Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Polisi Kenya ashtakiwa kwa mauaji wakati wa amri ya kutotoka nje usiku
Polisi mmoja nchini Kenya ameshtakiwa kwa mauaji ya kijana Yasin Moyo, 13, ambaye alipigwa risasi akiwa barazani, wakati polisi wakisimamia utekelezaji wa amri ya kutotoka nje usiku.
Duncan Ndiema amekanusha mashtaka hayo.
Nje ya mahakama, wakili wake amesema kuwa serikali itahitajika kuthibitisha kwamba risasi iliyomuua kijana huyo ilitoka kwenye bunduki ya mteja wake.
Kesi hiyo inawadia huku wasiwasi ukiendelea kuongezeka juu ya nguvu inayotumiwa na polisi wakati wanatekeleza hatua za kukabiliana na virusi vya corona.
Hatua ya kutotoka nje usiku ilianzishwa mwisho wa Machi, pamoja na hatua zingine ili kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya corona.
Machi 30, Yasin alikuwa anashuhudia kinachoendelea akiwa kibarazani kwao katika nyumba moja ya ghorofa mjini Mathare, moja ya vitongoji duni katika mji wa Nairobi, wakati polisi wanashika doria, mama yake Khadija Abdullahi Hussein alizungumza na BBC Africa Eye.
'Nimepigwa risasi'
"Baada ya dakika chache nilisikia milio ya risasi, kwa hiyo nikawaambia watoto walale chini. Kisha nikagundua kwamba Yasin ameanguka chini ya kiti alipokuwa amesimama.
"Akaniambia: 'Mama nimepigwa risasi.'"
Bwana Ndiema ameshtakiwa baada ya uchunguzi uliofanywa na mamlaka ya kutathmini utendakazi wa polisi (IPOA).
Kwasasa hivi polisi huyo amezuiliwa na Jumatato mahakama itasikiliza ombi lake la kutaka kuachiliwa kwa dhamana.
Media captionKenya: Police brutality in the battle against coronavirus in Mathare
Mapema mwezi huu, BBC Africa Eye iliangazia wenyeji kuwa na hasira kuhusu namna watu walivyohudumiwa na polisi kipindi hiki cha corona.
Watu saba waliuawa katika sehemu mbalimbali nchini Kenya siku tano za kwanza za kutekeleza kanuni hiyo ya kutotoka nje usiku, Shirika Mikataifa la Kutetea Haki za Binadamu Amnesty International limesema
Rais Uhuru Kenyatta baade aliomba msamaha "kwa utumiaji nguvu uliotekelezwa".