Virusi vya corona: Mikutano mikubwa ya Kampeni za uchaguzi yaibua hofu ya maambukizi ya virusi vya corona

Jumatatu katika mji wa Gitega watu walikua wemejaa kiasi cha kubaba wakati wa kampeni za mgombea wa chama tawala

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jumatatu katika mji wa Gitega watu walikua wemejaa kiasi cha kubanana wakati wa kampeni za mgombea wa chama tawala
Muda wa kusoma: Dakika 2

Picha zinazoonyesha mikusanyiko ya maelfu ya watu waliokusanyika Jumatatu kwa uzinduzi wa mikutano ya kampeni za kisiasa nchini zimeibua wasi wasi mkubwa ya kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona kabla ya taifa hilo kufanya uchaguzi unaotarajiwa tarehe 20 Mei mwaka huu.

Mikutano mikubwa ilishuhudiwa jana katika mji wa kisiasa wa Gitega ambako chama tawala cha CNDD-FDD, pamoaja na mkoa wa Ngozi uliopo Kaskazini mwa nchi ambako wapinzani wakuu walizindua kampeni zao.

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini humoimetoa sabuni na ndoo kwa wagombea wa uchaguzi ilivitumiwe na wafuasi wao kunawa mikono wakati wa kampeni , wakati mmoja pia kemikali za kuua vimelea pia zilitumika.

Lakini "idadi ya watu waliohudhuria mikutano hiyo ilikuwa kubwa mno kiasi cha kutotoshwa na maji na vitakasamikono vilivyokuwepo " mmoja waliohudhuria mkutano wa kampeni katika mkoa wa Kirundo ameiambia BBC.

Katika mitandao ya kijamii baadhi ya watu walielezea hofu zao huku wakiishutumu serikali kwa kuhatarisha maisha ya watu:

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

'Hakuna tisho la kutosha kuahirisha uchaguzi'

Serikali ya Burundi imefunga mipaka yake ili kuzuwia kusambaa kwa virusi, na kurugusu shehena za malori ya mizigo tu kuingizwa nchini kutoka mataifa jirani.

Ndaniya nchi, watu wameshauriwa kutosalimiana kwa mikono na kunawa mikono mara kwa mara, na maisha yanaendelea kama kawaida.

Taifa hilo limerekodi visa 14 vya Covid-19, na serikali imesisitiza kuwa bado hakuna tisho la kuifanya iahirishe uchaguzi mkuu.

Alipotazama picha za mikutano ya kisiasa, Dkt Olivier Manzi mtaalamu wa mamgonjwa ya maambukiziameiambia BBC kuwa hayo ni maeneo yanayoweza kuwa kitovu cha maambukizi ya virusi vya corona.

Baadhi ya watu waliokua wamehudhuria kampeni za mgombea wa chamacha upinzani cha CNL katika mkoa wa Ngozi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baadhi ya watu waliokua wamehudhuria kampeni za mgombea wa chamacha upinzani cha CNL katika mkoa wa Ngozi

Dkt. Manzi ambaye anafanya kazi katika Shirika la Afya Duniani (WHO), ameiambia BBC kuwa mikusanyiko hiyo ni maeneo yanayosambaza kwa kasi virusi vya corona.

"Kwa mfano nchini Senegal, kulikua na visa vichache mwanzoni lakini baada ya mikusanyiko mikubwa ambayo ilitokea idadi ya visa ilipanda haraka, hii pia imeshuhudiwa katika baadhi ya mataifa mengine " - anasema Daktari Manzi.

Nchini Italia, mechi ya soka katika uwanja wenye uwezo wa kuchukua watu 44,000 wa San Siro tarehe 19 Februari kati ya Atalanta Bergamo na Valencia kutoka Uhispania inaamiwa kuwa chanzo cha kuenea kwa kasi kwa maambukizi ya virusi vya corona kaskazini mwa nchi hiyo.

"Hilo ni bomu lisiloonekana. Hatukujua virusi vinazunguka miongoni mwetu" - Giorgio Gori, meya wa Bergamo aliliambia jarida la michezo la Marca.

Taarifa za corona

Taarifa zaidi kuhusu corona:

Maelezo ya video, Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?