutano kama hiyo, lakini naamini sasa hivi hayuko sawa. Amezungumza baadhi ya mambo mabaya."

Profesa Nichols ameongeza kuwa amekatishwa tamaa kwasababu alikuwa na matumaini kwamba West atafanikiwa kuwatoa kijasho wagombea wengine ikiwa angekuwa na timu nzuri ya ushauri.

"Nilikuwa natamani sana kuona kitakachotokea, lakini baada ya leo, matumanini yamebadilika na kuwa wasiwasi."

Je Kanye West atakuwa debeni?

West, ambaye alitangaza kwamba atagombea urais Julai 4, tayari siku ya ukomo ya kumwezesha kuingia debeni katika majimbo kadhaa imepita.

Anahitajika kukusanya saini za kutosha ili kuingia kwenye kinyang'anyiro.

Juma lililopita, ndio alifanikiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha urais Oklahoma jimbo la kwanza ambapo ametimiza masharti kabla ya siku ya ukomo.

Ili aweze kuingia kwenye kinyang'anyiro cha urais South Carolina anahitajika kukusanya sahihi 10,000 kufikia mchana saa za eneo hilo siku ya Jumatatu.