Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
DRC yatangazwa kuudhiditi kabisa ugonjwa wa Ebola eneo la Mashariki
Mlipuko mbaya zaidi wa Ebola nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo umetangazwa kwisha, karibu miaka miwili tangu ulipotokea.
Hakuna wagonjwa wapya wa ugonjwa huo walioripotiwa Kaskazini Mashariki ya nchi hiyo, ambapo makundi kadhaa ya watu wenye silaha wamekuwepo, tangu tarehe 27 mwezi Aprili
Watu 2,280 wamepoteza maisha tangu kuanza mwezi Agosti mwaka 2018.
Mlipuko huo ulikuwa Afrika Magharibi kati ya 2014 na 2016 watu 11,000 wakiripotiwa kupoteza maisha.
Shirika la Afya duniani (WHO) amesema kuwa kumalizwa kwa mlipuko huo eneo la Mashariki, ambako pia suala la usalama ni tete, ni sababu ya kusheherekewa kwa kuwa hali ilikuwa ngumu na hatari kwa miaka miwili kwa wale waliokuwa wakipambana nao.
Hatahivyo, DR Congo, ambayo ina ukubwa wa eneo la bara la Ulaya Mashariki, inapambana na mlipuko mpya Kaskazini-Magharibi mwa nchini humo.Katika eneo la Mbandaka kulitangazwa tarehe 1 mwezi Juni vifo vya watu 13. Tathimini ya kijenetiki ilionesha kuwepo kwa aina nyingine ya virusi tofauti na ile iliyo Mashariki.
WHO nchini DRC iliiambia BBC kuwa hali ya Mbandaka- iko karibu kudhibitiwa.
Lakini milipuko mipya ya Ebola inatarajiwa kutokana na kuwepo kwa wanyama wenye virusi hivyo katika sehemu nyingi za DR Congo, WHO imeeleza.
Kwa mlipuko kutangazwa kuisha, inapaswa kusiwe na mgonjwa kwa siku 42 tangu mgonjwa wa mwisho kuthibitishwa kutokuwa na ugonjwa huo na kuruhusiwa kutoka hospitalini.
Kwa nini imechukua muda kwa ugonjwa huu kumalizika?
Mlipuko Mashariki mwa nchi hiyo ni wa kumi kushambulia nchi hiyo tangu mwaka 1976, pale virusi vilipogundulika na jopo la wanasayansi walioamua kuuita Ebola, jina la mto.
Waziri wa Afya Eteni Longondo alieleza kuwa '' ni ugonjwa mgumu kuukabili na hatari'' katika historia ya Congo.
Mzozo wa mashariki umesababisha hali ya mamlaka kutoaminika, hali ambayo ilisababisha mazingira ya wahudumu wa afya kufanya kazi kuwa magumu .
Mwandishi wa masuala ya afya Rhoda Odhiambo amesema kuwa kulifanyika zaidi ya mashambulizi 420 ya vituo vya huduma za afya tangu mwaka 2018, hali iliyozorotesha jitihada za kudhibiti kuenea kwa mlipuko huo.