Virusi vya Corona: Madai ya wanasayansi kuhusu 5G ni 'upuuzi mtupu'

Dhana zinazodai kuwa teknolojia ya 5G ilisaidia kusambaza coronavirus zimelaaniwa na wanasayansi.

Video imekua ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha minara ya mawasiliano ya simu za mkononi ikiungua katika miji ya Birmingham na Merseyside - sambamba na madai hayo.

Video hiyo imekua ikishirikiswa watu kupitia mitandao ya Facebook, YouTube na Instagram - zikiwemo kurasa rasmi zenye maelfu ya wafuasi.

Lakini wanasayansi wanasema kuwa wazo la uhusiano kati ya Covid-19 na 5G ni "upuuzi mtupu" na lisilowezekana kibaiolojia.

Nadharia hizi zimetajwa kama "taarifa mbaya zaidi feki" na Mkurugenzi wa tiba katika taasisi ya huduma za afya nchini Uingereza Bwana Stephen Powis.

Dhana potofu

Wengi wanaoshirikisha ujumbe huu wanasambaza taarifa potofu zinazodai kuwa teknolojia ya 5G - ambayo inatumiwa katika mitandao ya simu za mkononi na hutegemea taarifa zinazosambazwa na mawimbi ya radio - inahusika kwa namna fulani na coronavirus.

Nadharia hizi zinaonekana kujitokeza kwa mara ya kwanza kupitia jumbe za Facebook mwishoni mwa mwezi wa Januari, wakati mbapo kisa cha kwanza cha virusi hivyo kilipotokea nchini Marekani.

Madai hayo yanaonekana kwa kiasi kikubwa kuwa ya aina mbili:

  • Dhana moja ni kwamba 5G inaweza kuzuia utendaji wa mfumo wa kinga, na hivyo kuwafanya watu kupata virusi kwa urahisi.
  • Madai mengine yanasema virusi vinaweza kwa namna fulani kuambukizwa kupitia matumizi ya teknolojia ya 5G.

Madai haya yote ni "upuuzi mtupu ," anasema Dkt Simon Clarke, profesa wa masuala ya seli za microbiolojia katika Chuo Kikuu cha Reading.

" Wazo kwamba 5G hupunguza mfumo wa kinga ya mwili si swala hata la kuchunguzwa ," anasema Dkt Clarke.

"Mfumo wako wa kinga ya mwili unaweza kupunguzwa na vitu mbalimbali ikiwemo mwili kuchoka siku nzima, au kwa kutokula lishe bora.

Mabadiliko hayo si makubwa lakini yanaweza kukufanya uwe katika hali ya kupatwa na virusi."

Huku mawimbi thabiti ya radio yakiwa na uwezo wa kusababisha joto, 5G si imara vya kutosha kuweza kuwatia joto watu kiasi cha kuleta madhara.

"Mawimbi ya Radio yanaweza kuvuruga saikolojia unapopatwa na joto, ikimaanisha kuwa mfumo wako wa kinga ya mwili hauwezi kufanya kazi ipasavyo. Lakini viwango vya nishati kutoka kwa mawimbi ya radio ya 5G ni vidogo sana na haviko imara kiasi cha kusababisha athari kwenye mfumo wa kinga ya mwili . Hakuna uchunguzi uliokwishafanyika juu ya hili ."

Mawimbi ya radio yanayotumiwa katika 5G na teknolojia nyingine za simu za mkononi hutumia masafa ya chini ya kiwango cha sumaku ya umeme.

Nishati yake ni ya chini kuliko hata kiwango cha nishati ya mwanga wa taa , haina nguvu kiasi cha kuharibu seli za mwili-kinyume na mionzi yenye masafa ya juu ambayo inajumuisha miale ya jua na mionzi ya kimatibabu (medical x-rays)

Haiwezekani kwa 5G kueneza virusi vya corona, Adam Finn, profesa wa matibabu ya watoto katika Chuo kikuu cha Bristol, anaongeza.

"Janga la sasa la coronavirus lilisababishwa na virusi vinavyoambukizwa kutoka kwa mtu mmoja aliyeathiriwa kwa mtu mwingine.

Tunafahamu hili ni kweli. Hata tuna virusi vinavyokuzwa katika maabara zetu, vilivyochukuliwa kutoka kwa mtu aliyekua anaugua.

Virusi na mawimbi ya nishati ya umemeinayotengeneza mawasiliano ya mitandao ya intaneti na simu za mkononi hufanya kazi tofauti. Tofauti yake ni sawa na ya chaki na jibini," anasema.

Unaweza pia kusoma:

Ni muhimu pia kutambua kuwa nadharia nyingine zinazosambazwa kwamba - virusi vya corona inasambazwa katika miji ya Uingereza ambako teknolojia ya 5G haijatumiwa, na katika nchi kama Iran ambazo bado hazijaanza kutumia teknolojia hiyo.

Kulikua na taarifa nyingi za kutisha kuhusu 5G zilizosambazwa kabla ya mlipuko wa virusi vya corona ambazo kitengo cha BBC cha uchunguzi wa ukweli wa taarifa zinazoenea- Reality Check has kilikua tayari kinazichunguza , moja ya taarifa hizo ni kuhusu ikiwa 5G inasababisha hatari za kiafya .

Mapema mwaka huu, uchunguzi wa muda mrefu kutoka kwa Shirika linalosimamia ulinzi wa mawasiliana ya kimataifa yasiyotumia mionzi (ICNIRP) lilipinga madai haya, likisema hakuna ushahidi kwamba mitandao ya simu inasababisha saratani au ugonjwa mwingine wowote ule.

Lakini kile kinachoonekana ni kwamba taarifa potofu zimeongezeka.

Shirika la biashara ya simu za mkononi nchini Uingereza-Trade body Mobile UK limesema kuwa taarifa potofu na nadharia kuhusiana na 5G na coronavirus "zinatia hofu," huku Idara ya Digitali, utamaduni , habari na michezo ikirejerea kuwa "hakuna ushahidi kabisa wa uhusiano huo ".

Virusi huvamia seli za binadamu au wanyama na kuwatumia kuzaliana, ambalo ndilo jambo linalosababisha maambukizi. Virusi haviwezi kuishi kwa muda mrefu nje ya kiumbe kisicho hai, kwa hiyo lazima vitafute njia ya kuingia mwilini- kupitia matone ya makamasi kupitia kikohozi au chafya.

Inaaminiwa kuwa coronavirus iliruka kutoka kwa mnyama hadi kwa binadamu- na ikaanza kusambaa kati ya binadamu na binadamu.

Unaweza pia kutazama: