Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mauji ya Tulsa: Kile kilichotokea katika mauaji ya 'Black Wall Street', mojawapo ya uhalifu mbaya zaidi katika historia ya ubaguzi Marekani
Mauaji hayo yametajwa kuwa mabaya zaidi dhidi ya jamii ya watu weusi nchini Marekani lakini ni tukio ambalo halijulikani
Kutokana na maandamano makubwa dhidi ya polisi yaliyoenea Marekani kote, siku hizi tukio baya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya mji wa Tulsa huko Oklahoma limeanza kukumbukwa.
Tukio hilo la kinyama lilitokea mwaka 1921 na kusababisha vifo vingi pamoja na uharibifu mkubwa katika jamii ya watu weusi katika eneo linalojulikana kama "Black Wall Street . "
Cha kushangaza, ni kwamba rais wa Marekani, Donald Trump amechagua mji huo kuanza kufanyia kampeni zake za uchaguzi wa rais, Novemba 3.
Je mauaji hayo yalitekelezwaje?
Mashambulizi hayo yalianzia kama uvumi kuwa kijana mweusi alikuwa ameshambulia msichana wa kizungu katika hoteli ya Tulsa iliyopo mjini.
Ilikuwa majira ya asubuhi , Mei 30, 1921, na Dick Rowland alikutana na mwanamke anayeitwa Sarah Page kwenye lifti. Maelezo ya kile kilichotokea yanatofautiana na walioshuhudia.
Taarifa zikaenea katika jamii ya wazungu katika mji huo, ambapo kila mmoja alizichochea kwa sababu watu wengi walikuwa wanasimuliana tofauti tukio hilo.
Polisi wa Tulsa walimkamata Rowland siku iliyofuata na kuanza kufanya uchunguzi.
Ripoti mbaya ambayo iliandikwa Mei 31 kuhusu tukio lililotokea katika mji wa Tulsa, iliandikwa katika gazeti la Tulsa Tribune hivyo kuibua ghasia kati ya jamii ya watu weusi na watu weupe , karibu na mahakama ambapo mku wa mji huo alikuwa anajaribu kuziba ghorofa ya juu ili kumlinda Rowland kutoshambuliwa na watu hao.
Kulikuwa na milio ya risasi, na jamii ndogo ya watu weusi ilianza kukimbilia katika kitongoji cha Greenwood ambako kunafahamika kama "Black Wall Street" kwa ajili ya kuhifadhi biashara zao ,kubwa na mali zao.
Mapema asubuhi , Juni 1, Greenwood ilivamiwa na kuunguzwa na waandamanaji wa jamii ya wazungu.
Baadae gavana wa Oklahoma bwana James Robertson alitangaza vita na kutuma wanajeshi.
Siku moja baada ya ghasia hizo za ubaguzi kutokea, vurugu zikaisha.
Wakati wa mapigano hayo, magorofa 35 yaliharibiwa na hii ina maanisha kuwa zaidi ya nyumba 1,200 ziliharibiwa.
Zaidi ya watu 800 walikuwa wamejeruhiwa na wengine 39 walidaiwa kuwa walifariki lakini wana historia wanakisia kuwa watu wapatao 300 walikufa .
Zaidi ya watu 6,000 ambao wengi walikuwa Wamarekani weusi walishikiliwa katika kituo cha maridhiano ya kisheria na baadhi walikuwa huko kwa muda wa siku nane.
Black Wall Street
Katika miaka ya mwanzoni ya miaka ya 1900s, kitongoji cha Greenwood kilibadilishwa muonekano kwa kuwa sehemu ya burudani kama vile kumbi za filamu, migahawa, maduka na studio za kupiga picha.
Ulikuwa mji ambao umejitenga na mingine ukiwa umetenganishwa na barabara ya reli.
Jina la Black Wall Street ("Black Wall Street") linaonyesha kuwa uchumi umekuwa, na kufanya wakazi jirani wa eneo hilo kuona kuwa ni mji mzuri zaidi wa jamii ya watu weusi katika nchi hiyo.
Uchumi ambao ulilipuliwa kwa muda wa siku mbili kwa risasi na ghasia umerudi .
Changamoto za nyuma
Mauaji hayo ya kimbari ya Tulsa hayakutokea kama tukio lililopangwa. Kuelewa kile ambacho kilitokea , jambo moja ambalo linaeleweka ni kuwa miaka miwili kabla wakati Marekani iliporejea kutoka vita ya kwanza ya dunia , wanajeshi wengi wa jamii ya watu weusi walikuwa walichomwa wakiwa hai nwakiwa wamevalia sare zao za jeshi.
Kwanza wakati wa msimu wa joto1919 ambao unajulikana Marekani kama kiangazi chekundu "Red Summer" uhalifu mkubwa wa kunyonga na matukio mengine ya kihalifu yalitokea katika miji mingine ya nchi dhidi ya jamii ya Wamarekani weusi.
"Mauaji ya kimbari ya Tulsa yalianza katika muktadha wa ," Ben Keppel, ambaye ni profesa wa idara ya historia katika chuo kikuu cha Oklahoma, aliifafanulia BBC World.
"Kuna ushahidi wa kutosha kuwa eneo la jirani kulikuwa kituo kikubwa cha uchumi mkubwa, na kusababisha hali ya chuki.
"Uwepo wa Wall Street ulikuwa wakati mgumu wa ubaguzi ambao uliichukiza jamii ya wazungu, nani anaweza kutoa mfano wa usawa wa hisia ambazo zingepelekea kuchoma moto, " alisema Keppel.
"Vilevile baada ya vita, uchumi wa Marekani ulishuka na kuathiri sekta ya mafuta. Kulikuwa na ubaguzi ambao ulikuwa umezikwa na kurejea tena wakati wa changamoto za kiuchumi.
"Inabidi kuelewa kile ambacho kilitokea kupigana, dhidi ya Imani kuwa watu weupe ndio wana mamlaka," alisema mwana historia.
Janga lililofichwa
Hata hivyo kwa muda mrefu , ilikuwa si rahisi kuelewa kile kilichotokea kwa sababu milikuwa hakijulikani.
Keppel mwenyewe hakuwahi kusikia kuhusu mauaji ya kimbari ya Tulsa hadi alipofika chuo kikuu cha Oklahoma kama profesa na tukio hilo lilitajwa na mwanafunzi mmoja darasani, mwaka 1994.
Lakini yeye mwenyewe hakuwahi kusoma historia hiyo akiwa shuleni au katika mafunzo yake ya kuwa mhadhiri wa chuo.
Hali hiyo imebadilika. Janga hilo lilikuwa tayari sehemu ya mtaala wa kufundishia shule nchini humo ingawa Wamarekani wengi walikuwa hawafahamu kilichotokea.
Katika nafasi yake ya kuratibu mpango wa kituo cha utamaduni cha Greenwood , Michelle Brown alijaribu kutunza kumbukumbu hiyo na kukusanya ushahidi kwa watu wachache walionusurika ambao wako hai mpaka sasa.
"Baada ya tukio hilo la kimbari , jamii zote mbili zilificha kile ambacho kilitokea , walitaka kuendelea tu na maisha, " Brown alimwambia mwandishi wa BBC Jane O'Brien.
"Kuzungumzia janga hilo ilikuwa inaleta ahueni maana lilikuwa la maumivu sana. Kuna akina mama ambao hawakufahamu nini kilitokea kwa watoto wao, kuna watoto walibaki bila wazazi na hawakufahamu lolote kuhusu wao."
Watu wapatao 300 walifariki na kuzikwa katika makaburi ya pamoja na miili yao haikupatikana.
Na hakuna aliyeadhibiwa kwa kile kilichotokea.
"Hatua za kisheria zilichukuliwa mwaka 1990 katika harakati za kujaribu kuwapa haki walionusurika lakini kutokana na uhalifu uliotokea hakuna kilichofanyika," alisema Profesa Keppel.
Mamlaka ya Tulsa ilizindua mradi mwaka jana wa kubaini makaburi ya pamoja yaliowazika wahanga kwa kutumia mfumo wa rada ili kubaini ..
"Inatupasa kuzungumza kuhusu hili kama jamii kwa sababu mji unahangaika, mji umegawanyika kwa sababu hatukuhusika katika sehemu hii ya historia, inabidi tufanye kitu ambacho kitatufanya tuendelee tukiwa wamoja, kuna uhitaji wa kuwapo kwa majadiliano ya watu kupata na kusameheana, " alisisitiza Brown.
Ni vigumu kurekebisha
Suala la kurekebisha kilichotokea ni gumu sana. Njia ya treni bado inagawa pande mbili za mji huo wa Greenwood na miji mingine.
Kufuatia dondoo za kihistoria, hakuna ushahidi wa uwepo wa ukuta huo mweusi mjini Tulsa .
"Familia yangu iliishi hapa mwaka 1921, na sasa hakuna mwisho," alisemaTherese Aduni.
Babu yangu alikuwa anatengeneza saa, baba yangu alizaliwa miezi michache baada ya mauaji ya kimbari.
"Walikubali tu neno mauaji ya kimbari kwa miaka mingi na waliita ghasia na kampuni za bima hawakulipa uharibifu uliotokea kwa wafanyabiashara au wamiliki wa nyumba au kwa yeyote aliyepoteza chochote," Aduni aliieleza BBC.
"Watu wanataka kulifumbia macho hili, tunaasikia kuhusu mauaji yaliyotokea Japan, manusura wa haolocaust , kwa nini sio sisi'' ? anauliza.
Kwake Aduni, suala la kufidiwa kuja kwa namna ya maendeleo ya uchumi, ni jambo ambalo analipinga kwa sababu ni mfumo ambao unakataliwa na jamii.
"Hatuna maduka makubwa! Tunataka maduka makubwa , maduka ya viatu na nguo ... tunataka biashara zote ambazo tulikuwa nazo, hiyo ndio itakayokuwa fidia."
Maafisa wa mji wanasema wanafanyia kazi kukabiliana na suala la usawa na kuna hatua zilizopigwa.
Mjadala mkubwa
Keppel amebainisha kuwa kuna nakala nyingi sasa za vitabu na ripoti zilizoandikwa kuhusu tukio la Tulsa ambalo lilitokea karibu miaka 100 iliyopita.
"Na matumaini kuwa huku karne hii ikiisha , sio tu taasisi zitaamka , lakini pia jinsi ambpo wamerkani wanajichukulia kama jamii kutakuwa na mabadilko," alisema.
"Katika maeneo yote ya nchi kuna simulizi ambazo zimefichwa na muhimu kuibuliwa na kujadiliwa. Lazima tuelewe kile kilichotokea Tulsa na miji mingine ,tunapaswa kujifunza," alisema.
Keppel alifananisha na mjadala mkubwa kuhusu ubaguzi ulioibuka hivi karibuni nchini Marekani.
" Kinachotokea sasa kinapaswa kuwafundisha watu kwa muda.
Kwa miaka 10 iliopita au miaka mitano au mmoja , tabia hii mbaya ya polisi imekuwa ikijirudia rudia katika nchi nzima na watu wamechoka.
"Kuna matukio machache katika historia ambayo yanachochea mabadiliko kwa kuibua hisia na mjadala mkubwa. Natumaini kuwa jambo hili ni moja wapo,"alimaliza.