Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Majasusi wa Urusi waulenga utafiti wa chanjo ya corona Marekani na Ulaya - wanataka nini?
Majasusi wa Urusi wanalenga makampuni yanayojaribu kutengeneza dawa ya chanjo ya virusi vya corona nchini Uingereza, Marekani na Canada, wataalamu wa masuala ya usalama wametahadharisha.
Kituo cha kitaifa kinachoshughulika na masuala ya usalama wa mitandao ya kompyuta kimesema majasusi wanafanya kazi hiyo kama ''sehemu ya watumishi wa idara ya usalama,''
Kituo hicho hakijasema ni makampuni gani yanayolengwa na wadukuzi hao au kama kuna taarifa zozote zilizoibiwa.
Lakini kituo hicho kimesema kuwa utafiti kuhusu chanjo haujaathiriwa na wadukuzi.
Urusi imekana kuhusika na tukio hilo.
''Hatuna taarifa kuhusu nani aliyedukua makampuni ya madawa na vituo vya utafiti nchini Uingereza. Tunaweza kusema jambo moja - Urusi haihusiki na majaribio ya udukuzi,'' alisema Dmitry Peskov, msemaji wa Rais Putin, kwa mujibu wa shirika la habari la Tass.
Tahadhari ilichapishwa kwenye taasisi za kiusalama za Uingereza, (NCSC) ,Canada (CSE), Idara ya usalama wa ndani Marekani (DHS) na Shirika la
usalama wa miundombinu ya kimtandao (CISA) pia Idara ya usalama wa taifa ya Marekani (NSA).
Mtaalamu wa masuala ya usalama amesema kuwa ni ''kweli'' , ingawa Urusi imekana, wadukuzi wa Urusi wanahusika.
Taasisi za Uingereza, Marekani na Canada zimesema wadukuzi wameharibu programu inayosaidia kufikia mifumo ya kompyuta , na walitumia programu za Well Mess na Well Mail kuweka na kupakua makablasha kutoka kwenye mashine zilizoharibiwa.
Phishing ni barua pepe zilizotengenezwa kwa ajili ya kumrubuni mtumiaji wa mtandao ili kutoa taarifa zake binafsi.
Spear phishing ni shambulio la kimtandao linaloundwa kwa makusudi ili kufanya udanganyifu kwa mtu.
Mara nyingi barua pepe humfikia mtu kutoka katika anuani inayoaminika, na inaweza kuwa na taarifa binafsi ili kufanya ujumbe uweze kuwa na
ushawishi zaidi. Lakini mmoja wa wataalamu wa masuala ya usalama wa mitandao ya kompyuta amesema kuwa si Warusi pekee wanaohusika kwenye kampeni hii.
''Wana watu wengi , tuna watu wengi, Wamarekani wana watu wengi zaidi, kama ilivyo kwa China,'' alieleza Profesa Ross Andersin kutoka Chuo cha Cambridge cha Maabara ya Kompyuta.
Wote hujaribu kuiba kila mara.''
Je ni nani wa kulaumiwa?
NCSC imeeleza kuwa kuna kikundi cha udukuzi kiitwacho APT29, ambacho pia kinajulikana kwa jina The Duks au Cozy Be
Imesema kuwa kuna uhakika zaidi ya 95% kuwa kikundi hiki ni sehemu ya maafisa wa intelijensia nchini Urusi.
Cozy Bear kwa mara ya kwanza walitambulika kuwa ''tishio '' mwaka 2014 kwa mujibu wa Kampuni ya usalama ya Crowdstrike.
Kundi hilo limeelezwa kuwa liliwahi kufanya udukuzi dhidi ya kamati ya kitaifa inayoratibu usaidizi wa wagombea wa Democrat nchini Marakani wakati wa uchaguzi wa urais mwaka 2016.
Mwaka 2017, ilikishambulia chama cha Labour, wizara za ulinzi na mambo ya nje, halikadhalika idara ya usalama wa taifa nchini Norway.
Ripoti ya wataalamu wa masuala ya usalama imejumuisha hitimisho la ushauri kuhusu namna ya kufanya kusaidia kuyalinda makampuni dhidi ya mashambulio ya kimtandao.
''Mwaka 2020, APT29 imelenga makampuni yanayohusika na utafiti na utengenezaji wa chanjo nchini Canada, Marekani na Uingereza, ikiaminika kuwa na lengo la kuiba taarifa na taarifa za umiliki wa mpango wa utengenezaji na majaribio ya chanjo dhidi ya Covid-19.'' Ilieleza ripoti hiyo.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Dominic Raab amesema: ''Haikubaliki kabisa kuwa maafisa wa usalama wa urusi wanawalenga wale wanaopambana kuhakikisha janga la corona linadhibitiwa.
''Wakati wengine wakiendeleza vitendo hivi vya ubinafsi kwa kutumia namna mbaya , Uingereza na washirika wake wako kwenye kazi ngumu ya kupata chanjo na kulinda afya ya watu duniani.''
Marekani imesema nini?
Mwanzoni mwa mwaka 2020, John Demers, msaidizi wa mwendesha mashtaka wa usalama wa taifa nchini Marekani, alitahadharisha kuwa wadukuzi kutoka nchi za kigeni walikuwa wakijaribu kuiba utafiti wa chanjo.
Alisema kuwa nchi ya kwanza kupata chanjo itakuwa na ''faida kubwa ya kupata mafanikio ulimwenguni.''
Kwa sababu hiyo, wadukuzi wamekuwa wakijaribu kuiba tafiti hizi katika nchi kadhaa.
Demers na wengine ambao wamekuwa wakifanya kazi katika idara ya usalama wamekuwa wakifuatilia nyendo hizo kwa karibu sana.
Hivi sasa wataalamu hao wamefahamu wazi nia ya wadukuzi na namna gani hutumia mifumo yao kupata kile wanachokitaka.