Burundi: Pierre Nkurunziza kuzikwa leo

Safari ya mwisho ya Nkurunziza

Chanzo cha picha, Ikulu Burundi

Maelezo ya picha, Safari ya mwisho ya Nkurunziza

Maelfu ya raia wa Burundi wamejitokeza katika mji wa Gitega kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais Pierre Nkurunziza wakati unasindikizwa kwa ajili ya mazishi ya taifa chini ya ulinzi mkali baada ya kufariki mapema mwezi huu.

Nkurunziza, ambaye aliongoza nchi hiyo kwa miaka 15, aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 55 kutokana na kile ambacho serikali imesema ni ugonjwa wa moyo.

Ijumaa ilitangazwa kuwa sikukuu ya taifa kwa ajili ya mazishi ya Nkurunziza.

Watoto wa shule waliovaa sare zao na raia walijitokeza barabarani kusubiri msafara uliobeba mwili wa Nkurunziza, kupita.

Uwanja wa Gitega ambapo hafla ya mazishi inafanyika pia kumejaa raia kutoka kila pembe ya nchi hiyo, wote wakiwa wamevaa nguo za rangi nyeupe kulingana na ombi la serikali.

Nkurunziza atazikwa katika mnara uliojengwa hivi karibuni huko Gitega katika ambalo lilitengwa kwa ajili ya waathirika wa majanga mengine kwa miaka mingi, lakini halikuwahi kuzinduliwa rasmi.

Safari ya mwisho ya Nkurunziza

Chanzo cha picha, Ikulu Burundi

Maelezo ya picha, Safari ya mwisho ya Nkurunziza

Denise Nkurunziza, mke wa aliyekuwa Rais wa Burundi amehudhuria hafla hiyo kwa ajili ya mume wake, Pierre Nkurunziza na kuzungumzia matendo ya mume wake ya kupigiwa mfano wakati wa utawala wake hadi mwisho wake.

Katika uwanja wa mchezo wa kandanda wa Gitega ambapo Waziri Mkuu wa Tanzania na mke wa rais wa Zambia walikuwa miongoni mwa wageni wa heshima, Bi. Nkurunziza amesema Mungu amempa "nguvu kipindi hiki cha majonzi".

Bi. Nkurunziza ambaye pia alikuwa amelazwa kwa ugonjwa usiojulikana, alilazimika kuondoka hospitalini Nairobi, nchini Kenya siku moja baada ya serikali kutangaza kifo cha mume wake kwa ugonjwa wa moyo Juni 9, 2020.

"…Binafsi nimempoteza mpendwa wangu, watoto wamempoteza mzazi wao. Namshukuru Mungu kwa kutupa nguvu kwa kuwa imara kipindi hiki kigumu, baada ya kumpoteza mtu ninayempenda ghafla." - Ameliambia taifa.

Bi. Nkurunziza ambaye alikuwa na watoto watano, alimsifu mume wake kwa mema aliyotendea nchi hiyo na kwamba mwisho wake umekuwa mwema na kufa kifo cha amani.

Hata hivyo, upinzani nchini Burundi na makundi ya haki za binadamu mara kwa mara yalikuwa yakishtumu serikali ya Nkurunziza kwa kushindwa kuwa na uvumilivu na kutekeleza ukiukaji wa haki za binadamu.

Leo hii, Pierre Nkurunziza ambaye ameiongoza Burundi kwa kipindi cha miaka 15, atazikwa Gitega katika makaburi maalum ambayo yamejengewa wiki mbili zilizopita.

Baada ya kifo cha Nkurunziza baadae hii leo, bendera za taifa katika nchi za Kenya, Rwanda, Uganda na Tanzania zitapandishwa tena juu baada ya kupeperushwa nusu mlingoti kwa karibia wiki mbili kama njia moja ya kuonesha heshima kwake.

Safari ya mwisho ya Nkurunziza

Chanzo cha picha, Ikulu Burundi

Maelezo ya picha, Safari ya mwisho ya Nkurunziza

Mlolongo wa magari yatakayosindikiza maiti yake utatoka kwenye hospitali hiyo utatoka Karusi na kuelekea katika mji wa Gitega ambao ni mji mkuu wa kisiasa katikati mwa Burundi.

Wananchi wameomba kusimama kwenye barabara kumuaga marehemu.

Kunatarajiwa hafla fupi ya jeshi kumtolea heshma za mwisho kwenye uwanja wa mpira wa Ingoma mjini Gitega,kabla ya mwili wake kupitishwa mbele ya wananchi watakaokuwa uwanjani humo kumwaga na baadae kufanyika maziko rasmi.

Tangazo la serikali ya Burundi linasema kwamba shughuli nyingine kama kuweka mashada ya maua kwenye kaburi lake au hotuba zitakazotolewa zitafahamishwa leo.

Rais Pierre Nkurunziza alifariki dunia tarehe 8 mwezi huu kutokana na mshtuko wa moyo kama ilivyotangazwa na serikali ya nchi hiyo.

Burundi"s President Pierre Nkurunziza

Chanzo cha picha, Reuters

Marais

Nkurunziza ni nani?

Pierre Nkurunziza amekuwa mwanasiasa wa Burundi na kuwa madarakani tangu mwaka 2005.

Bwana Nkurunziza, kijana wa aliyekuwa mbunge, alinusurika mauaji 1993 ya wanafunzi wa Kihutu katika chuo kiuu cha Burundi ambapo alikuwa mhadhiri na kujiunga na waasi wa FDD kundi ambalo baadae lilibadilika na kuwa chama tawala cha CNDD-FDD ambacho alikuja akawa kiongozi.

Alikuwa mwenyekiti wa chama tawala cha CNDD-FDD, hadi alipochaguliwa kama rais wa Burundi.

Baada ya makubaliano ya Amani ya Arusha kati ya serikali na waasi, Nkurunziza alitajwa kuwa waziri wa mambo ya ndani kabla ya bunge kumchagua kama rais Agosti 2005.

2015, Nkurunziza alichaguliwa katika uchaguzi uliokuwa na utata na chama chake kwa muhula wa tatu madarakani.

Wafuasi wake na wanaompinga Nkurunziza walikosa kukubaliana katika suala la ikiwa ilikuwa halali kwake kugombea tena na maandamano yakafuata.

Pia unaweza kutazama

Maelezo ya video, Safari ya kisiasa ya Pierre Nkurunziza nchini Burundi