Virusi vya corona: Dhana potofu mitandaoni zina athari gani kwa watumiaji wa mitandao

Habari ghushi ni 'kirusi chenyewe'

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Habari ghushi ni 'kirusi chenyewe'
Muda wa kusoma: Dakika 6

BBC inafuatilia taarifa za upotoshaji kuhusu virusi vya corona ambazo zimesababisha mashambulizi, vifo na vitendo vya uchomaji moto, na wataalamu wanasema vitendo hivi vimesababishwa na taarifa ghushi mitandaoni na kuwa hali hii inaweza kuongezeka kwa kiasi kikubwa.

Tulifikiri serikali ilikua inatuvuruga'' anasema Brian Lee Hitchens, ''au ilikua inahusu mtandao wa 5G. Hivyo hatukufuata sheria wala kutafuta msaada haraka.''

Brian, 46, anazungumza kwa simu kutoka katika klitanda cha hospitali alimolazwa mjini Florida. Mke wake anaumwa sana - akiwa mahututi kwenye mashine ya kusaidia kupumua katika wodi mkabala naye.

''Changamoto iliyokuwa ikiwakabili ni mapafu ya mkewe,'' anasema '' alikuwa hajitambui.''

Baada ya kusoma nadharia za uongo mtandaoni, walifikiria kuwa ugonjwa huo ni wa uongo- au sio ugonjwa mbaya au hatari kuliko wa mafua. Lakini mwanzoni mwa mwezi Mei, wenza hao walipata maambukizi ya Covid 19.

''Na sasa nimegundua kuwa virusi vya corona si ugonjwa bandia,'' anasema akiwa anaishiwa pumzi. ''ugonjwa upo na unasambaa.''

Brian Lee Hitchens alifikiri kuwa hakuna ugonjwa uitwao covid-19 lakini yeye na mkewe waliambukizwa

Chanzo cha picha, Brian Lee hitchens

Maelezo ya picha, Brian Lee Hitchens alifikiri kuwa hakuna ugonjwa uitwao covid-19 lakini yeye na mkewe waliambukizwa

Upotoshaji hatari wa taarifa

Timu ya BBC imekuwa ikifuatilia taarifa za kupotosha zilizokuwa zikiongezeka kuhusu virusi vya corona. Tumechunguza watu kadhaa- baadhi yao ambao hawakuripotiwa- kuongea na watu waliopata maambukizi na mamlaka za tiba zikijaribu kuthibitisha taarifa hizo.

Madhara yameonekana duniani kote.

Uvumi ambao ulisababisha mashambulizi ya makundi nchini India na watu kuuawa kwa sumu Iran. Wahandisi mitambo ya simu wamekuwa wakitishiwa na kushambuliwa na minara ya simu imekuwa ikichomwa moto nchini Uingereza na nchi nyingine kwa sababu ya nadharia za uongo.

Bidhaa za usafi zenye sumu

Ilikuwa mwishoni mwa mwezi Machi pale Wanda na Gary Lenius walipoanza kusikia kuhusu hydroxychloroquine.

Wenza hao waligundua kuwepo kwa kiambato chenye jina linalofanana kwenye nembo iliyokuwa kwenye chupa ya zamani ambayo ilikuwa nyumbani kwao Phoenix.

Hydroxychloroquine inaweza kuwa muhimu katika kupambana na virusi- lakini utafiti unaendelea, bado haijathibitishwa. Siku ya Jumatatu, Shirika la Afya duniani WHO ilizuia matumizi ya dawa hiyo kwenye majaribio baada ya utafiti wa hivi karibu ni kuonesha kuwa matumizi yake yanaweza kumsababishia mgonjwa kuwa kwenye hatari ya kupoteza maisha kutokana na Covid-19.

Makisio kuhusu ufanisi yalianza kusambaa mitandaoni nchini China mwishoni mwa mwezi Januari. Mashirika ya habari, vikiwemo vyombo vya habari vya China, viliandika kwenye mtandao wa Twitter kuhusu tafiti za zamani kuhusu dawa hiyo.

Dawa za Hydroxychloroquine

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Dawa za Hydroxychloroquine

Kisha Daktari mmoja nchini Ufaransa alidai kuwepo kwa matokeo ya kutia moyo. Ingawa baadae kulikuwa na mashaka kuhusu utafiti huo, shauku kuhusu matumizi ya hydroxychloroquine ilipamba moto.

Pia dawa hiyo ikajipatia umaarufu kupitia Ikulu ya Marekani, pale Rais Trump alipoandika katika ukurasa wake wa Twitter.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

''Unapoteza nini ?'' alisema tarehe 3 mwezi Aprili. ''Meza.'' katikati ya mwezi Mei, alisema- alikuwa akifuatilia ushauri wake mwenyewe. Kila maoni yaliyokuwa yakitolewa yalikuwa yakisababisha malumbano makali mitandaoni kuhusu dawa hiyo, kwa mujibu wa data kutoka kwenye chombo kinachofuatilia data mtandaoni CrowdTangle.

Matumizi ya dawa kupita kiasi ni nadra, lakini hali ya hofu iliyotokana na janga la corona limewafanya watu kuchukua hatua zisizo za kawaida.

Nchini Nigeria, watu kadhaa walifikishwa hospitalini kutokana na tatizo la matumizi ya kupita kiasi ya dawa ya hydroxychloroquine na kusababisha sumu, hali iliyosababisha maafisa wa afya wa jimbo la Lagos kuwaasa watu dhidi ya matumizi ya dawa.

Mwanzoni mwa mwezi Machi mtu mmoja raia wa Vietnam alifikishwa katika hospitali moja kitendo cha udhibiti sumu mjini Hanoi baada ya kunywa kiasi kikubwa cha chloroquine. Alikuwa mwekundu na hakuweza kuona vizuri. Mkurugenzi wa hospitali , Dokta Nguyen Trung Nguyen, alisema mtu huyo alikuwa na bahati ya kupatiwa matibabu haraka- vinginevyo angeaga dunia.

Gary Lenius hakuwa na bahati sana. Dawa ambayo yeye na Wanda walikunywa ilikuwa ni kemikali tofauti, na ilikuwa sumu.

Ndani ya dakika chache, wote walianza kuhisi kizunguzungu na mwili kuwa na joto kali. walitapika na kuanza kupata shida ya kupumua. Gary alifariki na Wanda alilazwa hospitalini.

Wanda baadae alisimulia kwa nini walikunywa dawa hiyo.

''Trump alisema ni tiba,'' alisema Wanda.

Donald Trump

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Donald Trump

Sumu itokanayo na vileo

Nchini Iran, mamlaka zimesema mamia wamepoteza maisha kutokana na matumizi ya kilevi chenye sumu baada ya tetesi kuwa ina ufanisi katika kutibu virusi.

Afisa kutoka shirika la dawa Kambiz Soltaninejad alisema kuwa hayo ni madhara ya ''habari ghushi kwenye mitandao ya kijamii.''

Katika tukio moja mtoto mwenye umri wa miaka mitano nchini humo alipofuka macho baada ya wazazi wake kumnywesha pombe katika jaribio la kupambana na virusi vya corona.

''Tunajua kuwa taarifa mbaya huharibu maisha,'' anasema Clare Milne, makamu mhariri wa shirika la fact-checking nchini Uingereza.

Maafisa wa Iran

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maafisa wa Iran

'Rafiki yangu alikula sabuni'

Rais Trump alikisia kuwepo kwa idadi kadhaa ya dawa za tiba mbali na hydroxychloroqine. Mwishoni mwa mwezi Aprili, alisema kuwa tiba ya kemikali inaweza kudhibiti virusi vya corona.

''Kisha ninaona kemikali huweza kuua vijidudu dakika moja. Dakika moja. Je tunaweza kufanya hivyo kwa kuchoma sindano?''

Dkt Duncun Maru wa hospitali ya Elmhurst jijini New York, alisema wafanyakazi wenzake waliwatibu wagonjwa ambao waliumwa sana baada ya kutumia kemikali za kuua wadudu.

''Dawa hizi zinaweza kuwa na athari za muda mrefu, kama vile saratani na athari katika mfumo wa umeng'enyaji chakula,'' anaeleza.

Dkt Duncan Maru
Maelezo ya picha, Dkt Duncan Maru

Kuchoma moto na mashambulizi

Nadharia za uongo zimekuwa zikistawi kupitia mitandao ya kijamii. hasa zinazohusu virusi vya corona- nyingi zimekuwa mitandaoni na kusababisha vitendo vya kuchoma mali na mashambulizi.

Nchini Uingereza, zaidi ya minara ya simu 70 imeharibiwa kwa sababu ya tetesi kuwa teknolojia ya 5G ni ya kulaumiwa kuhusu janga la corona.

Mnara wa simu ulichomwa moto Huddersfield mwezi Aprili

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mnara wa simu ulichomwa moto Huddersfield mwezi Aprili

''Bila shaka angeweza kujaribu kuingia ndani na kunishambulia kama nisingefunga milango haraka,'' alisema Dylan. ''ilikuwa inatisha.''

Aliondosha gari haraka sana. Hakuna aliyekamatwa akihusishwa na tukio hilo.

''Tumeona nadharia nyingi za uongo kwenye mitandao kuhusu mtandao wa 5G,'' anasema Claire kutoka taasisi ya Full Fact. ''tetesi zinasosambaa zikihusu virusi vya corona.''

Mashambulizi na ubaguzi wa rangi

Mwezi Machi, Mkurugenzi wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ameonya kuwa janga la virusi vya corona linaleta ''hatari ya uadui''.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Alikuwa akiangazia suala la ubaguzi dhidi ya watu wa jamii ya Asia na China.

Mwezi Aprili, wanaume watatu waumini wa dini ya kiislamu walishambuliwa kikatili katika matukio tofauti mjini Delhi. Walipigwa baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa waislamu walikuwa wanasambaza virusi.

Katika kijiji Sisai kilicho kidogo Mashariki mwa India, magenge hasimu ya uhalifu yalipambana. Tukio hilo lilitokea siku moja baada ya shambulio dhidi ya mtoto mmoja muislamu kutokana na taarifa za uzushi kuwa waislamu wanasambaza virusi. Kijana mdogo mmoja alipoteza maisha mwingine alijeruhiwa vibaya.

Mwanaume wa kiislamu akiswali mjini Delhi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanaume wa kiislamu akiswali mjini Delhi

Ripoti za uongo zimesambaa katika jamii za kikabila pia. Huko Bradford, Uingereza, uzushi ulienea kuwa wagonjwa wasio jamii ya weupe walikuwa wameachwa wafe.

Na mjini Indore nchini India, madaktari walikuwa kwenye operesheni ya kumtafuta mtu ambaye alikuwa akidaiwa kushambuliwa na mawe kwa sababu alikuwa na maambukizi ya virusi vya corona. Video ya kupotosa kwenye mtandao wa WhatsApp ikidai kuwa waislamu waliokuwa na afya njema walichukuliwa na wahudumu wa afya na kuingiziwa virusi kwa sindano.

Madaktari wawili walijeruhiwa vibaya baada ya tukio la mwanzoni mwa mwezi Aprili.

Kuugua kutokana na taarifa za kupotosha

Taarifa za kupotosha mitandaoni zinaweza kuwa na athari za moja kwa moja, na kwenye mitandao ya kijamii kama vile Facebook ilisema wataondoa machapisho yote kuhusu corona yanayosababisha hofu.

Lakini pia machapisho ambayo yanaweza kuleta athari hapo baadae.

Ruka Facebook ujumbe

Haipatikani tena

Tazama zaidi katika FacebookBBC haihusiki na taarifa za kutoka mitandao ya nje.

Mwisho wa Facebook ujumbe

'Tunapoteza watu wengi kutokana na upotoshaji'

Kutokana na taarifa za uongo zinazosambaa mitandaoni , WHO imeita hali hiyo ''ifodemic'' watu wengi wamepotoshwa na kile wanachokisoma mitandaoni.

Hawajiui kwa kunywa dawa bandia kama tiba, ila wanapunguza uwezekano wa kuishi kwa kufikiri kuwa virusi vya corona si kitu kibaya.

Madktari wanachohofia ni maendeleo katika utafutaji wa chanjo- jambo ambalo litakuwa mafanikio makubwa kwa miaka mingi- njia ambayo inapata changamoto ya kuwepo kwa taarifa za kupotosha.

Mustakabali wa suala hili unaogopesha, wataalamu wanasema kutokana na kile wanachokishuhudia sasa.

''Watu wengi wanapoteza maisha. Hufika hospitali wakiwa katika hatua za mwisho za kuugua'', anasema dkt Fernando mjini NewYork . Ni punde tu amemaliza zamu yake ya usiku, na kama tulivyokuwa tukizungumza kwa Skype, akiwa amevalia barakoa yake. ''Tumewatazama hivi wakipoteza maisha mbele ya macho yetu.''

Brian, mgonjwa wa corona jimboni Florida, ana ujumbe kwa watu wanaoishi kwa kujiwekea dhana za uongo.

''Msiwe wapumbavu kama nilivyokuwa mimi,'' alisema. '' na kitu hichohicho kitawatokea kama ilivyonitokea mimi na mke wangu''.