Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Sababu ya maandamano kuwa na nguvu wakati huu nchini Marekani
Maelfu ya Wamarekani wamekuwa wakiandamana katika mitaa mingi nchini humo kupinga ubaguzi - kwa mara ya kwanza idadi ya watu imekuwa kubwa kiasi hicho. Lakini ni kwa nini tukio hilo la mauaji ya George Floyd limesababisha muitikio mkubwa kiasi hicho?
George Floyd sio Mmarekani mweusi wa kwa kwanza ambaye kifo chake kilisababishwa na polisi na kusababisha maandamano.
Kulikuwa na maandamano pia ya kutaka mabadiliko baada ya kufariki kwa Tamir Rice, Michael Brown na Eric Garner ambao wote waliuwawa na polisi.
Lakini wakati huu, muitikio unaonekana ni tofauti,muitiko wa maandamano ni mkubwa na umesambaa katika maeneo mengi.
Kumekuwa na maandamano Marekani yote katika majimbo yote 50 na DC - ikiwemo miji ya mjini na vijijini ambako kuna raia wengi wa kizungu.
Serikali za mtaa, wadau wa michezo na biashara wameonekana kuunga mkono wakati huu - haswa kutoka manispaa ya Minneapolis katika ofisi za polisi.
Na maandamano dhidi ya thamani ya maisha ya watu weusi 'Black Lives Matter' yanaonekana kuangalia ubaguzi zaidi - yakiwa na idadi kubwa ya watu ambao wengi ni wazungu na jamii nyingine wakiwa pamoja na wakiwa pamoja na wanaharakati wa watu weusi.
Kuna vigezo vingi ambavyo vimejumuishwa kwa pamoja kwa ajili ya mabadiliko baada ya kifo cha George Floyd.
Mwanaharakati Frank Leon Roberts, ambaye ni mwalimu pia anayefundisha pia masomo ya harakati za thamani ya maisha ya watu weusi mjini pia New York University, ameiambia BBC.
Kifo cha Floyd ndio kimechochea haya yote yanayotoa sasa'
Afisa polisi, Derek Chauvin, aliendelea kukandamiza goti laki katika shingo ya bwana Floyd kwa karibu dakika tisa - hata wakati bwana Floyd alirudia kusema kuwa hawezi kupumua na mwishowe akapoteza uhai kabisa.Tukio hilo lilirikodiwa vizuri katika picha ya video.
"Katika matukio mengi ya awali ya vurugu za polisi, kulikuwa na uwezekano wa kutokea kwa simulizi ambayo isiyoeleweka- kueleza nini kilichotokea haswa, au polisi kudai kuwa walifikia uamuzi huo ili kutetea maisha yao pia" alisema bwana Roberts.
"Lakini katika tukio hili , lilikuwa tofauti kabisa na lilionekana wazi kuwa haki haikutendeka - watu waliweza kumuona huyo mtuhumiwa [Floyd] akiwa hana silaha yeyote ya kuweza hatarisha maisha yao polisi.
Watu wengi wamejumuika katika maandamano haya kwa mara ya kwanza, jinsi walivyoona kile ambacho alifanyiwa George Floyd's, hawakuweza kubaki nyumbani.
"Kuna mamia ya vifo ambayo huwa hayachukuliwi katika video lakini tukio hili limeseza kuwafumbua watu macho kujua chuki ambayo inaendelea," Sarina LeCroy, muandamaji kutoka mji wa Maryland, aliiambia BBC.
Ni sawa na Wengfay ambaye alisema ataendelea kuunga mkono harakati za maisha ya watu weusi lakini kifo cha George Floyd kilikuwa cha kusikitisha sana na kilimfanya kwa mara ya kwanza kwenda barabarani kuandamana kwa mara ya kwanza.
Kilivuta hisia za wengi kutaka mabadiliko ya haraka sasa.
Maandamano hayo yamekuja wakati wa mlipuko na changamoto ya ajira.
"Historia huwa inabadilika wakati ambao msukumo ambao hukulitarajia unapotokea, ," alisema bwana Roberts.
Kifo cha bwana Floyd kilitokea katikati ya mlipuko wa virusi vya corona wakati ambao amri ya kutotoka nje ya nyumba zao ilipotolewa na kusababisha watu wengi kutokuwa na ajira , kwa asilimia kubwa jambo ambalo halikuwahi kutokea tangu mwaka 1930.
"Uko kwenye hali ambayo kila mtu katika nchi yuko kwenye marufuku ya kutoka nje na watu wengi wako ndani wanaangalia TV... watu Zaidi wanalazimika kuangaliwa Zaidi - wako katika wakati ambao hawawezi kuangalia mbali na wanaweza kukwazika kwa haraka.
Mlipuko wa corona tayari umebadili namna tunavyoishi na kufanya kazi na wamarekani wengi waliopo nyumbani wamejiuliza wenyewe ni namna gani ya isiyo ya kawaida haikubaliki tena", aliongeza.
Kiuhalisia kama watu Zaidi ya 13% Marekani hawana ajira hivyo watu wengi wanaweza kwenda kwenye maandamano bila ya kuwa na kipingamizi chochote.
Kifo cha bwana Floyd kilitokea muda mfupi baada ya kifo cha Ahmaud Arbery na Breonna Taylor.
Bwana Arbery, 25, alipigwa risasi na polisi tarehe 23 Februari wakati akiwa anafanya mazoezi mjini Georgia, baada ya wakati wa eneo hilo kumshuku kuwa amefanana na mwizi.
Breonna Taylor, 26, alikuwa mtumishi wa huduma ya afya ambaye alipigwa risasi nane wakati akiwa anaingia katika makazi yake.
Majina ya hao wote wawili yalitajwa katika maandamano ya hivi karibuni ya 'Black Lives Matters' huku waandamanaji wakiwa wanataja jina la bi.Taylor.
Bwana Roberts alielezea kifo cha bwana Floyd kama nyasi zilizosalia katika jamii nyingi , na kuongeza kuwa haya yanatokea wakati huu wa kiangazi ambapo watu wanataka kutoka nje, hivyo ni kitu ambacho wanaona pia kina manufaa kwao.
Vivyo hivyo mwaka huu ni wa uchaguzi , ina maanisha kuwa wanasiasa wataweza kuchukulia maanani Zaidi suala hili na kuchukua hatua kukabiliana nalo.
Maandamano haya yanaonekana kuwa sio ya watu weusi tu
Huku ikiwa ni vigumu kuonyesha takwimu ya watu wanaoandamana kulingana na rangi au asili yao, waandamanaji wengi ambao wanaunga mkono harakati hizi wanaonekana sio wamarekani weusi wenyewe.
Kwa mfano mjini Washington DC, Makumi ya maelfu ya waandamanaji ambao wamejitokeza barabarani siku ya Jumamosi karibu ya Zaidi ya nusu sio watu weusi.
Wengi wa waandamani walikuwa wamebeba mabango yakiashiria harakati hizo.
Katika sanduku la maoni ya ABC, Kuna maoni ya Wamarekani wapatao 74% ambao wamehisi kuwa kifo cha bwana Floyd ilikuwa sehemu ya kuvuka kutoka katika namna ambavyo wamarekani weusi wanavyotendewa ndivyo sivyo na polisi.
Haya ni mabadiliko ya haraka ambayo yanafanana na maoni yaliyotolewa mwaka 2014, baada ya kifo cha Michael Brown na Eric Garner - ambapo 43% ya Wamarekani walihisi kuwa tatizo ni kubwa Zaidi, ABC iliripoti.
Wakati harakati za kupambania haki ya mtu mweusi imekuwa ya kila mtu sio watu weusi wenyewe tu ... watu weupe wenyewe Marekani wamekosa maneno ya kuongea kuhusu ubaguzi", bwana Roberts alisema.
"sio kitu ambacho wanakifurahia na kuzungumzia suala la ubaguzi wanahisi wanashambuliwa wao na kuhisi kuwa hawana haki ya kuongea kwa sababu wanaweza kuwa wanamdhihaki mtu."
Hata hivyo sasa maandamano haya yanaonekana kuungwa mkono na wazungu Zaidi na wanajihisi kuwa sawa kwa hisia ya kuwa tofauti ".
Aliongeza kuwa idadi kubwa ya maandamano katika miji mikuu kulikuwa na maandamano hata kwenye vitongoji vidogo kama Anna ambako kuna ubaguzi mkubwa wa rangi , huko Texas, ambako kunajulikana kwa kikundi cha watu weupe cha Ku Klux Klan.
Kutokana na hali ya kifo cha bwana Floyd ilivyo imewafanya watu waungane kiurahisi zaidi.
Kwa maoni yake mwandishi wa habari Judy Mueller aliyeandika kuhusu , Mji wangu mdogo ulioingia katika maandamano, hatuko peke yetu.
Mwandishi huyo alisema watu wapatao 40 walikuwa wanaandamana huko Norwood, Colorado.
Waandaaji wa maandamano walisema kuwa kuunga mkono harakati hizi ni jambo muhimu na sio suala la kisiasa , Candy Meehan kutoka Republican, alisema "Sidhani kama hili ni suala la kisiasa … kibaya ni kibaya tu."
Waandamanaji weusi wameupokea ushiriki wao.
Eric Wood, kutoka makazi ya DC , alisema alijiunga katika maandamano baada ya kifo cha Trayvon Martin mwaka 2012, na kifo cha Breonna Taylor mapema mwaka huu, lakini ,muitikio wa maandamano haya ndio unaonekana kuwa mkubwa Zaidi.
"Wamarekani weusi ambao ni wachache wamekuwa wakiandamana dhidi ubaguzi kwa miaka mingi .Sauti zetu hazikuwa na uzito mkubwa kama sasa ambapo tumepata ushirika wa wazungu.
Pamoja na hayo bwana Roberts alidai kuwa d: "Historia inaeleza wazi kuwa watu wanaohitajika kubadilika ni wale ambao mfumo ulipo unawapendelea."
Tukio la polisi lina maana gani?
Waandamanaji wengi nchini Marekani wamekuwa wakifanya maandamano ya amani - wakati huo huo polisi nao walionekana kuunga mkono maandamano hayo .
Ingawa katika matukio kadhaa kulikuwa na ghasia kati ya polisi na waandamanaji.
Wiki iliyopita, mamlaka iliwaondoa waandamanaji wasiandamane nje ya ikulu ya Marekani White House. Baada ya muda mfupi, rais Donald Trump alipita mtaani na kutaka kupiga picha mbele ya kanisa.
Waandishi wa habari wengi wameripotiwa kulengwa kushambuliwa na polisi kwa kurushiwa mabomu ya gesi .
Baadhi ya maandamano yalitokea baada ya kuona polisi wanatumia nguvu nyingi kuzuia maandamano hayo.
Ben Longwell na Justine Summers walisema kuwa kuliwa na wahudumu wa afya ambao waliamua kuingia katika maandamano hayo DC - licha ya ugumu wa kuacha nafasi uliokuwepo kati ya mtu na mtu kutokana na hatua ambazo polisi walichukua.
"Hii ndio mara yangu ya kwanza katika maisha yangu kuwaogopa polisi, alisema bwana Longwell .
"Uhalisia ni kuwa hatutaki mtu yeyote kuumia, lakini tumegundua kuwa harakati za kisiasa na vyombo ya habari vinafanya jambo hili kuepo, alisema Roberts.
Hatima ya maandamano haya ni nini?
Waandamanaji wengi wamekuwa wakitaka mabadiliko fulani - ikiwa ni lazima polisi kuvaa kamera , kupunguza ufadhili kwa polisi na kuhamasisha watu kupiga kura kwa wingi.
Bwana Roberts alisema ni mapema mno kusema kama maandamano haya yanaweza kuleta mabadiliko ya harakati za muda mrefu wa miongo kadhaa tangu miaka ya 1950."