Berzosertib: Dawa mpya ya saratani inayozuia uvimbe yawapatia matumaini wagonjwa

Dawa inayoweza kuzuia seli za saratani kujikarabati zenyewe imeonesha ishara za mapema za kufanya kazi.

Zaidi ya nusu ya wagonjwa 40 wa saratani waliopewa dawa ya Berzosertib iliwasaidia kuzuia uvimbe mwilini.

''Berzosertib ina uwezo zaidi inapopewa mgonjwa ambaye tayari anafanyiwa tiba ya kemikali {chemotherapy}'', ulisema utafiti huo unaoendeshwa na taasisi ya saratani ICR na Royal Marsden.

Majaribio yalilenga kupima dawa hiyo.

Dawa hiyo ni ya kwanza kufanyiwa majaribio ambayo huzuia protini inayosaidia katika ukarabati huo wa seli. Inapoathirika Protini hiyo huzuia saratani kukarabati seli zake.

Ni miongoni mwa tawi la tiba kwa jina 'precision', ambazo hulenga jeni maalum ama mabadiliko ya jeni.

Utafiti huo ulishirikisha wagonjwa walio na uvimbe wa muda mrefu ambao hakuna dawa imefanikiwa kuwatibu.

Hiki ndicho kilichojulikana kama awamu ya kwanza ya majaribio, ambayo yametengenezwa kupima usalama wa tiba.

Lakini ICR imesema kwamba watafiti walipata ishara za mapema kwamba berzosertib inaweza kuzuia uvimbe kukuwa.

'Inaonesha matumiani'

Mmoja wa waanzilishi wa utafiti huo Profesa Chris Lord, ambaye ni mtaalam wa vimelea katika taasisi ya ICR, alisema kwamba ishara hizi za mapema zilionesha matumaini ,akisema kwamba halikuwa suala la kawaida kwa vipimo vya awamu ya kwanza kuonesha matokeo.

Vipimo zaidi vitahitajika ili kuonesha uwezo wa dawa hiyo. Utafiti huu ulishirikisha idadi ndogo ya wagonjwa ....hivyobasi ni mapema mno kusema kwamba dawa ya Berzosertib imeonesha mafanikio katika kutibu saratani , alisema Dkt. Darius Widera katika chuo kikuu cha Reading.

"Uwezo mkubwa wa dawa ya Berzosertib inapotolewa kwa mchanganyiko wa tiba ya kemikali , hutoa sababu ya kuwa na matumaini kuhusu majibu ya tafiti zinazotarajiwa kufanyika mbeleni."

Philip Malling, mgonjwa wa saratani mwenye umri wa miaka 62 alipatikana na saratani ya utumbo 2012 na alishirikishwa katika jaribio hilo baada ya miaka miwili ya tiba ya kemikali ambayo haikumpa matumaini yoyote.

''Niliambiwa kwamba hakuna kitu cha ziada tunachoweza kufanya'', alisema. Mwezi Apili 2014 niliambiwa kwamba huenda nikawa nimefariki kufikia krisimasi.

Hivi sasa amekuwa akipatiwa tiba ya Berzoserti kwa miaka sita, uvimbe aliokuwa nao umepungua na hali yake kuimarika.

''Tiba hii ndio kila kitu kwangu'', bwana Malling aliambia BBC.

Another patient, whose ovarian cancer returned following a different course of treatment, saw her tumours shrink after combination treatment with the drug and chemotherapy.

Mgonjwa mwengine ambaye saratani yake ya shingo ya uzazi ilirudi kufuatia tiba tofauti za saratani alipata usaidizi baada ya uvimbe aliokuwa nao kuisha baada ya mchanganyiko wa dawa hiyo na tiba ya kemikali.

Tiba ya kemikali hufanyakazi kwa kuharibu seli za jeni , hivyobasi kuitumia pamoja na tiba hiyo mpya inayozuia seli kujikarabati , inaonesha kutoa faida nyingi zaidi.

Na Berzosertib ina uwezo wa kulenga seli zilizopo katika uvimbe bila kuathiri seli nyengine za kiafya, alisema Profesa Lord.

''Majaribio yetu ndio ya kwanza kujaribu usalama wa familia ya tiba inayokabiliana na saratani miongoni mwa wanadamu na ni matumaini kuona matokeo mazuri katika awamu za mapema'' , alisema Profesa Johann de Bono, mkuu wa kitengo cha utengenezaji wa dawa katika taasisi ya ICR iliopo Royal Marsden.

Katika siku za usoni, dawa hizi zinaweza kupiga jeki madhara ya tiba kama vile ile ya kutumia kemikali , na kukabiliana na sugu inayoweza kupatikana katika tiba zinazolengwa, aliongezea.

Huku ikiwa utamaduni wa kukabiliana na saratani ni uorodheshaji wa aina ya uvimbe - saratani ya matiti, saratani ya mapafu na nyinginezo - dawa hiyo inalenga uvimbe usiokuwa wa kawaida mwilini.

Uwezo wake umetumika, kwa mfano katika saratani ya tezi dume kuzuia athari ya homoni ya kiume inayohusika katika kusababisha uvimbe.

Iwapo itatumika pekee, inaweza kupunguza uwezo wake zaidi ya tiba ya chemotherapy , ambayo huvamia na kuua seli bila kuchagua.

Awamu ya pili ya kufanyia majaribio dawa hiyo tayari imeanza.