Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Coronavirus: Kwa nini mashine za kusaidia kupumua ni muhimu kwa wagonjwa wa virusi vya corona?
Serikali za nchi kadhaa duniani zimeagiza maelfu ya mashine za kupumulia kusaidia kupunguza msongamano hospitalini kwasababu ya janga la mlipuko wa virusi vya corona.
Kwa wagonjwa walioathiriwa zaidi na maambukizi haya, vipumuzi ndio suluhisho muafaka vyenye kuongeza uwezekano wa kuokoa maisha.
Je mashine za kusaidia kupumua ni nini na zinafanyakazi vipi?
Kwa kifupi, mashine hii inatekeleza jukumu la kupumua wakati ambapo ugonjwa huu umesababisha mapafu kushindwa kufanya kazi.
Hii inampatia mgonjwa muda wa kukabiliana na virusi hivi na kupata afueni.
Kuna aina mbalimbali ya vipumuzi zinazoweza kutumiwa.
Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), asilimia 80 ya watu wenye virusi vya Covid 19 ambao unasabaishwa na virusi vya Corona wanapona bila ya matibabu ya hospitali.
Lakini mmoja kati ya sita anaweza kuugua sana na kuwa na matatizo ya kupumua.
Katika visa kadhaa kama hivi, virusi hivi vinaharibu mapafu. Mfumo wa kinga ya mwili unabaini kwamba kuna tatizo mahali na kupanua mishipa ya damu ambapo seli zaidi za kinga huingia.
Lakini hili linaweza kusababisha majimaji kuingia kwenye mapafu, na kufanya iwe vigumu zaidi kwa mtu kupumua na hatimaye viwango vya hewa ya oksijeni mwilini kushuka.
Ili kuondoa hili, vipumuzi vinatumiwa kusukuma hewa, na kuongeza kiwango cha oksijeni hadi kwenye mapafu.
Vipumuzi pia vina unyevuunyevu ambao unabadilisha joto ili liweze kwendana na joto la mwili la mgonjwa.
Wagonjwa wanapewa tiba kutuliza misuli ya mfumo wa kupumua na hivyo kupumua kwao kunadhibitiwa na mashine. Watu wenye dalili za wastani wanaweza kutumia mashine hizo kupitia barakoa, na vifaa vingine vya kufunika mdomo na vyuso ambavyo vinaruhusu angahewa au mchanganyiko wa gesi kusukumwa hadi kwenye mapafu.
Pale ambapo mashine inatumika kutoa hewa ya oksijeni na kusukumwa kwenye valvu, mara nyingi inatumika kwa wagonjwa wa Covid 19 pengine kwasababu inapungunza hatari ya usambaji wa virusi kwa kupitia kupumua.
Tiba ya aina hii haihitaji mirija kuingizwa moja kwa moja ndani ya mwili wa mgonjwa mfano kupitia ngozi.
Hatahivyo, vyumba vya wagonjwa mahututi kawaida huwa vinahudumia watu wenye matatizo makubwa ya kupumua ili kuhakikisha kwamba kiwango cha oksijeni mwilini kinaendelea kuwa sawa.
Dr Shondipon Laha, kutoka chama cha kuangalia wagonjwa mahututi, ameiambia BBC kwamba wagonjwa wa Covid 19 hawahitaji mashine ya kusaidia kupumua na pia wanaweza kutibiwa nyumbani.
Lakini ingawa kuna hatari zake iwapo mtu atatumia mashine hiyo, kama vile kutotambua nani atakayepata athari za muda mrefu, amesema, ''wakati mwengine vipumuzi ilikuwa ni njia pekee ya kuhakikisha mgonjwa anapata oksijeni."
Tatizo jingine, Dr Laha ameelezea, ilikuwa ni kuwa na idadi stahiki ya wafanyakazi ambao wanaweza kusimamia mashine zote za kusaidia kupumua zinazotarajiwa kutumika.
"Kupumuzi hiki pia kina madhara yake - kinaweza kusababisha mgonjwa akapata madhara makubwa iwapo hakitasimaiwa vizuri," amesema. "Upande wa kiufundi ni changamoto. Watu wanaufahaumu wa aina mbalimbali ya mashine za kutoa hewa safi katika mazingira mengine lakini huenda wakahitaji usaidizi katika kuzitumia kwenye vyumba vya kuangalia wagonjwa iwapo ni hawana uzoefu".
Lakini Je UK inamashine ngapi za kupumulia - na je ni ngapi ambazo zinaweza kuhitajika?
Mfumo wa afya Uingereza unaripoti kuwa na mashine 8,175 za vipumuzi na kwasasa hivi inahitaji mashine zingine kwa dharura.
Serikali inaamini kwamba hadi mashine 30,000 huenda zikahitajika wakati janga hili litakapofika kilele chake - na imeagiza mashine mpya 10,000 kutoka kwa kampuni ya teknolojia ya Dyson.
Vyanzo vya kampuni ya Dyson vimeiambia BBC kwamba kwasasa wanaunda mashime mpya kabisa ambayo imeshafanyiwa majaribio kwa mwanadamu na kwasasa iko tayari kuanza kutumika".
Pia huenda mashine 5,000 zaidi zikaagizwa.
Kampuni nyengine ya Uingereza ya Gtech, imeunda mashine mpya kabisa ambayo inaweza kutoa huduma hii hata umeme utakapopotea.
Idadi ya kampuni nyingine kadhaa - ikiwemo ile ya muungano wa makampuni ya Airbus, Meggit and GKN pia nayo yameorodheshwa kusambaza mashine za kupumulia kwa kuzingatia muundo uliopo.
Wakati huohuo, timu ya wanasayansi na wahandisi kutoka chuo kikuu cha Oxford na King College London vimezindua mashine zao za gharama ya chini na kusema kwamba zinaweza kuanza kutengenezwa haraka iwezekanavyo.
Na watafiti katika chuo kikuu cha East Anglia wanafikiria kutumia mfumo wa 3D ili kuzalisha vipuri vya mashine ya kusaidia kupumua haraka iwezekanavyo pamoja na barakoa na vifaa vungine muhimu.