Korea Kaskazini yasema Korea Kusini ni kibaraka wa Marekani

Maelezo ya video, Kaesong: Televisheni ya serikali ya Korea Kaskazini imeonesha vile ofisi ya uhusiano mwema kati ya nchi hiyo Korea Kusini ilivyoungua
Muda wa kusoma: Dakika 7

Korea Kaskazini imeelezea kwanini iliamua kulipua ofisi ya pamoja katika mji wa Kaesong.

Kwenye taarifa iliyotolewa, Korea Kaskazini imeishtumu Korea Kusini kwa kuvunja makubaliano yao ya 2018 na kuonesha tabia za kama "mbwa koko" huku dada yake kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini akimshtumu rais wa Korea Kusini kwa kuwa kibaraka wa Marekani.

Wakati huohuo, waziri wa Korea Kusini wa uhusiano wa masuala ya nchi hiyo na Korea Kaskazini ametoa barua yake ya kujiuzulu baada ya uhusiano wa nchi hizo mbili kuzorota zaidi.

Unification Minister Kim Yeon-chul speaking to a committee in the national assembly on Tuesday

Chanzo cha picha, EPA/YONHAP SOUTH KOREA OUT

Maelezo ya picha, Waziri wa uhusiano wa nchi mbili za Korea Kim Yeon-chul akizungumza mbele ya kamati bungeni Jumanne

Kim Yeon-chul amesema kwamba anawajibika kwa hali iliyotokea.

Hatua hiyo inawadia baada ya Korea Kaskazini kulipua ofisi ya pamoja ya nchi hizo mbili za Korea iliyokuwepo mpakani ambayo ilijengwa kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili.

Wakati huohuo, jeshi la Korea Kaskazini limesema kwamba litatuma wanajeshi wake katika maeneo yasioruhusiwa vita kwenye mpaka wa nchi hizo mbili.

Upande wa Korea Kusini nayo imekuwa ikiendelea kusema iko tayari kwa mazungumzo, lakini pia imeishitumu Korea Kaskazini na kutaja vitendo vyao kama watu wasio na akili na vyenye kusababisha uharibifu zaidi.

Katika wiki za hivi karibuni, wasiwasi umekuwa ukiendelea kuongezeka - kwa kiasi fulani ukisemekana kuchochewa na raia wa Korea Kaskazini waliotoroka Korea Kusini ambao wanapinga serikali kwa kuendeleza propaganda zao kupitia mpaka wa nchi hizo mbili.

Images of a building being blown up

Chanzo cha picha, twitter.com/nknewsorg

Maelezo ya picha, Chombo cha habari cha Korea Kaskazini kimechapisha picha za ofisi iliyoungua

Korea Kaskazini imesema nini?

Chombo cha habari cha Korea Kaskazini kinachomilikiwa na serikali kimeshtumu Korea Kusini kwa kuvunja makubaliano ya 2018, ikiwemo azimio la Panmunjom.

Taaifa hiyo ilimfananisha waziri wa ulinzi wa Korea Kusini na "mbwa koko muoga" ambaye anajiona mwenye fahari na jasiri, anayepindainda mazungumzo na mshirika mwenzake na kuchochea mazingira ya kuzozana.

Wakati huohuo, jeshi la Korea Kaskazini limesema kwamba itapeleka wanajeshi walke katika eneo kulikokuwa na ofisi ya ushirikiano kwa pande hizo mbili mji wa kiviwanda wa Kaesong na mlima Kumgang - eneo la kitalii mashariki mwa pwani.

Aidha Kim Yo-jong - dada yake kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong-un - alimshambulia Rais wa Korea Kusini kwa maneno.

"Sababu kutofanikiwa kwa makubaliano mazuri ya kaskazini na kuzini - ambayo hayakutekelezwa hata chembe ni kibaraka wa Marekani."

"Hata kabla ya wino wa makubaliano ya kaskazini na kusini kukauka, alikubali 'ushirikiano wa kikazi wa Korea Kusini -Marekani' chini ya shinikizo la mkuu wake.

Jumanne, jeshi la Korea Kaskazini lilisema linafuatilia hatua inatakayochukuliwa na jeshi lake kwenda eneo hilo ambalo haliruhusiwi shughuli za kijeshi.

Mkuu wa jeshi alisema liko katika hali ya tahadhari na tayari kutekeleza hatua yoyote itakayochukuliwa na serikali.

Taarifa hiyo inawadia baada ya dada yake kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kutishia kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Korea Kusini Jumamosi.

"Nahisi kabisa wakati umewadia wa kukatiza uhusiano na mamlak aya Korea Kusini," alisema Kim Yo-jong, ambaye anashikilia nafasi ya juu katika ngazi ya siasa za Korea.

Aliahidi kuchukua hatua, na kwamba ameagizajeshi , na kumalizia taarifa yake kwa maneno yafuatayo:

"Uchafu unastahili kutupwa jalalani."

Moon Jae-in and Kim Jong-un

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, The days of smiles and handshakes between President Moon and Kim Jong-un seem well in the past

Korea Kusini imejibu vipi?

Rais Moon Jumatano alisema Korea Kaskazini inatekeleza vitendo kama wasio na akili na kuonya kwamba Seoul haitakubali vitendo vya Kaskazini visivyokuwa na msingi.

Licha ya kulipuliwa kwa ofisi ya ya ushirikiano wa pamoja kwa nchi hizo mbili, Kusini ina matumaini kwamba makubaliano ya 2018 yanaweza kutekelezwa.

"Msimamo wetu ni kuwa makubaliano ya kijeshi ya Septemba 19, yanastahili kutekelezwa bila pingamizi lolote kwa misingi ya kupatikana kwa Amani katika rasi ya Korea na kuzuia migogoro," Waziri wa ulinzi wa Korea Kusini amesema.

Ilionya kwamba, ingawa vitendo vyovyote vya kijeshi vya Korea Kaskazini vinafuatiliwa kwa karibu, na hatua thabiti itachukuliwa kwa uchokozi wowote wa kijeshi.

Korea Kusini pia ilitoa wito wa kutuma ujumbe wake maalum ili kushughulikia hali ya sasa lakini Korea Kaskazini imekuwa haraka sana kukataa wazo hilo.

Images of a building being blown up

Chanzo cha picha, twitter.com/nknewsorg

Maelezo ya picha, Chombo cha habari cha Korea Kaskazini kimechapisha picha za ofisi iliyoungua

Jumanne, Korea Kaskazini ilikipua ofisi ya pamoja ya nchi hiyo na Korea Kusini karibu na mpaka wa mji wa Kaesong, maafisa wa Korea Kusin wamesema.

Hatua hiyo iliwadia saa chache baada ya Korea Kaskazini kutoa vitisho vya kuchukua hatua za kijeshi katika mpaka wa Korea.

Eneo lililolipuliwa lipo kwenye eneo la Korea Kaskazini, ofisi ambayo ilifunguliwa 2018 kusaidia nchi hizo mbili kuwasiliana.

Ofisi hiyo ambayo imekuwa kiunganishi kwa nchi hizo imekuwa bila mtu kuanzia Januari kwasababu ya hatua zilizochukuliwa kukabiliana na virusi vya corona.

Katika kipindi cha wiki za hivi karibuni, wasiwasi kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini umekuwa ukizidi kuongezeka, kutokana na makundi ya raia wa Korea Kaskazini yaliyotorokea Kusini. Ambayo yamekuwa yakituma ujumbe wa propaganda.

Dada ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Yo-jong, kutishia kulipua ofisi hiyo katika taarifa aliyoitoa wikendi.

Wizara ya Korea Kusini inayosimamia maridhiano ya nchi hizo mbili mjini Seoul imethibitisha kwamba saa 14:49 saa za eneo hilo, kumetokea mlipuko.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Awali, jeshi lilikuwa limesema kwamba liko tayari kuchukua hatua yoyote itakayoagizwa na serikali na kuwa liko tayari pia kubadilisha eneo hilo kuwa ngome yao na kugusia kuwa liko macho.

Participants attend an opening ceremony of the joint liaison office in Kaesong, North Korea, September 14, 2018.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Ofisi iiliyochomwa moto ilifunguliwa Sepemba 2018 kwa taadhima kuu

Jumanne, Pyongyang ilitangaza kwamba inakata mawasiliano yote na Seoul.

Wasiwasi kati ya nchi hizo mbili umekuwa ukiongezeka kwa muda sasa kwasababu ya vipeperushi ambavyo vimekuwa vikisambaa katika mpaka wa maeneo hayo mawili ambavyo kawaida huwa vinatumwa kwa njia ya maputo.

Waziri wa ulinzi wa Korea Kusini Jumanne amejibu vitisho hivyo kwa kusema kuwa inashirikiana na Marekani kufuatilia kwa karibu hatua za kijeshi upande wa Korea Kaskazini.

Maelezo ya video, South Korean activists launch propaganda balloons over border (2014 video)

Ofisi ya Kaesong ya ushirikiano wa nchi hizo mbili ina maanisha nini?

Mji wa Kaesong kwa miaka minne umekuwa nembo ya uhusiano ambayo umekuwa ukiyumba kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini.

Mwaka 2003, mji huo ulijitokeza kama eneo la kiviwanda wa Kaesong ambayo ilianzishwa na Korea zote mbili.

Mji huo, kuna wakati ulikuwa na zaidi ya viwanda 120 ambapo watu zaidi ya 50,000 wa Korea Kaskazini na mamia ya mameneja wa Korea Kusini.

Lakini 2016, mji huo ukafungwa baada ya kutokea kwa msukosuko wa kisiasa na kupelekea kusitishwa kwa shughuli.

Tangu 2018, mambo yalionekana kurejea katika hali yake ya kawaida pale nchi zote za Korea zilipokubaliana kufungua ofisi hiyo ya pamoja katika mji wa Kaesong.

Lakini MMachi 2019, Korea Kaskazini ilitangaza kwamba inajitoa kutoka kwa ofisi hiyo - baada ya mkutano uliokuwa unapangwa kufanyika baina ya Marekani na Korea Kaskazini kushindikana.

Kim Yo-jong ni nani?

Kim Yo-yong

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Dada ya kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Yo-jong, ameendelea kujionyesha kama mwenye madaraka ya juu

Katika miaka ya hivi karibuni, dada ndogo wa Kim Kim Jong-un amejitokea kuwa mtu wake wa karibu na mshika mkuu.

Kuanzia 2014, kazi kubwa ya Kim Yo-jong imekuwa kulinda hadhi ya kaka yake na kuchukua majukumu muhimu katika chama.

Kutokana na mabadiliko yaliyofanyika 2017 katika chama cha Kikomunisti,, iliashiria kwamba anachukua nafasi ya juu ya uongozi ingawa jukumu lake kubwa limesalia kwenye propaganda.

2018, alionekana kutanda kwenye ulingo wa kimataifa katika michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridid kwa kuwa mtu wa kwanza kutoka familia ya Kim kutembelea Korea Kusini.

Mchango wake umeendelea kumfanya kuwa karibu na kuongeza uaminifu kati yake na kaka yake.

Aprili pale Kim alipokuwa haonekani hadharani huku maswali mengi yakiibuka kutokana na afya yake - alioneshwa kama mwenye uwezokano wa kuwa mrithi wake.

Wiki za hivi karibuni, amekuwa akitoa matamshi makali dhidi ya Korea Kusini na kuonekana hususan, kuwa mwenye kushughulikia masuala ya nchi hiyo na Korea Kusini kulingana na tovuti ya NK News.

Hata hivyo imekuwa vigumu kufahamu madaraka ya watawala wa Korea Kaskani.

Na kufanya iwe changamoto zaidi kujua nguvu yake - kiwango cha mtandao wake wa kisiasa - kwa dada huyo mwenye umri wa miaka 32.

Kwanini Korea Kaskazini inafanya hivi?

Analysis box by Laura Bicker, Seoul correspondent
Maelezo ya picha, Uchambuzi na Laura Bicker, mwanahabari wa BBC Seoul

Korea Kusini imechukulia tishio hilo kwa uzito mkubwa.

Shughuli za kijasusi zimeimarishwa katika eneo salama na Rais Moon ametoa wito wa kuwa na utulivu - na kutaka Pyongyang kujizuiza kufanya hali hiyo kuwa mbaya zaidi.

Lakini hali hii imefika vipi hapa?

Kwanza, Korea Kaskazini imelalamikia makundi yanayoendeleza propaganda. Korea Kusini imeamua kuzuia vipeperushi vinavyoingizwa nchini humo kupitia mpaka kama sehemu ya makubaliano kati ya nchi hizo mbili za Korea kati ya Rais Moon na Kim Jong Un mwaka 2018.

Pili, Pyongyang imekasirishwa na hatua ya seoul ya kutoshinikiza Marekani kuiondolea Korea kaskazini vikwazo.

Kwa hiyo, kuna uwezekano ikawa jambo kubwa.

Pia muda wa kuchukuliwa kwa hatua ya kukatizwa kwa mawasialiano hadi vitisho vilivyochukuliwa vya kijeshi kama kuliko pangwa.

Korea Kaskazini huenda inapalilia tatizo ili kuweza kuadhibu Korea Kusini na pengine kutumia fursa hiyo kama njia ya kuwa na ushawishi kwenye mazungumzo ya siku za baadae.

Kwa tishio lililotolewa, kunalenga kurejesha nyuma hatua ambayo imeshapigwa na Rais Moon 2018.

Jumla ya majengo 20 marefu yakiulinzi yalibomolewa - huku kukiwa na matumaini ya kubadilisha eneo hilo la mpaka lenye shughuli nyingi za kijeshi duniani kuwa eneo salama.

Rais Moon alisema anatafuta njia ya kufikiwa kwa Amani ambako hakuwezi kubadilishwa tena katika rasi hiyo ya Korea.

Hata hivyo Korea Kaskazini huenda ikawa iko karibu kumthibitishia kuwa alikosea.

Presentational grey line

Mzozo wa vijipeperushi ulianza lini?

Wiki jana Pyongyang ilikatisha mawasiliano yote na Korea Kusini, ikiwemo mawasiliano ya moja kwa moja kati ya viongozi wa nchi hizo mbili.

Ilisema kwamba imekasirishwa na raia wa Korea Kaskazini waliotorokea Korea Kusini ambao wanatuma vipeperushi kapitia mpaka wa nchi hizo mbili.

Makundi ya watu hao mara kwa mara yamekuwa yakituma maputo yenye vipeperushi na vyenginevyo ikiwemo chakula, pesa dola 1 kulipia gharama, redio na kifaa cha USB pamoja na taarifa za Korea Kusini.

Serikali ya Korea Kusini imejitahidi kusitisha tabia hiyo kwa kusema kwamba inaweka makaazi ya walio karibu mpaka hatarini.

Rais Moon Jae-in Jumatatu aliisihi Korea Kaskazini kurejea katika meza ya mazungumzo na wala sio kufanya hali kuwa mbaya zaidi.

Je eneo lisiloruhusiwa shughuli za kijeshi kuna maanisha nini?

Eneo hilo lilianzishwa baada ya Vita ya Korea Kaskazini miaka ya 1953 ili kutenga eneo salama kati ya nchi hizo mbili.

Kwa miongo kadhaa eneo hilo mara kwa mara huwa linashuhudia milio ya risasi, wanajeshi wa Korea Kaskazini hutoroka na mazungumzo ya amani hufanyika kutuliza hali. Upande wa Korea Kusini, eneo hilo ni kivutio cha utalii.

File photo of the DMZ

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mpaka wa Korea ni eneo lenye shughuli nyingi zaidi za kijeshi duniani

Wakati wa maridhiano kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini, eneo hilo pia lilikuwa la maridhiano ya ana kwa ana kati ya Kim Jong-un, Donald Trump na Moon Jae-in.

Kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita, serikali ya Korea Kusini mjini Seoul imejitahidi kubadilisha eneo hilo ambalo lilikuwa uwanja wa mapigano makali hadi ukanda wa Amani.

Makubalino ya kupunguza wasiwasi wa kijeshi katika eneo hilo la mpaka kulifikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili katika mkutano wa Pyongyang uliofanyika Septemba 2018.

Hadi kufikia sasa, licha ya jina lake, eneo hilo bado ni lenye shughuli nyingi za kijeshi duniani.

Donald Trump and Kim Jong-un

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mazungumzo ya amnai ya kimataifa yalikuwa yameleta matumaini kidogo kwamba wasiwasi kati ya nchi hizo kunaweza kutafutiwa ufumbuzi