Nguvu ya lugha ya Kiswahili nje ya mipaka ya Afrika Mashariki

Swahili ni lugha ya taifa Tanzania, yenye idadi ya watu takriban milioni 59.7
Kuna zaidi ya lugha 100 zinazongumzwa nchini Tanzania lakini kiswahili kinazungumzwa na asilimia 90 ya idadi ya watu na ni moja ya nguzo muhimu inayounganisha makabila 130.
Kiswahili, kwasasa ni lugha inayotumika shuleni na kwenye biashara.
Ukuaji wa lugha hiyo nje ya Tanzania katika kipindi cha miaka 20 iliyopita kumechangiwa sana na tasnia ya muziki, ambayo imefanikiwa kukabiliana na utofauti wa utamaduni katika eneo hilo.
2017, Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza katika eneo la jangwa la Sahara kuwa na lugha ya Afrika ambayo ni rasmi hata katika mtaala wa elimu badala ya Kiingereza.
Kiingereza kinatumika katika mataifa mengi Afrika na kimekuwa kiungo muhimu kwa mfumo wa mawasiliano katika uchumi wa dunia pamoja na kufungua fursa za ajira na maendeleo ya kisiasa.
Baada ya Tanzania kupata uhuru wake 1964, watoto walitarajiwa kujifunza Kiingereza katika shule za msingi na kujifunza kiswahili katika shule za upili.
Hatahivyo, serikali ya Tanzania ilibaini kwamba watoto wa Tanzania hawakuonekana kunufaika kwa kiasi kikubwa na masomo ya Kiingereza na pia ikawa vigumu kwao kuzungumza kwa lugha ya Kiingereza.
Kilichojitokeza katika kufundisha masomo kwa Kiingereza kilikuwa ni matokeo duni kwa masomo husika, kwahiyo serikali ikaamua kubadilisha kiswahili na kuifanya kuwa lugha rasmi katika mtaala wa elimu.
Swahili na uchumi
Hatahivyo, kulikuwa na wasiwasi kwamba kutumia kiswahili kunaweza kusiwe na tija sana katika kukuza uchumi wa Tanzania ikilinganishwa na kuwasiliana kwa Kiingereza.

"Ni jambo ambalo tunaweza kutamani siku za usoni kwasababu naamini fika kuwa unapozungumzia uwezo wa uchumi, ni lazima uangalie na soko," Amani Shayo, msimamizi wa kampuni ya Empower Ltd, nchini Tanzania, inayohusika na usajili, na utoaji mafunzo kwa wafanyakazi ameiambia BBC.
"Lakini hali ilivyo kwasasa, ambapo kampuni nyingi ni za kimataifa, zinafanya kazi kwa kiwango cha kimataifa na lugha ya mawasiliano ni Kiingereza."
Ili kufikia fursa mpya nje ya nchi na ndani ya Tanzania, Bwana Shayo anaamini kwamba bado kuwa na uwezo wa kuzungumza Kiingereza kwa sasa ni jambo la msingi.
Unaweza kutazama
Ilihali Vyuo Vikuu katika maeneo mbalimbali duniani vimeanzisha kiswahili kama lugha ya kujifunza, huku Afrika Kusini ikiamua kuanza kufundisha lugha hiyo kuanzia shule za msingi.
Vilevile, kiswahili ni lugha pekee ya Afrika ambayo imetambuliwa rasmi na Umoja wa Afrika, ambako pia inaonesha kuendelea kupata umaarufu.
"Ikiwa hutaweza kufahamu lugha moja inayozungumzwa na wengi itakuwa vigumu kufanya biashara. Lugha hii naitambua kama bidhaa, kwasababu tunahitaji kuchapisha vitabu vingi zaidi na kuajiri waalimu wengine wa Kiswahili," amesema Dr Ernesta Mosha, mkurugenzi wa Taasisi ya taifa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kwake yeye, lugha ya Swahili itafanikiwa kuenea na kuwa lugha inayozungumzwa na wengi kwa kupanua uchapishaji, elimu na sekta ya ufasiri.















